Maamuzi ya mwisho - Simulizi

Barackachess

Senior Member
Sep 1, 2018
156
121
SEHEMU YA KWANZA
Kanisa lilibaki na mshtuko mkubwa waumini nao hawakuamini tukio waliloliona mbele ya macho yao. Padri alibaki akiwa amezubaa hakujua nini kinaendelea kanisani hapo
pindi Laurance alipo kataa kumvisha pete Nasra kwa sababu ya barua aliyoikuta ndani ya koti lake la suti pasipo kujua ni nani aliye husika kuiweka. Alichukua uamuzi wa kuisoma na kusitisha zoezi la kumvisha pete Nasra mara baada ya kuona jina la mpenzi wake wa zamani likiwa limeandikwa mbele ya barua hiyo.

Msimamizi wake alijaribu kumzuia asiendelee kuisoma lakini Laurance alionyesha sura ya ukali na hasira na kuendelea kuisoma barua. Waumini wote waliokuwepo kanisani hapo walibaki kimya kwa muda huku wengine wakiwa wanateta kwa sauti ya chini. Wangu mpendwa wa nafsi; Naomba msamaha kwa wale wote nilio wakwaza katika historia hii ya maisha yangu naomba msamaha kwa mama yangu mzazi japo ametangulia mbele ya haki lakini naimani kuwa malaika wanasikia sauti yangu na jinsi nafsi yangu inavyo umia na ujumbe huu watakufikishia.

Naomba radhi kwako mpenzi Laurance japo natambua kuwa itakuwa ngumu kwako kuelewa kwa nini nimeamua kuchukua uamuzi huu mgumu. Naomba utambue tu kuwa nimeamua kufanya hivi nikiwa na akili yangu timamu na ninaamini kuwa mwisho wa simulizi hii sitakuwa na wewe tena maishani.Najua jinsi gani nafsi yako inavyaumia hata mimi huku niliko moyo unaniuma na najutia sana maamuzi haya lakini naomba ukubaliane na ukweli huu na nitaomba mara baada ya kifo changu usambaze ujumbe huu kwa jamii kwa njia yoyote ile iwe magazeti, mitandao ya kijamii,blogs,website hata makala mbalimbali ili watu waweze kujifunza na kuelimika kwa kupitia mimi na wasije kuyarudia makosa kama niliyo yafanya kwenye maisha yangu.


Kipenzi rafiki yangu Regina ndiye ajuae historia yote ya maisha yangu tangu siku ya kwanza nilipowasili katika jiji hili la Dar es Salaam mpaka leo hii nikiwa nimebakiza siku moja ya kuishi juu ya uso huu wa dunia japo naye hatambui kama sitakuwa nae tena juu ya uso huu wa dunia. Najua leo ni siku yako ya harusi na nilitamani kama ningeolewa na wewe kwa sababu mapenzi yetu yameanza tangu zamani lakini nina sikitika kwa kuwa malengo yote tuliyopanga tangu kipindi cha mapenzi yetu hadi uchumba wetu hakuna hata moja lililo timia.Nakupenda sana Laurance lakini sina budi kukuacha tutaonana tena Paradiso kwenye mji wa milele mungu akipenda.Sina cha kukupatia japo nilikuahidi mengi zaidya niliyokupatia lakini sitaweza kufa pasipo kukuachia japo kitu cha shukrani. Nadhani Regina atakupatia kitu kitakacho kufanya unikumbuke daima na huu ndio UAMUZI WANGU WA MWISHO.

**********​

Haya yalikuwa maneno ya mwisho yaliyoachwa na Janeth siku moja kabla ya kifo chake kutokea.Barua hii ilimkamata vilivyo Laurence pale kanisani alipokuwako siku ya
harusi yake.Alishindwa kuendelea kuisoma barua hiyo na kuanza kulia kwa uchunguhuku akivua koti lake la suti nakuanza kukimbia mbio mpaka kiti cha mwisho cha kanisa sehemu aliyokuwa ameketi Regina. Watu wote kwenye harusi hiyo walibaki wakiwa wanashangaa na kutojua ile barua aliyoikuta kwenye mfuko wa koti lake la suti ilikuwa
imebeba ujumbe gani? Je ni nani aliye husika kuiweka?


MWANZO

Saa moja na robo asubuhi Laurance anaamka na kumuangalia mpenzi wake aliyekuwa pembeni ya ubavu wake akiwa bado amelala fofofo. Kichwa chake kilikuwa
kimetawaliwa na mawazo mengi sana juu ya upatikanaji wa pesa katika siku hiyo. Maisha ya wawili hawa yalikuwa ni maisha duni yakitawaliwa na kila aina ya umaskini,
Njaa, maradhi, maadui, na chuki hivi vyote kwa pamoja vilikuwa ni sehemu katikamaisha yao waliyokuwa wakiyaishi.

Licha ya ugumu huu wa maisha Janeth alionesha kukubaliana na kila hali waliokuwa wakipitia na mpenzi wake na kuridhika na kidogo wakipatacho.Hakuna kati yao
haliyewai kufikiria kumkimbia mwenzake kwa sababu tu ya maisha waliyokuwa wakiishi. Siku zote waliweka imani ya kuyashinda maisha hayo waliyokuwa wakiishi.
Jua lilizidi kupanda katika uso wa ardhi ya dunia. Akiwa bado kitandani hatambui wapi anaweza kujipatia riziki katika siku hiyo alihisi kitu kipya moyoni mwake. Haikuchukua muda mrefu sana Janeth akawa ameamka na macho yao yakagongana kwa kutazamana.

‘’Umeamka salama?’’ Laurance alimuuliza Janeth kwa kumuangalia usoni mwake

“Nimeamka salama hofu kwako’’

‘’Hali yangu kama unavyoiona nipo salama”

Ukimya ulitawala kati yao kwa dakika kadhaa kila mtu akiwa anatafakari mambo yake.Janeth akamsogelea Laurence karibu.Uso wake ulionyesha wazi kwamba anajambo moyoni analotaka kumueleza.

“Laurance”


“Naam nipo hapa nakusikia’’ Aliitika huku akiitazama sura ya Janeth iliyokuwa katika kifua chake.

“Kuna jambo nataka kukushirikisha”

“Lipi hilo mpenzi”

“Ni juu ya maisha yetu haya tunayoishi. Natamani sana na sisi siku moja tuje kuishi
kwenye nyumba nzuri, Tukiwa na familia yetu bora yenye furaha’’

“Nikweli lakini mawazo hayo yatabaki kama ndoto nahisi maisha yetu tumepangiwa
umaskini sijui miujiza gani itatokea kuja kuyabadilisha maisha yetu haya tunayoishi’’

“Nataka kujihusisha najambo fulani lakini lita gharimu kiasi kikubwa cha pesa na mpaka

sasa sijui nitakipata wapi hicho kiasi cha pesa?”

"Ni kitu gani hicho na kitagharimu kiasi gani cha pesa na lini kinatakiwa?”

“Kinagharimu pesa nyingi isitoshe sio hapa kijijini kwetu ni nje ya mkoa huu wa
Mwanza.Kita gharimu kama shilingi laki sita na nusu. Nataka nikashiriki SHINDANO LA
MITINDOaa litakalo fanyika Dar Es Salaam mwishoni mwa mwezi huu”

“Janeth umeshanza kengeuka na maisha ya hapa kijijini. Yani kwa akili zako zote
ulizofikiria umeona hilo swala ndilo litakalo tuingizia pesa na kuyabadili maisha yetu
haya tunayoishi hapa kijijini? Hayo mashindano ni wizi mtupu ebu fikiria SHINDANO LA
MITINDO unadhani ni nchi ngapi zitashiriki eeh? Kutakuwa na wasichana wangapi
wenye vigezo zaidi yako eehh? Huko ni kupoteza muda na unaufanya ubongo wako
kuwa na akili mgando katika kuchanganua mambo ebu jikuze kidogo janeth aggghh”

Aligundua kwamba wazo lake halikumfurahisha japo nafsini mwake kulidhamiria ushindi katika mashindano hayo makubwa na ya kimataifa iwapo kama atapata nafasi ya kushiriki. Alitamani Laurance aelewe kusudi alilo nalo. Lakini dalili za mwanzo tu zilionyesha kuwa mawazo yake yalionekana hayana umuhimu mkubwa katika kichwa na akili za Laurance. Hakutaka tena kuendeleza mazungumzo hayo kila mtu alibaki kimya akitafakari mambo yake akilini mwake. Jua lilizidi kupanda na muda nao ulizidi kusogea ndipo Laurance akaamka kutoka katika kitanda chake na kuchukua kipande cha mti na kukitumbukiza kinywani mwake tayari
kwa kuswaki na huu ndio ulikuwa mswaki wake kila siku.


Mara baada ya kumaliza kupiga mswaki akachukua nguo zake zilizokuwa zimelundikwa kwenye kapu lao la kuifadhia nguo zao kisha akavaa tayari kwa safari ya kwenda
kutafuta fedha.

‘’Mimi na kwenda tutaonana baadae’’

‘’Sawa miangaiko mema’’

Mara baada ya kumuaga mpenzi wake chapuchapu aliondoka na kuingia mtaani kwa ajili ya kutafuta riziki ya siku. Laurance alikuwa na marafiki zake wawili aliokuwa akishirikiana nao katika mambo mbalimbali mmoja alikuwa akiitwa Kelvin na mwingine Desmond wote hawa kwa pamoja walikuwa hawana shughuli za kufanya hapa kijijini. Umasikini na ujinga ndivyo vitu vilivyo watawala kichwani mwao mara nyingi walikuwa wakishinda virabuni wakinywa pombe za kienyeji kwa pesa walizo zipata katika shughuli zao zisizo za halali kama wizi wa mifugo, uporaji na uvamizi katika maduka ya ushirika hapa kijijini.

Mara nyingi walikuwa wanapenda kukutana kwenye virabu vya pombe na kupanga mikakati yao ya kutafuta pesa kwa nguvu.Laurance hakuipenda tabia ya marafiki zake
mara nyingi aliwaonya na kuwataka wabadilishe mienendo yao ya maisha kwa pesa walizo zipata kwa kuwekeza katika maswala ya kilimo ili waweze kujitengenezea pesa
halali lakini ushauri wake ulionekana sio kitu chochote kwenye bongo zao. Siku hii ya leo walikutana katika kilabu kimoja kilicho na umahalufu mkubwa sana hapa
kijijini kijulikanacho kwa jina la Masetu.

Kama ilivyo kawaida siku zote pindi watakapo kutana walikuwa wakipanga mikakati ya shughuli za kiuhalifu kwa kutafuta pesa kwa kutumia nguvu ya miili yao ili kuyaendeleza maisha yao hapa kijijini. Wakiwa wanaendelea na mazungumzo yao kwa mbali walimuona Laurance akija huku uso wake ukionekana umegubikwa na mawazo mengi kana kwamba amekerwa na jambo fulani huko atokako.

‘’Oya Kelvin Yule anaekuja si Laurance?”

“Ni yeye sijui amekuja kufanya nini hapa kilabuni kwa ninavyo mjua mimi jamaa hanywi
wala havuti na huwa apendelei kukaa na walevi sasa sijui leo kulikoni??”

“ Pengine ana tatizo namuona kama hayuko sawa”

“Tena huyo anaisogelea meza yetu tumpuuzie kama anashida atatuambia”

Laurance moja kwa moja aliisogelea meza waliyokuwa wameketi Kelvin na Desmond alikisogeza kiti kilichokuwa kando yao na kuketi pamoja nao. Wote walimtazama kwa sekunde kadhaa kisha wakamcheka kwa dharau kicheko kilicho mfanya Laurance ajisikie vibaya na kunyanyuka kwenye kiti alicho kuwa amekaa na kutaka kuondoka
zake.

“ah-aaaahhh bwana wewe unakuwa unakosea sana unanyanyuka unakwenda wapi? au sisi sio vijana wenzako??”(Desmond aliongea maneno hayo huku akiwa amemdaka mkono ili kumzuia asiweze kuondoka


“Siwezi kuendelea kukaa mahala hapa”

“Tulia usiwe pupa haya mambo ni madogo ni kitendo cha kufikiri tu?”

Alirudi kuketi kitini huku akiwa na mawazo mengi kichwani mwake. Mawazo yake yalikuwa ni juu ya namna ya kupata pesa kwa lengo la kujikomboa na hali ya umaskini
walio nao yeye pamoja na mpenzi wake Janeth. Alitambua kuwa shughuli wafanyazo rafiki zake si shughuli za halali lakini maji yalisha mfika shingoni na hakuna mtu
mwingine ambaye ataweza kumpatia msaada wa pesa za chapuchapu hapo kijijini kama sio Desmond au Kelvin.

Lilikuwa ni jambo gumu kwake kueleza shida na matatizo yanayo msibu na hii ni kutokana na yeye kuwa ni mpingaji wa kwanza katika harakati zao za kuchocheana
katika shughuli zao za kiuhalifu. Muda wote alionekana akiwa ameinamisha kichwa chake chini huku akitafakari ni wapi agusie ili aweze kuyaeleza kwa kina mambo haya yanayo mtatiza kwa marafiki zake ambao kwa wakati huo walikuwa wakiji starehesha kwa kunywa gongo (POMBE HALAMU)

“Laurance vipi ndugu yangu mbona upo hivyo leo? Unaonekana kama unamawazo mengi! sina uhakika kama huko utokapo ni salama kwa maana nyie watu mnaoishi na
watoto wa kike huwa hamuishiwi shida za hapa na pale hebu tukusaidie walau chupa tano za gongo upunguze mawazo” Kelvin aliongea maneno hayo huku akimuita muhudumu kwa lengo la kumuagizia pombe Laurance lakini Laurance alikataa kata kata kunywa pombe kwa sababu huwa hana mazoea ya kunywa pombe. Kitendo hiki kiliwakera Desmond na Kelvin hali iliyo sababisha kumpa hofu na mashaka na kuhisi pengine hataweza kusaidiwa endapo ataeleza matatizo yake bila kunywa pombe lakini alijipa moyo.

Haikuchukua muda mrefu aliaanza kuwaeleza sababu zilizo mfanya atoke nyumbani kwake asubuhi na kufika kilabuni hapo kwa lengo kubwa la kuwatafuta ili aweze kuwaeleza shida zake zinazo mtatiza kama kuna uwezekano wa kupatiwa chochote aweze kupata msaada kutoka kwao. Aliwaeleza jinsi gani hali ya kimaisha kwake inavyokuwa ngumu kwa upande wake kiasi kwamba anakosa hata pesa ya chakula kitakacho watosha yeye pamoja na mpenzi wake kwa siku. Jambo kubwa juu ya yote alichokuwa anafikiria na kukihitaji ni kupata kiwango kidogo cha pesa kitakacho muwezesha kuanzisha shughuli yoyote hapo kijijini
iwe ni kilimo au ni biashara yoyote itakuwa inampa uhakika wa kumuingizia kiwango fulani cha pesa.

Aliwaahidi kama atasaidiwa basi atajitahidi faida atakayokuwa anaipata kwa kitu atakacho kianzisha nusu yake atakuwa akilipiza deni hilo taratibu atakalo kopeshwa
kutoka kwao. Walimsikiliza kwa umakini maneno yake yaliwaingia katika akili zao kila mmoja akiweka nia ya kumsaidia moyoni mwake kwa sababu alikuwa akionyesha hali ya uhitaji sana wa pesa kwa wakati huo.

“Laurance hii dunia ni duara fanya ufanyalo lakini tambua akilini mwako kuwa utarudi palepale. Umeona sasa leo hii umetuona sisi kama dhahabu inayomeremeta katika mchanga wa jangwani lakini zamani sisi ulikuwa unatuona kama hatuna maana kwako haya sasa leo umejileta mwenyewe na kutueleza hiyo mijitatizo yako. Ni sawa shughuli tuzifanyazo sio halali lakini unatakiwa ujifunze kula na vipofu na sio kututenga kama ulivyotutenga wewe’’

Ilikuwa ni sauti ya Desmond inayokwaruza kwa ukali wa pombe anayokunywa.Laurance alibaki kimya hakuwa na neno lolote la kuwajibu zaidi ya kusubiri kama ataweza
kujibiwa ombi lake.

“Tumekubali kukusaidia ila na sisi tutaomba utusaidie”

Laurance alionyesha tabasamu kubwa alipo ahidiwa kusaidiwa japo moyo wake haukujua ni nini hasa na wao wanachotaka wasaidiwe wakati yeye hana kitu?

“Asanteni kwa kusikiliza ombi langu lakini ni nini mnachotaka niwasaidie?”

“Usijali ni jambo la kiujasiri kidogo na endapo utafanikiwa kutusaidia hizo pesa sisi tutakupatia na tutakuongezea nyingine zaidi kama shukrani na wala hatuta kudai kiasi chochote kile hapo baadae”

“Naanza kuingiwa na woga nielezeni basi niondoe wasiwasi moyoni mwangu”

“Laurance kama utakuwa katika hali ya wasiwasi hakika hiki kitu hutaweza kutusaidia kabisa, Tunahitaji uwe jasiri na mwenye moyo mgumu kidogo ili tufanikishe hili jambo.Upo tayari katika hilo?”

Allipata mgogoro wa nafsi katika kujibu moja kwa moja ombi alilo ombwa. Moyo wake ulikuwa mgumu kutoa jibu la haraka haraka ukizingatia kazi walizo kuwa wanafanya
rafiki zake hazikuwa ni kazi halali. Nafsi na fikra zake zilikuwa bado zinasita kuchukua maamuzi ya haraka kujibu alichoulizwa.Alikuwa bado hatambui nini cha kufanya aliamua kuchukua uamuzi waharaka haraka wa kukubali mawazo ya rafiki zake ili aweze kusaidiwa.

“Nipo tayari”

Desmond na Kelvin walimtazama kwa umakini wa hali ya juu pindi alipokubali wazo lao. Ndipo Kelvin akakata ukimya uliopo kwa kumuuliza swali Laurance.

“Safi sana kiukweli umeonyesha moyo wa ujasiri na ushupavu sasa nafikiri muda umefika wa wewe kutatua shida zako na uhakika kwa hili dili la leo tutakalo kwenda kulicheza nilazima uyamalize matatizo yako yote nafikiri hata shemeji yetu nyumbani akiona unarudi na donge la pesa ni lazima atazidisha mapenzi kwako.Si unajua tena msichana mzuri kama yule anahitaji matunzo. Tuachane na hayo kuna kitu nataka kujua kutoka kwako nataka tu nisibitishe kama fikra zangu zipo sawa. Hapa wote tulipo mimi na Desmond hatujui kuendesha gari vipi mwenzetu unaujuzi kidogo?”

Mawazo yake yalimfikirisha labda pengine Kelvin aliuliza hivyo pengine anataka amtafutie kazi ya udereva wa magari makubwa. Lakini bado alikuwa hana uhakika juu ya fikra zake hizo. Aliwajua vyema rafiki zake kwamba dili lao kubwa lilikuwa ni matendo maovu na hakupenda kabisa kuwa nao karibu lakini kutokana na shida na matatizo ya kifedha ilimbidi tu awatafute.

“Ndio ninao uwezo wa kuendesha gari la aina yoyote hata trekta pia naweza”

“Safi sana wewe utatufaa sana siku ya leo. Kikubwa tunachokuomba uzingatie na usikilize kwa makini haya tunayo kuambia hapa ifikapo leo saa sita ya usiku wakati watu
wote wa kijiji hiki wakiwa wamelala tunaomba tukutane katika msitu wa Masetu kule karibu na barabara ya mabasi yaendayo Dar es salaam tunahitaji msaada wako wa kutufikisha Nyakato usafiri tunao”

Moyo wa Laurance uliogopa sana hakuelewa ni kwa nini alihitajika usiku mzito kama huo. Tena wanakijiji wote wakiwa wamelala? Ili mbidi tu akubali kwa sababu alikuwa na shida sana ya kifedha hivyo chochote utakacho ambiwa ilimbidi akubali.Kitu kilicho kuwa kina mtatiza na hakuwa na uhakika nacho ni juu ya usafiri wanao usemea.

“Sawa na ahidi sita waangusha na nitatekeleza kila mlicho niambia siku ya leo mahali hapa”

Desmond na Kelvin walilipokea jibu ilo kwa furaha kubwa sana shughuli waliyokuwa wanahitaji kukamilisha usiku ilihitaji mtu mwenye uwezo wa kuendesha gari kwa sababu walihitaji kufanya jambo moja zito litakalo waingizia mamilioni ya pesa na jambo hilo litawahitaji watembee kilomita 147.5 kuanzia hapo kijijini walipo.

Usiku wa saa sita giza nene likiwa limetawala juu ya uso wa dunia. Watu wote kijijini hapo walikuwa wamejifungia makwao na familia zao wakiwa wamelala fofofo sababu ya uchovu wa shughuli mbalimbali za mchana hasa kilimo. Hakuna kiumbe kingine zaidi ya popo kilichokuwa kinakatiza katika anga na ardhi ya kijiji hicho.

Laurance aliamka huku akiwa amemuacha mpenzi wake kitandani akiwa amelala. Kichwa chake kilikuwa kimedhamiria kupata pesa katika siku hiyo endepo tu
atawasaidia rafiki zake kuwapeleka eneo wanalo taka. Kichwa chake kilifikiri kama atapata hizo pesa umaskini kwake unaweza kuisha na akaonekana mtu wa thamani. Janeth alikuwa bado haelewi ni nini kinaendelea. Yeye alichokuwa akifikiri kichwani mwake ni labda pengine mpenzi wake alikasirika sana na
wazo lake la kushiriki shindano la mitindo (modelling ) alilo mueleza asubuhi.Alidhani labda kuamka kwake huko ni kutokana na kukosa usingizi sababu ya hasira alizo nazo
kwa sababu asubuhi hawakuagana vizuri.

“Kuna nini mbona leo umeamka usiku na mbona unavaa viatu una kwenda wapi? Halafu tangia asubuhi tulipo achana nakuona haupo sawa nini tatizo?” Laurance alipuuza maswali ya mpenzi wake na hakutaka kumjibu chochote aliamini endapo akimjibu maswali anayomuuliza mawazo yake na kumueleza aendako anaweza kushawishiwa asiondoke. Aliendelea kuongea na kumuuliza maswali mengi lakini hakuna hata moja alilojibiwa. Hakuelewa ni kwa nini ameamua kutomjibu maswali yake.

Muda nao ulizidi kusogea hatimaye akawa amemaliza kujiandaa akamtazama mpenzi wake kwa huruma nyingi huku machozi yakiwa yana mlenga.

“Mimi naondoka tutaonana asubuhi”

Janeth akakurupuka kitandani na kwenda kufunga mlango na komeo ili asiweze kuondoka mpaka ajue ni wapi anapoelekea. Alipofika pale mlangoni alimtazama Janeth
kwa macho ya huruma yalio lengwa na machozi kwa mbali.

“Ungejua ya kwamba naondoka kwa lengo ya kutengeneza maisha yetu bora hakika usinge nizuia hapa mlangoni.Nakupenda sana Janeth sijapenda mimi kuondoka muda huu lakini imenibidi tu tafadhari niruhusu niondoke nafikiri asubuhi nitakueleza kila kitu”Janeth maneno hayo yalimpenya vilivyo masikioni mwake na kujikuta akiachia mlango na kumpisha.

“Lakini Laurance napaswa kujua na unakwenda wapi?” Laurance bado alionyesha msimamo wake. Alichofanya ni kumkumbatia na kumbusu kwenye paji la uso wake na kuanza kuondoka.

“LAURANCE………LAU…..LAURANCE……LAURANCEEEEEEEEE……………………..” Janeth alimuita lakini Laurance hakuitika aliendelea kukaza mwendo na kupotelea
gizani na kumuacha Janeth akiwa na masikitiko na msongo wa mawazo huku akilia. Baada ya dakika 45 tayari alikuwa ameshafika katika msitu alio ambiwa akutane na rafiki zake. Msitu ulikuwa unatisha sana sauti za vyura wa ardhini ndizo zilitawala msituni hapo. Hapakuwa na dalili yoyote ya kuwepo mtu katika eneo hili na hapo ndipo hofu ikaongezeka maradufu.

Wakati akiwa anaendelea kuzubaa na kushangaaa huku na kule ghafla mwanga wa tochi ulimmulika usoni. Macho yake hayakuweza kujua ni nani aliye mmulika hii ni kutokana na mwanga mkali kuwaka kwenye macho yake

“Usiogope ni sisi Kelvin na Desmond fanya haraka twende barabarani”

Alipata matumaini mapya baada ya kugundua kuwa waliokuwa wakimuwashia tochi ni Desmond na Kelvin. Walianza kukimbia mbio huku wakiruka vichaka na mifereji ya maji machafu. Walikatiza kwenye mashamba ya watu bila kujali mazao yaliyo pandwa. Mwendo walio kuwa wakikimbia ulikuwa si mwendo wa kawaida ulikuwa ni mwendo
mkali kama wakimbiaji wa mbio za olimpiki nchini Beijing.

Hakuelewa kwa nini rafiki zake hao walitaka wakimbie! Hakupata jibu ilimbidi tu afuate amri. Baada ya dakika kumi wakawa wamefika kwenye pango fulani pango lilikuwa na giza kali mno wakawasha tochi na kuingia.

“Laurance unaliona hilo begi chukua vaa mgongoni na sisi tuna mabegi yetu haya hapa mawili tutavaa mgongoni. Haya mabegi yana nguo ndani za kubadilisha usiwe na
wasiwasi utaelewa baadae kwa nini tunakupa begi?” Laurance akavaa begi mgongoni wakati huo Kelvin alikuwa akiangaika kufukua ardhini na hatimaye akatoa bunduki mbili aina ya AK 47 pamoja na bastola moja.

“Chukua hii kwa usalama wako huko tuendako” Kitendo cha kukabidhiwa bastola kilimshitua sana. Hapo ndipo moyo wake ulipozidi kuogopa. Kelvin akafungua sanduku jingine lililo kuwa pembeni ya lango la pango akatoa OVERLORY tatu za bluu pamoja na soksi za kuziba nyuso zao zilizoachia sehemu ndogo tu ya macho.

Baada ya dakika kadhaa wote wakawa wamekwisha vaa mabegi yao mgongoni tayari kwa kwenda kufanya tukio la ujambazi. Laurance hakutegemea alicho kiona. Mawaazo ya alicho kuwa anafikiri na anachokiona hivi sasa vilikuwa ni vitu viwili visivyo shabiana.

“Lakini hamkuniambia kama mnataka msaada wangu kuwasaidia katika shughuli zenu hizi. Mlicho niambia niwasaidie kuwapeleka sehemu fulani mnayo ijua nyie na usafiri mkasema mnao sasa kwa nini mnanitaka na mimi nifanye kazi zenu. Kama ndivyo hivyo sipo tayari kuungana na nyie na sihitaji tena msaada wowote kutoka kwenu?”

Desmond alipandwa na hasira na kumsogelea kwa umakini Laurance na kumkunjiasura ya kikatili kiasi cha kumtisha Laurance.

“Sikia nikwambie cheza na kila kitu ila usicheze na akili zetu. Endapo kama utaleta jeuri tutaitawanya roho yako na mwili wako tutauwacha hapa hapa uliwe na wanyama wa msituni. Hivyo basi ni lazima utii amri tutakayo kuambia fuata sheria zetu bila shuruti lasivyo hatuta kuwa na huruma na wewe na hatuta jali unatufahamu kiasi gani tutakuangamiza kama tuangamizavyo wengine”

Hofu ilimzidi, alijihisi kujiingiza kwenye matatizo zaidi alishindwa kuelewa atawezaje kujiondoa kwenye mikono yao.Alijiona kama mtekwa. Ilimbidi tu asikilize na kutii amri
zao.

“Ulishawai kumwaga damu ya binadamu mwenzako??”

“Hapana” (alijibu)

“Basi leo utajua tu lasivyo huko tutakapo kwenda usipokuwa makini roho yako utaiacha huko huko”

Hakuamini kama rafiki zake wanaweza wakawa na roho za kinyama kiasi hicho. Walitembea kwa miguu zaidi ya mita mia moja na hatimaye wakafika kwenye barabara
kuu ya magari yaendayo Dar es salaam. Barabara ilikuwa nyeupe. Hakuna gari wala pikipiki wala mtembea kwa miguu aliye katiza njia yote ilikuwa ni nyeupe.

“Laurence hapa inatubidi tupange mawe barabarani ilituweze kuliteka gari lolote litakalo katiza eneo hili ili litusaidie kutufikisha Nyakato na sasa hivi ni saa saba na dakika thelathini na saba tunatakiwa tuondoke hapa saa nane na nusu. Na dereva wa gari hilo anatakiwa auliwe.”

Mara baada ya tamko hili utekelezaji ulianza mara moja. Walikata matawi ya miti na magogo na kuyapanga barabarani pamoja na mawe mengi nayo yaliwekwa barabarani
na kuziba njia kabisa. Haikuchukua zaidi ya nusu saa gari aina ya TOYOTA HILUX lilitokea upande waliokuwepo. Bila kupoteza muda walisubiri lifike lile eneo walipotegesha mtego wao lisimame. Haikuchua muda dereva wa lile gari akasimama. Alipo simama tu Desmond alitokea ghafla na kumkaba shingoni na kumlaza chali juu ya barabara na kumwagia risasi nne za kifua na palepale akakata roho. Nahii ndiyo ilikuwa mara ya kwanza Laurance kuona mauwaji mbele ya uso wake.

“Twendeni huyu tayari hayupo nasi. Tayari tumembatiza jina la marehemu. Tumpakize humu humu kwenye gari tutajua tunaenda kumtupa wapi. Laurance shika uskani endesha gari kwa kasi ya ajabu mpaka Nyakato”

Mara moja Laurance alitii amri alijua kumbe rafiki zake walikuwa hawana mchezo na kazi yao aliamini endapo akileta jeuri anaweza kuondolewa uhai wake muda wowote
ule watakapo hitaji. Gari lilitembea kwa kasi. Haikuchukua muda ndani ya saa moja na nusu walikuwa wameshafika Nyakato. Umbali kati ya sehemu waliotoka hadi hapo ni kilomita 147.5 na hii inaonyesha ni jinsi gani walivyokuwa wanakwenda kwa kasi.

“Wewe baki hapa sisi tunaenda kuvamia hiyo nyumba ya muhindi jana tuliambiwa ameingiza ndani shilingi milioni thelathini. Tusubiri mpaka tutakapo rudi endapo ukionakuna mtu yeyote unaehisi pengine ni afisa usalama bastola unayo tutaharifu kwa kuipiga juu au kwa kumuua” (Kelvin aliongea)

Laurance aliitika na kutii amri. Alibaki kwenye gari huku akitazama ile maiti nyuma ya gari iliyokuwa ikivuja damu nyingi kifuani na masikioni.Akavua shati lake na kumfunika
sehemu inayotokwa na damu sana ili kuzuia damu isitapakae sana. Wakati akifanya hivyo wazo likamtuma kumpapasa mifukoni. Akatazama kulia na kushoto alipo ona kupo salama akaweka bastora kwenye kiti cha mbele cha gari na kuanza kumpapasa marehemu mifukoni. Hakuona kitu akamlaza na kuanza kufungua droo za gari kwenye dashboard ya gari.


Akaona vitu vidogo vidogo vitatu vya kila rangi mithili ya mawe vikiwa vimezungushwa na pamba nyingi na vitambaa vingi. Alipo kazia macho yake kwa umakini akagundua ni TANZANITE.

“Thanks GOD (asante mungu)” (alijisemea moyoni)

Akaangalia kulia na kushoto hakuona mtu. Akavua viatu vyake na kudumbukiza yale madini ndani ya viatu vyake. Alipo maliza tu kufanya hivyo alishtushwa na mlio wa simu
ukitoka kwenye gari. Haraka haraka akaanza kulikagua gari lote na baadae akaiona. Ulikuwa ni mlio wa sms. Akaichukua simu ile na kuusoma ujumbe ule

“hello mr upo wapi? sisi tupo hapa hotelini tunakusubiria wewe utuletee huo mzigo”

Bila kupoteza muda Laurance akachukua simu hiyo na kuizima na kutupa kwenye kiti cha nyuma moyo wake ukiwa unatabasamu na kujiona tayari amekwisha kuwa tajiri
kijijini.

Akiwa bado anafikiria na kupanga plan za maisha yake ghafla alisikia mlio mzito wa bunduki na kilio cha mwanamke kikitoka kwenye nyumba aliyo waliyoingia Desmond na Kelvin akili zake zikahisi kuwa tayari mauwaji yametokea na bila shaka yule mwanamke aliye toa hiyo sauti atakuwa ni mke wa muhusika aliyevamiwa. Akiwa analifikiria hilo mlio mwingine ulisikika na ile suti ya kilio ikakata ghafla.

Akijiweka tayari kwa mashambulizi, akawasha gari na kuliweka sawa kwa kuondoka. Baada ya sekunde kadhaa Kelvin na Desmond wakatoka mule ndani wakiwa wanakimbia mikononi wakiwa wamebeba mifuko iliyo jaa pesa walizoiba. Wakaingia ndani ya gari na kufunga milango pamoja na madirisha na kisha wakatoa amri.

“Ondoa gari haraka”

Laurance aliondoa gari kwa mwendo usio wa kawaida na kuanza kurudi kijijini.

Desmond na Kelvin mioyo yao ilifurahi sana kwa sababu tangu waanze matukio ya ujambazi hawajawai kuiba pesa nyingi zinazo karibia milioni thelathini lakini leo
wamezipata. Walimuahidi Laurance kugawana pesa hizo nusu kwa nusu kwa kila mmoja kwa kujipongeza kwa shughuli zito waliyo ifanya. Mawazo ya Laurance hayakufikiria tena pesa hizo yalikuwa yakifikiria madini aliyo yapata japo hakutaka kuwashirikisha wenzake.

Safari ikiwa inaendelea gari lilizima ghafla wakiwa barabarani na muda huo ilikuwa tayari ni saa kumi na moja asubuhi

“Vipi mbona gari limezima??”(Desmond aliuliza)

“Mhh sijui labda injini imepata hitilafu kwa sababu tangu mwanzo wa safari nililiona hili

swala nafikiri hii gari imetembea umbali mrefu bila kuzimwa”

“Sasa tufanyaje na huyu maiti nae tufanyaje”

“Hata sijui…!!”

“Hebu litoe barabarani liweke pembeni tuanze kutembea kwa miguu nafikiri ni kilomita chache zimebaki kufika kijijini. Na juu ya ukubwa wa tukio hili inabidi twende tukajifiche mbali na TANZANIA ili kuzima kesi kwa sababu mpaka sasa tumeondoa roho tatu”

Laurance alibaki kimya pasipo kuwajibu chochote nafsi yake ilimuuma alipo kumbuka tukio alilofanya. Alijiona kama ameshiriki dhambi kubwa sana na tena ni dhambi ya mauti. Akaliweka gari pembeni ya barabara wakashusha mizigo na yale mabegi yao ya mgongoni na kutoa zile nguo na kuzibadilisha na zile nguo za OVERLORY wakazitelekeza kwenye gari pamoja na silaha zao zote walizo zitumia.

“Na hii maiti tuifanyaje?” (Laurance aliuliza)

“Achana nayo chakufanya inabidi tusaidiane kulisukuma gari hadi kwenye mto uliopo hapo mbele kidogo halafu tulidumbukize mtoni nafikiri litakuwa wazo zuri tena katika kipindi hiki cha mvua mto umejaa gari litazama lote”

Wakaanza kulisukuma gari mpaka karibu na eneo la mto wakalielekeza upande wenye shimo lefu juu ya daraja wakalisukuma na Kulidondoshea humo lakini kwa bahati
mbaya halikuzama lote. Wakaachana nalo na kuanza kukimbia mchakamchaka kuelekea kijijini.

Ilipohitimu saa moja asubuhi wakawa wameshafika eneo la kijiji wakajificha kaatika kichaka kimoja kwa lengo la kugawana pesa. Zoezi hili lilikwenda vizuri kwa sababu pesa walizo iba ni million 30 hivyo kila mmoja alipata milioni 10. Kila mmoja wao alionyesha tabasamu moyoni mwake…Japo bado nafsi ya Laurance ilikuwa ikiumia sana moyoni japo hakutaka kuonyesha hisia zake mbele yao.

“Jamani kunakitu nimesahau kwenye gari halafu ni muhimu sana?”(Laurance aliongea huku akionyesha hali ya woga)

Wote Walishtuka na kumtazama. Laurance alionyesha hali fulani ya kuchanganyikiwa kichwani mwake.
“Vipi tena? ni nini hicho tueleze? Mbona watutia hofu” (Desmond aliuliza)

“Leseni yangu ya gari”

“Wewe ni mpumbavu sana kwa nini utembee na leseni ya gari. Itakuwa rahisi kwetu kukamatwa pindi polisi watakapo pekua lile gari”

“Hatuwezi kurudi kulikagua?” (Laurance aliuliza kwa upole)

“Hilo haliwezekani tushaharibu mambo kule tulipotoka. Na nilazima eneo lile watu wameshaanza kujaa kushangaa tukio hivyo tukijisogeza eneo lile tutajiingiza matatizoni. Na kama ikitokea polisi wakakubaini pindi watakapo iona leseni yako tafadhrii usitutaje.Sikutegemea kama wewe ni mzembe kiasi hicho mchizi wangu"

Laurance aliishiwa nguvu na hapa ndipo alipo ona hatia ipo mikononi mwake. Baada ya kugawana pesa kila mtu aliondoka na kurudi kwake. Laurance njia nzima alikuwa akiwaza na kutokwa na machozi na kulaani kuwa umaskini wake ndio chanzo cha matatizo yake.

Moja kwa moja alienda mpaka nyumbani kwake na kumkuta Janeth akiwa nje ya nyumba akitwanga kisamvu.Alimuangalia kwa huruma na kumsogelea Janeth alipo muona Laurance alimkimbilia na kumkumbatia nakumbusu lakini bado aligundua kuwa mpenzi wake hakuwa na furaha.

Janeth ilimbidi asimamishe shughuli zake na kutoa mkeka ndani ya nyumba na kuuweka nje ili waketi pamoja na kujua nini kinacho mfanya mpenzi wake asiwe na furaha?
Lilikuwa swala gumu kulielezea na kila alipo kuwa akikumbuka machozi yalimwagika kama mtu aliyefiwa.

Akiwa anaendelea kulia akaingiza mkono kwenye begi akatoa pesa zote zilizopo begi kiasi cha shilingi milioni 10 nakumkabidhi Janeth huku akiendelea kulia kwa uchungu.
Janeth alibaki na mshangao .

“Hizi ni shilingi ngapi?”

“Hizo ni millioni kumi”

“Hee ni kazi gani uliyofanya imekupatia pesa nyingi kiasi hiki? Hapana nina wasiwasi…”

Laurance alihisi kutoneshwa kidonda alipo ulizwa swali hilo. Machozi na majuto ndivyo vitu vilivyo mtawala. Jameth bado alikuwa na hamu ya kujua hizo pesa kazipataje. Alichukua muda wa masaa mawili na nusu kumbembeleza ili aweze kumwambia ukweli juu ya pesa hizo.Ndipo Laurance alipopata ujasiri wa kufunguka na kumueleza kila kitu kilivyo kuwa tangu siku ya kwanza alipo kutana na wakina Desmond na Kelvin.

“Laurance unataka unambie hizi pesa zimepatikana kwa njia ya umwagaji damu wa mtu asiye na hatia….Kwa nini lakini umeamua kushirikiana na marafiki wabaya na nilisha kukataza kuwa na hao marafiki zako…Kwa nini lakini Laurance ni bora tungekufa na umaskini wetu kuliko haya mambo uliyo yaleta, kufanya hivi sio kwamba unanipenda hapana Laurance umekosea sana” Janeth aliongea manenno hayo huku akilia kwa uchungu na hasira zaidi ya mumewe alivyo kuwa akilia. Laurance alimtazama Janeth na kumkumbatia huku wote wakilia kwa masikitiko ma huzuni kubwa mioyoni mwao.

“Janeth sikujua…sikufikiri kama itakuwa hivi….Na kama ningekataa ninge uliwa. Kinacho niumiza kichwa ni juu ya hiyo leseni.Ni lazima nitakamatwa tu kwa sababu leseni hiyo ina picha yangu.Sina jinsi Janeth maisha yangu siku yoyote yatakuwa jela.Ninacho kuomba tumia vizuri pesa hizi…tumia vizuri sana….Ikiwezekana shiriki hata yale mashindano uliyokuwa unayataka ila ninacho kuomba tumia pesa hizi kutafutia pesa nyingine usitumie pesa hizi kununulia vitu vya thamani kwa sababu pesa hizi zina harufu ya damu usiyo weza kuisikia ila ni mungu pekee. Na kama ukinunulia kitu cha kudumu kwa pesa hizi hakika litakuwa ni jambo baya.” Kilio kiliongezeka huku wakiwa wamekumbatiana kwa nguvu kila mmoja alionyesha hisia zake za maumivu juu ya swala hilo.

“Laurance unaonaje hizi pesa tukazitupa”

“Hapana usizitupe fanya kama nilivyo kueleza”

“Naomba basi hili swala tumshirikishe na mama yangu”

“Usijali mpenzi"

*****************

Baada ya wiki moja kila kitu kikawa wazi kwa mama yake Janeth juu ya pesa za mchumba wa mwanae…Kiukweli aliumia ukizingatia Laurance alikuwa ni yatima hivyo
alimchukulia kama ni mwanae (Mtoto wake). Lakini Laurance alikuwa anasiri nzito moyoni mwake na siri hiyo hakutaka Janeth ajue alimshirikisha Mama wa Janeth tu. Na siri hiyo ilikuwa ikihusu yale madini ya TANZANITE aliyoyapata siku ile ya usiku wa tukio walilofanya Nyakato. Kwa kuwa moyo wa Laurance uliamini hauna maisha malefu mtaani alimuomba mama wa Janeth ahifadhi madini hayo kwa kuyaficha mpaka pale tu atakapo kuwa salama kutoka kifungoni. Na kwa kuonyesha upendo mama Janeth alikubali na ali muahidi kuitunza siri hiyo…

Ilikuwa ni jumapili Janeth, Laurance, na mama Janeth walikuwa nyumbani wakila chakula cha mchana mara mlango ukafunguliwa na watu wasio julikana wakaingia mpaka ndani sebuleni walipokuwa wameketi.

“Sisi ni maafisa usalama na tumeambiwa nyumba hii ndiyo anayoishi Laurance na tunatumaini ndiye mwenye hii leseni na kuanzia sasa yupo chini ya ulinzi na bila shaka atakuwa ndiye huyu hapa”

Vilio vilianza upya Laurance akatiwa nguvuni. Hakutaka kugombana na polisi wala kuwabishia akanyosha mikono yake na kukubali kutiwa pingu mikononi.

“Janeth, mama, mimi naondoka niombeeni huko niendako na mbaki salama…….Janeth nakupenda sana tafadhali tunza penzi langu.. Naamini mkono wa bwana utanilinda na hatakubali kondoo wake niangamie.” (haya ndiyo yalikuwa maneno yake ya mwisho)

“Hatuna muda wa kupoteza hapa muuwaji mkubwa wewe pumbavuuuuuuu……….unajikuta una maneno ya busara kumbe ni ibirisi hebu twende ukaozee jela” Hii ilikuwa ni sauti ya polisi iliyotamkwa huku akipigwa mabuti na kuingizwa kwenye gari la polisi…huku wakinyanyua juu juu kama furushi la mahindi Janeth na mama yake walilia kwa uchungu.Hawakuamini kama Laurance ataweza kutoka tena jela waliamini ndio utakuwa mwisho wake.Wakati huo Desmond na Kelvin nao walitiwa nguvuni zile silaha walizo telekeza kwenye gari zilikuwa na alama za vidole vyao na ilibainika alama ya vidole vilivyokuwa kwenye bunduki ya AK47 ndiyo ilihusika na mauaji yote ya kutisha na ilibainika ni DEsmond ndiye aliyekuwa muhusika wa tukio hilo.


ITAENDELEA. USIKOSE SEHEMU YA PILI YA SIMULIZI HII
JE UNGEPENDA NIENDELEE NA SEHEMU INAYO FUHATA, NIPE MAONI YAKO TAFADHALI.
 
Kwa jina gani niisake
Kaka register hapa bure Log In uweze kusoma sehemu zote tatu, Mimi ndiye muandishi wa riwaya hii, Nairusha kila siku saa 2 usiku kupitia page hiyo ya website , Napatikana kwa namba 0763133454 (Sms pekee) Ahsante kwa support mungu akubariki.
 
Tuendelee
Ahsante sana ndugu, Sehemu ya pili ipo hewani tayari, register hapa bure Log In uweze kusoma sehemu zote tatu, Mimi ndiye muandishi wa riwaya hii, Nairusha kila siku saa 2 usiku kupitia page hiyo ya website , Napatikana kwa namba 0763133454 (Sms pekee) Ahsante kwa support mungu akubariki.
Kwa jina gani niisake
Kwa jina gani niisake
Kaka register hapa bure Log In uweze kusoma sehemu zote tatu, Mimi ndiye muandishi wa riwaya hii, Nairusha kila siku saa 2 usiku kupitia page hiyo ya website , Napatikana kwa namba 0763133454 (Sms pekee) Ahsante kwa support mungu akubariki.
 
Ndugu sehemu ya pili na ya tatu ipo hewani, KUSOMA MUENDELEZO WA HADITHI HII TAFATHARI ISOME KUPITIA LINK HII Log In (BURE) kisha ukishajiunga nitumie sms 0763133454 ili mimi nikufungulie link.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom