Maana ya mteja ni mfalme

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Leo mchana niliingia kwenye restaurant moja hapa Moshi mjini inayotazamana na Shree Hindu Temple. Nikaagiza chakula wakaleta baada ya muda mrefu na kuwapigia kelele kwa sababu wahudumu walikuwa wanaangdalia video ya harusi sijui ya nani. Anyway, hiyo si muhimu. Baada ya kula nikashangaa wahudumu wananipita tu, nikashtukia dk 15 zimepita tangu nimalize kula. Nikamwita mhudumu kwa sauti ya ukali
MIMI : we mhudumu weeee
MHUDUMU: sema...
MIMI: Huoni kuwa nimemaliza kula?
MHUDUMU: kwahiyo...
MIMI: Nataka kulipa
MHUDUMU: lipa sasa
MIMI: shi'ng ngapi?
MHUDUMU: elfu tatu mia sita
MIMI: mbona unafanya kazi kama umelazimishwa?
MHUDUMU: hapa hatufukuzi wateja mzee...
 
Mdau - Hio ni kawaida kabisa kwa hizi Bar & Restaurant zetu!!! Huduma kwa wateja ni sifuriiiiiii kabisa!!!!! Kwasasa hata hizi bar za uswasi hususani huku kanda ya kaskazini kuna Wakenya kibao wafanya hizo kazi sababu wabongo hawana customer service skills!

Customer Service ni donda ndugu huku bongo.......
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom