MAANA HALISI YA NDOA

MAANA HALISI YA NDOA

Alkam Alkam

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2018
Posts
603
Reaction score
512
Ndoa nyingi hazidumu kwa sababu kabla ya kufunga ndoa watu wanakuwa Obssesed na Wedding Ceremony Imaginations, bila kujua Ndoa inaenda mbali zaidi ya hapo

Kuna Ndoa na kuna Harusi...Wengi mnapenda zaidi harusi, na mnapowaza ndoa picha inayowajia ni

Suti kali, Bonge la Shela kutoka Uturuki, Make Up ya ukweli ya bibi harusi kutoka Marekani

Ukumbi Mikocheni, Mashosti kuingia ukumbini na Wimbo wa Wanafiki mkae kimya

HARUSI TU HIYO USIRINGE

HAYA NDOA HII HAPA DADA

Je, umewahi kuwaza Mmeo au mkeo akiumwa miaka 5 mfululizo utaweza kumvumilia?? Umewahi kuwaza Watoto watakapo zaliwa na ulemavu utawa-care namna gani?? Mtakapokosa watoto miaka 6 ya ndoa utahimili kweli wewe maneno ya Mama Mkwe na Mawifi kwamba unawajazia Choo cha kaka yao na huna kizazi?

Ndoa ni zaidi ya Sherehe ya Harusi.
Baada ya yale Matarumbeta kuzimika usiku kifuatacho ni Majukumu mazito na Kiapo kisicho vunjika. Achana na Fantasy za Kwaito,waza mbali kidoogo...

NDOA NI AGANO SIO MCHEZO

Je, Uko tayari kuwa Mme au Mke wa mtu mmoja tu au Ma-Ex watarejea kidogo kidogo kama hupati Satisfaction ya kutosha kwa mumeo? Huwa mnawaza hayo au mnawaza Zawadi ya Kamati itatoa Verossa ya kuanzia maisha?? Sidhani... Kabla ya kuoa na kuolewa jiulize, Unatamani Ndoa au ni tamaa ya Sherehe ya Harusi?
 
Back
Top Bottom