Maana ya utumwa wa mapenzi!

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Hii ina maana pana sana, lakini naweza kutoa moja kama mjumuisho wa yote! Utumwa wa mapenzi unaweza kutokea pale, utakapompenda mtu ambaye hana habari na wewe kabisa, yaani unajikuta ukioza juu yake, lakini anakuwa hana mapenzi na wewe kabisa.

Wakati mwingine unaweza ukamshawishi mtu huyo kwa vitu fulani, akakubali kuwa na wewe lakini sio kwa mapenzi ila kwa kuwa kuna kitu fulani atapata kutoka kwako.
Kama ukiruhusu utumwa wa mapenzi, maisha yako ya kawaida, yanaweza kuharibika na kukosa muelekeo! Uwezo wako wa kufikiria utakuwa mdogo ma hata wakati mwingine kupunguza ufanisi wako wa kazi.
Muda mwingi utautumia kufikiri kwanini fulani hakuipendi? Una kasoro gani n.k, kimsingi kama ukiruhusu utumwa wa mapenzi, mpangilio wa maisha yako unaweza kuharika na kukosa muelekeo kabisa.
 
Shobo za mapenzi mbaya sana...yataka moyo kumpotezea mtu unaemfeel si unajua love doesn't ask why
 
Hivi hayo mambo bado yapo siku hizi? na ugumu wote huu wa maisha uache kuwaza utatusua vipi we umwaze fulani. aah mi hapana kwakweli hiyo ilikua sokondarii.
 

Elimu nzuri.
Short and Clear.
 
Hivi hayo mambo bado yapo siku hizi? na ugumu wote huu wa maisha uache kuwaza utatusua vipi we umwaze fulani. aah mi hapana kwakweli hiyo ilikua sokondarii.

Mimi mmoja wapo more thnx 6 yrs hii hali inanitesa nimejaribu nimeshindwa cjielewi kwa kweli
 
Mapenzi wee acha tu, wengine tunakufa na maumivu yetu moyoni. Life goes on

Ngoja nikwambie kitu..
Katika hali ya kawaida huwezi kupambana na maumivu ya mapenzi, nguvu ya maumivu yale ni kubwa mno huwezi kupambana nayo ukiwa unatumia akili yako lazima ikuburuze vizuri sana..

Ila kama unataka kushindana na nguvu ile mshirikishe Mungu katika vita ile uone matokeo yake, itakuwa rahisi sana na wala huwezi kufeel pain kubwa kiasi kile..
Ukimuachia Mungu trust me utasahau katika kipindi kifup sana na hutasikia maumivu hata kidogo..

Note:
Sijaokoka na wala sitegemei kuokoka katika maisha yangu, ila binadamu huwa tunajisahahu sana na huwa tunadhan tunaweza tukatatua matatizo yetu bila msaada wa kiroho..
Mshirikishe Mungu katika maisha yako ya kila siku na hakuna jambo litakalokuwa gumu.
 
Walioko chuoni!

Kumbebea demu chips/msosi kutoka canteen unapeleka hadi ghorofa ya nne! Tena umenunua kwa hela yako.

Huu ni utumwa pia!
 
Walioko chuoni!

Kumbebea demu chips/msosi kutoka canteen unapeleka hadi ghorofa ya nne! Tena umenunua kwa hela yako.

Huu ni utumwa pia
tunapozungumzia utumwa halisi wa mapenzi, ni pale ulipojitahidi kumshawishi mpenzi huyo, kwa kila njia ili nuweze kuwa naye! Inawezekana ulimshawishi kwa pesa na wakati mwingine, ndugu zake walimlazimisha kuishi na wewe, akaamua ingawa hakupenda.
 
Mapenz yanafanya mtu unakuwa mtumwa sana yanaumiza na hayana kanuni

ICHANA Mnapokuwa mmeingia kwenye ndoa, hapo sasa ndipo utumwa hukamilika! Sio rahisi kutoka tena (hasa kwa Wakristo) lakini mume/mke huyo atakuonyesha kila aina ya vimbwanga kuthibitisha kuwa hana mapenzi na wewe.
Inawezekana ukahitaji haki yako ya ndoa lakini akawa mgumu kukupa, kwa sababu hakupendi! Alikuoa/olewa na wewe kwa sababu ya shinikizo na sio mapenzi, lakini kwa kuwa tayari unakuwa umeshazoeana naye inakuwa vigumu kumtoa moyoni mwako.
 
Last edited by a moderator:
Mapenzi bwana ni kama mnyororo unaempenda kuna sehemu anapenda naye aliye pendwa kuna sehemu anapenda kumpata mtu mkapendana sawa sawa ni ngumu.
 
Katika haya mapenzi mtoaji zaidi ni mmoja mwingine ni mpokeaji tuu iwe ni upendo , uthamani , huruma ,hata material things.Inauma sana jamani unatamani mtu akuelewe unavyofeel lakini mtu anakuwa mbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…