Maana ya sanaa

Maana ya sanaa

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
*SANAA NI NINI ?* Kwa maelfu ya miaka sanaa imekuwa ikiendelea kushika uzito katika jamii nyingi za wanadamu huku ikiwa ni msaada katika jamii tofauti sanaa ilikuwepo toka enzi na enzi kabla na baada ya mitume . Mitume walipokuja walikuta sanaa nyingi zikifanyika duniani, walikuta ushairi, nyimbo,? Chezaji, uchingaji, ufinyanzi na nyingine nyingi zikifanyika na hata baadhi ya sanaa zipo katika vitabu vitakatifu vya dini. Sanaa ni neno liliochukuliwa katika msemo wa kiarabu, unaomaanisha *ufundi wa kuwasilisha mawazo yaliyo katika fikra za mwanadamu* , maana ambayo inatumika pia katika kuelezea za nwana sanaa bora ambae anawekeza katika kuelezea maoni yake katika njia iliyobuniwa zaidi. Wengine hutafsiri neno sanaa kama *umbo lililisanifiwa katika ustadi na kusanifika* , sanaa inaweza kuwa katika umbo moja lakini likawa na maane zaidi ya elfu sanaa na kipawa ambacho kila binadamu amepewa kulingana na mungu alivyoamua kumpa kipawa ambacho kama kikitumik vyema kinakuwa na faida sana na kikitumika vibaya kinakuwa nahasara isiyo na mfano. Sanaa ni kipawa kitokacho katika akili ya ndani ya mwanadamu kipawa hiki kina muda maalumu wa kufunguka, kuna ambao watafungukiwa mapema sana na katika umri mdogo, kuna ambai kitafunguka katika umri wa kati, wengine umri wa ujana, uzee na utu uzima. Siyo kila mmoja inakuwa ni rahisi kwake kugundu kipawa chake, wengi wetu tumechelewa kugundua vipaji vyetu kunakotokana na sababu nyingi ikiwemo mazingirq tunayoishi ama tuliyoishi, mfumi wa jamii zetu watanzania nao huchangia katika kuficha vipawa vya watu.
 
First to reply.... Wajuz wakimaliza kula watakuja
 
Ungeweka kwa aya ingependeza zaidi..
 
Sanaa ni yale maisha na mazingira yanayo kuzunguuka.

Hapo hapo ulipo, ukipata bahati ya kuchorwa ama kuchora, ukipata bahati ya Kupiga au kupigwa picha....

Kwa mazingira yoyote, kutokea hapo, tayari utapata maana na tafsiri nzima ya neno SANAA...

ARTS is/its just the way you are and you have.

Mjadala uendelee...!!
 
inawezekana ikawa ni falsafa nzuri kuwa hata mazingita ni sanaa
maana hata watu hufanya sanaa na ubunifu kulingana na mazungira waliyopo ikiwa bi katika njia ya kukabiliana nayo
 
Back
Top Bottom