Prosper C Manasse
JF-Expert Member
- Dec 8, 2015
- 635
- 690
"My OUTLOOKs"
* * * * * * * * *
<19/FEBR/2016>
*Upelelezi Ni Uchunguzi Wa Kina Unaofanywa Ili Kutafuta Na Kukusanya Ushahidi Ambao Utatumika Ktk Kutafuta Ukweli Dhidi Ya Tukio Fulani.
*Upelelezi Unaweza Kuwa Na Maana Nyingine Tofauti Lakn Yenye Mlengo Mmoja Tu Kupata Ukweli Wa Tukio Husika.
DHUMUNI LA UPELELEZI.
*Ni Kutafuta Ushahidi Ili Kupata Haki Kwa Mshitaki Na Mshitakiwa Ili Mmoja Asionewe Dhidi Ya Mwingine.
Watu Wengi Wanaposikia Upelelezi Umekamilika Huwa Wanadhani Kwmb Upelelezi Huo Umelenga Kumfunga Mshitakiwa Lakn Si Kweli, Dhumuni Halisi La Upelelezi Kukamilika Ni Kujitosheleza Kwa Vielelezo Ambavyo Vitatumika Kama Ushahidi Mbele Ya Mahakama Dhidi Ya Tukio Zima Ili Haki Itendeke.
FAIDA ZA UPELELEZI.
1. Kujua Ukweli Wa Tukio Na Kupata Ushahidi.
2. Kutenda Haki Kwa Mlalamikaji Na Mlalamikiwa.
3. Kuisaidia Mahakama Kuendesha Kesi Kwa Muda Mfupi Na Haki Kupatikana Haraka.
4. Kupunguza Gharama Za Kuendesha Kesi.
5. Mengineyo.
Mlalamikiwa Akiwa Kituo Cha Polisi Huitwa MTUHUMIWA Lakn Kesi Ikishafika Mahakamani, Jina Mtuhumiwa Hufutika Na Kubatizwa Jina MSHITAKIWA. Jina Mshitakiwa Litaanza Punde Baada Ya Mtuhumiwa Kusomewa Shitaka Lake.
Siku Zote Mlalamikaji Huwa Ndiye Shahidi Namba1 Na Kama Mlalamikaji Amekufa Kisha Kesi Ikafika Polisi Hadi Mahakamani, Basi Shahidi Namba1 Atakuwa Mtu Yeyote Wa Karibu Aloshuhudia Tukio Husika.
Mashahidi Hupangwa Kulingana Na Maelezo Yao Kutokana Na Jinsi Walivyoshuhudia Tukio. Uzito Wa Ushahidi Ndio Hutumika Kuwapanga Kwa Mtiririko Mzuri.
Haijalishi Mashahidi Ni Wengi Kias Gani, Kinachotakiwa Pale Ni Wao Kutoa Ushahidi Unaofanana Na Si Kutofautiana.
Hayo Yote Hapo Juu Ni Kwa Mujibu Wa Sheria Ya Mwenendo Wa Makosa Ya Jinai (Criminal Procedure Act) Na Sheria Ya Ushahidi (Law Of Evidence)
AINA ZA USHAHIDI.
*Kwanza Tutambue Kuwa, Kuna Aina Nyingi Za Ushahidi Ambazo Mtu Anaweza Kushuhudia Mbele Ya Mahakama.
1. Ushahidi Wa Kuona.
2. Ushahidi Wa Matamshi.
3. Ushahidi Wa Kitaalamu.
4. Ushahidi Wa Maandishi.
5. Ushahidi Wa Kimazingira.
USHAHIDI UPI UNAPOKELEWA NA KUKUBALIKA KUSIKILIZWA NA MAHAKAMA?
*Ushahidi Ambao Unakubalika Kusikilizwa Mahakamani Ni Ule Tu Unaondana Na Shitaka Lililopo Mahakamani. (The Evidence Should Be Relevant And Admissible) Lakn Pia Mahakama Inaweza Kukubali Ama Kukataa Ushahidi Fulani Kulingana Na Hatua Za Kiupelelezi Zilizotumika Kukusanya Ushahidi Ama Vielelezo Hivyo.
Mahakama Haipo Tayari Kusikiliza Ushahidi Wa Tukio Ambalo Haliko Mezani Mwake. Kama Ni Wizi Wa Gari Basi Toa Ushahidi Wa Kosa Husika Na Si Wa Wizi Wa Pikipiki.
HITIMISHO.
Kabla Hujapeleka Shauri Mahakamani, Hakikisha Unaushahidi Wa Kutosha Vinginevyo Utapoteza Muda Wako Bure.
KUMBUKA:
Mlalamikaji Ni Chanzo Kikuu Cha Upelelezi Kupata Ushahidi.