huenda ni kweli hiyo tafsiri ya kiingereza, maana mikoa yote hapa nchini ina boma, ambapo ilikuwa ni makao makuu ya serikali za wakoloni, mainly mwigereza na mjerumani.
lakini, ukiacha tafsiri zote za hapo juu, kwa mikoa mingine kama arusha, boma ni nyumbani kwa mtu yoyote, kwa maana kwamba alijenga na anaishi hapo na familia yake, na panaitwa hivyo kwa kutambua heshima yake zaidi katika jamii inayomzunguka.
au kwa sehemu nyingine wanaita mji wa fulani.