KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 18,136
- 32,836
Mkuu ubarikiwe sana kwa kuchukua muda wako na kuandika kitu chenye mantiki.....hongera kwa hilo.......Mkuu unachanganya mambo.
1. Kama chama kinakataa kupeleka majina hii ni kesi nyingine. Kwanza uelewe Spika au Bunge halihusiki na kesi ya hivi. Kwa sababu Spika anapelekewa jina tu anaambiwa fulani ni Mbunge wa Bunge lako muapishe awe Mbunge(NI AMRI KIKATIBA).. na hana mamlaka ya kuhoji uhalali wake.... japokuwa Mtu mwingine yeyote anaweza kuhoji KWA KUFUNGUA KESI MAHAKAMANI kama vile tu kesi zinazofunguliwa kupinga ushindi wa mbunge fulani aliyetangazwa na NEC.
Hivyo, Kesi hii kimsingi ni kesi ya Tume ya Uchaguzi NEC, kwani tume ndio iliwateua na kumuagiza Spika awapokee kama Wabunge. Swali hapa ni;
Kama tume iliwateua wabunge ambao hawajapendekezwa na chama walipata wapi majina?
Kwa nini CDM hawajaishtaki Tume kwa kuteua Wabunge ambao haijawapendekeza?
Au kuitaka NEC ieleze imepata wapi hayo majina.? (Natambua CDM iliwahi kuomba nyaraka kwa tume lakini ilikaa kisiasa zaidi walipaswa kwenda mahakamni na mahakama ndio iagize tume walete nyaraka husika).
Kwa suala hili CDM walimchafua na kumsingizia sana Spika Ndugai. Kwangu mimi niliona kama ulaghai wa kisiasa uliokuwa unafanywa na Chama.
2. Kufukuzwa COVID 19.
Kwamba Chadema imeacha kushughulika na NEC na imeamua kuwaadhibu walioteuliwa.. sawa;
Hapa pekee kuna walakini..
Jee Covid19 walijiteua?
Nani alipeleka majina yao NEC?
Kama kuna afisa alipeleka majina NEC ni nani?
Ofisa huyo alikuwa na mamlaka hayo kwa mujibu wa Chama?
Ni nani huyo na amechukuliwa hatua gani?
Au Walifoji nyaraka?
Kama walifoji nyaraka kwa nini wasipelekwe mahakamani kwa kufoji wafungwe na Ubunge wao UFE automatically?
Wakifungwa wanapoteza nyadhifa zote chamani na ubunge bila kusumvuka na uanachama wao.
Sijui kama vikao vya kamati kuu na Baraza kuu waliangalia haya. Wameamua kuchukua shortcut kuwafukuza. Sasa covid 19 wameenda mahakamani kuulizia uhalali wa kufukuzwa kwao. Hii ni fursa kwetu tusiojua ukweli kujua kinachoendelea
Ni tume waliwaingiza kibabe
Ni kina Mdee walifoji na kuwadanganya tume na kuwasaliti Chadema?
Kuna kiongozi aliwasaidia ndani ya Chadema na wanatuchezea shere!! na hatimae tujue walifukuzwa kihalali?
Je ubunge wao ni halali au sio halali?
Kama hakuna faulo ndani ya Chama basi chadema walipaswa kufurahia sana hawa kina Mdee kwenda mahakamani kwani kufanya hivyo ni kuweka ukweli Hadharani.. Kuiumbua tume na serikali kwa ujumla na kuonyesha usaliti wa kina Mdee.
Mimi nadhani nadhani CHADEMA insider watakuwa wanajua kinachoendelea isipokuwa wameamua hili suala kulipeleka kisiasa kama ajenda zingine za kisiasa...... CHADEMA Kuna watu wenye weledi na wasomi ambao najua bila wanalijua jambo hili......
Wao kama chama wanatakiwa kuwa wapole wakati huu ambapo jambo lipo mahakamani....kulalamika na kushinikiza jambo lolote zuri upande wao...kunafanya watu wawatilie mashaka kwamba hofu yao Nini........bahati mbaya hili suala linabebwa kwenye jamii kimihemko....hivyo kutunyima taarifa sahihi wadau....