Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,436
- 5,234
Kesi ya jinai namba 24514 ya mwaka 2025 iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania kwenye nchi za Malawi na Cuba Humphrey Polepole dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) na wenzake wanane imeendelea tena leo, Alhamisi Oktoba 16.2025, Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam chini ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Salma Maghimbi
Mapema leo, Mahakama ilianza kutoa 'uamuzi mdogo' wa pingamizi lililokuwa limewekwa jana, Oktoba 15.2025 na upande wa Jamhuri uliokuwa umeiomba Mahakama kuwaita Mahakamani na kuwauliza maswali ya dodoso (cross examination) Peter Kibatala na Godfrey Polepole kufuatia viapo vyao walivyowasllisha Mahakamani hapo, ikielezwa kwamba kwa kufanya hivyo itasaidia Mahakama kufikia uamuzi wa kesi iliyoko mezani, hata hivyo katika 'uamuzi huo mdogo' Mahakama imetupilia mbali pingamizi hilo, na kesi ya msingi kuanza kusikilizwa
Soma Pia: Ombi la kuletwa kwa Humphrey Polepole, mahakama yamjibu Kibatala HAIWEZEKANI
Wakili Peter Kibatala, anayemwakilisha Humphrey Polepole ambaye ametoweka kwenye mazingira tatanishi alianza kwa kuipitisha Mahakama kuhusiana na kile kilichopo kwenye kiapo cha ziada cha Godfrey Polepole kilichowasilishwa Mahakamani hapo
Kupitia kiapo hicho cha Godfrey Polepole, Wakili Kibatala amedai kuwa kutokana na taarifa kadhaa alizonazo Godfrey anaamini ndugu yaka anashikiliwa na Jeshi la Polisi, hivyo kuendelea kuomba afikishwe Mahakamani au aachiwe kwa dhamana