Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 3,542
- 3,451
Leo kuna Dada zetu na Kaka zetu wengi wamenaswa kwenye mtego uliotokana na kuhongwa wakiamoni wanafaidika kumbe ni mtego.
Hongo ni mtego unaofanya kazi kwenye ulimwengu wa kifikra kuliko ulimwengu wa vitu vinavyoonekana na kubainika kupitia milango mitano ya fahamu.
Ili kubaini mitego hiyo sharti mlango wako wa sita wa fahamu uwe wazi na usiingiliwe na vichocheo vya nje.
Unapopokea hongo inakulazimisha kurahisisha uumbaji wa tukio analotazamia aliyekuhonga na hili linafanyika kwa hatari yako au kwa lazima,ni kama inakufanya upekee mitetemo ya nguvu za kiumbaji za aliyekuhonga na kumsaidia kutekeleza kusudi lake.
Kuna watu wameoa,wameolewa au wameoana kutokana na nguvu iliyopo nyuma ya hongo na siyo hongo yenyewe.
Wapo Dada zetu walioolewa kwa hongo za viazi mbatata na kachumbari na wengine kwa soda baridi.Halikadhalika wapo akina Kaka ambao nao leo wamejikuta kwenye ndoa kutokana na hongo.
Hongo ni sawa na sadaka inayotolewa kuwajulisha hitaji la mtu.Kuwa makini sana usipende sana ofa ofa au burebure.Ni James la hatari sana kupokea chochote kwa mtu yoyote bila kutafakari kwa kina na kuruhusu "akili ya akili yako kufanya kazi".
Kuna watu leo ni wamekuwa mateka wa watu wengine kutokana na kushindwa kuelewa nguvu inayoambatana na kile unachopewa na mtu mwingine ni nguvu gani.
Binadamu yeyote anapotoa sadaka makanisani,kwa waganga kusaidia masikini n.k huwa kuna kitu anaambatanisha nyuma ya kile anachotoa"kunuwia"na tunachokiambatanisha kina nguvu na ndicho kinachotakiwa.
Hakuna msaada wa bure"kipo kinachosemwa nyuma ya huo msaada"..hatupaswi kufurahia tunasaidiwa au tunahongwa sana ila tujiulize ni nini kinachoambatana na hongo hizo.
Kuna akina Dada na akina Kaka leo wanatamanj kuolewa na kuoa wanashindwa kwa sababu walishafungwa na nguvu iliyombatana na hongo za watu wengine walizowahi kupokea.Suala hili halihitaji kwenda kwa Mchungaji kuombewa ila kujitathmini kwanza kabla ya kukurupuka.
Hayupo anayotoa kitu chochote bure awe ni matajiri au masikini "kipo anachohitaji"na ndicho anachokiambatanisha na kile anachokupatia.
Unaweza ukaona unapewa gari pesa,ofisi nzuri n.k lakini jiulize ni kipi cha maana kufurahia "Je ni kile kidogo unachoona au kikubwa usichokiona nyuma ya kitu?).