Maana halisi ya SWAT .

SWAT hawahusiki na upelelezi. Hawa sio intelligence unit, ni kitengo tu cha polisi chenye mafunzo maalum kwaajili ya kukabiliana na matukio ya uhalifu wa silaha na mapigano ya karibu (close combat).

SWAT hawafanyi kazi nje ya marekani. Hata FBI wenyewe ni mpaka wapewe kibali maalum kwa oparesheni za nje ya Marekani. Ni kazi ya CIA kushughulika na hayo majanga nje ya mipaka ya marekani.

SWAT hawahusiki na ufuatiliaji wa madawa ya kulevya. Hiyo ni kazi ya D.E.A (kwa marekani). Ila hawa D.E.A nao wana kitengo chao cha aina hii ya SWAT.

SWAT hawana makali ya kufikia kufananishwa na Navy seals. Kuanzia mafunzo mpaka uzito wa oparesheni. Kwa marekani labda Delta Force ndio wanaweza kufananishwa kidogo na Navy Seals.
 
Dejavu acha uwongo SWAT ni kikund cha betting kinachohusika na kukusanya mikeka
 
Ndiyo maana SWAT wako zaidi kwenye operation kama za rescue and the like lakini masuala ya investigations huwa ni FBI zaidi.
 
Afadhari umemuelewesha hawa SWAT kibongo bongo tunaweza waita FFU

Wanafanya pale polisi walipoishia
 
Delta Force, Navy Seals au Marine hao mafunzo yao ni ya kijeshi whilst SWAT ni polisi(more like paramilitary).
 
Delta Force, Navy Seals au Marine hao mafunzo yao ni ya kijeshi whilst SWAT ni polisi(more like paramilitary).
Uko sahihi, na pia SWAT sio special force, hawa ni law enforcement unit. Ni wa kawaida sana kuliko baadhi ya wachangiaji wanavyowapamba!
 
Sidhani kama ni sahihi kufananisha SWAT na FFU, labda CRT (Crisis Response Team) kwa Tanzania na RECCE Squad ya Kenya!
Ndio tulivo maanisha Kaka ila tumetolea mfano majukumu ya SWAT kwamba wanafanya pale wanaposhindwa hawa wengine
 
Wewe ndio umenena
 
huyu dejavu inawezekana yupo kwa wagwanda ila hamumuelewi tu.
Tatizo maraia ujuaji mwingi.
 
Afadhari umemuelewesha hawa SWAT kibongo bongo tunaweza waita FFU

Wanafanya pale polisi walipoishia
Kibongo haipo hiyo ... FFU wanalinda masanduku ya kura je kipindi hicho polisi huwa wameshindwa.? Hatuna mifumo mizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…