Maamuzi ya kiongozi yakitegemea vigelegele

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918
Historia inatuonyesha wazi kwamba viongozi wote walifanya maamuzi kwa kushinikizwa na kelele na vigelele vya mashabiki walifanya maamuzi mabaya sana, walijikuta wakivunja sheria na kujikuta wamewahukumu watu wasio na hatia.

Nitatoa mifano michache kutoka kwenye Biblia.

Yesu alisulubiwa kwa sababu ya kelele za watu wala hakuwa na hatia ila Pilato kiongozi wa wakati huu alitaka kuwafurahisha watu, akawauliza NIMTUMBUE YESU AU NISIMTUMBUE wakasema mtumbueeeeee.

Sulemani hakufuata kelele za watu au mashitaka ya mtu anayejua hujieleza alipowaambia askari wake wamtumbue mtoto wampe kila kila mmoja kipande chake...mmoja alisema tumbuaaaa, ila wapi akasema kuliko kumtumbua mpe yeye huyo mtoto...matokeo yake mfalme Sulemani alipata hekima ya kufahamu nani mwenyehaki ya kupewa mtoto.

Kwa stahili hii ya mashabiki nchi itatumbukia pabaya. Rais anahitaji hekima kuliko kelele za watu na vigelele vya watu kufanya maamuzi kama kiongozi mkuu wa nchi
 
Hauko mbali sana na mimi, ILA katika waliotumbuliwa najiuliza kuna aliyeonewa? Bado natafuta jibu
 
We kweli ni mufilisi. Unamjua Yesu wewe? Yaani umuweke kwa kumlinganisha na Kabwe, huyu ambae cdm walimpigia kelele sana. Ebu pumzisha akili kwanza, isije ku-knock tusije pata taabu ya ku-overhaul kichwa chote. Umeharibu siku yangu.
 
Historia inatuonyesha wazi kwamba viongozi wote walifanya maamuzi kwa kushinikizwa na kelele na vigelele vya mashabiki walifanya maamuzi mabaya sana, walijikuta wakivunja sheria na kujikuta wamewahukumu watu wasio na hatia.

Nitatoa mifano michache kutoka kwenye Biblia.

Yesu alisulubiwa kwa sababu ya kelele za watu wala hakuwa na hatia ila Pilato kiongozi wa wakati huu alitaka kuwafurahisha watu, akawauliza NIMTUMBUE YESU AU NISIMTUMBUE wakasema mtumbueeeeee.

Sulemani hakufuata kelele za watu au mashitaka ya mtu anayejua hujieleza alipowaambia askari wake wamtumbue mtoto wampe kila kila mmoja kipande chake...mmoja alisema tumbuaaaa, ila wapi akasema kuliko kumtumbua mpe yeye huyo mtoto...matokeo yake mfalme Sulemani alipata hekima ya kufahamu nani mwenyehaki ya kupewa mtoto.

Kwa stahili hii ya mashabiki nchi itatumbukia pabaya. Rais anahitaji hekima kuliko kelele za watu na vigelele vya watu kufanya maamuzi kama kiongozi mkuu wa nchi

Una kifua lakini????subiria matusi
 
RAIS MAGUFULI Ni Mpango wa Mungu...Wenye Akili watanielewa namaanisha nini
 
We kweli ni mufilisi. Unamjua Yesu wewe? Yaani umuweke kwa kumlinganisha na Kabwe, huyu ambae cdm walimpigia kelele sana. Ebu pumzisha akili kwanza, isije ku-knock tusije pata taabu ya ku-overhaul kichwa chote. Umeharibu siku yangu.

sio kabwe...ishu tunaongelea context nzima ya kuwajibisha watu bila kufuata taratibu na sharia.....Watu wawajibishwe...lakini sharia ifuatwe.....Mihemko haina nafasi
 
Nilikuwa nawaza if John anapenda kick basi siku ya mei mosi angepandisha mishahara ili kuwafurahisha watumishi.... I believe in him
 
We kweli ni mufilisi. Unamjua Yesu wewe? Yaani umuweke kwa kumlinganisha na Kabwe, huyu ambae cdm walimpigia kelele sana. Ebu pumzisha akili kwanza, isije ku-knock tusije pata taabu ya ku-overhaul kichwa chote. Umeharibu siku yangu.
Umeisoma habari hiyo vizuri? kuna mahali nimemtaja kabwe au nimeongelea in general...nimeeleza jinsi kiongozi anavyotakiwa kuepuka kufanya maamuzi kwa kushinikizwa na kelele na misisimko( emotions ) hivi mtu mwenye akili na mwenye kutamani kiongozi kufanya vizuri anawezaje kupinga ushauri huo? tatizo mnataka kuweka watu wote ktk kapu moja.
 
RAIS MAGUFULI Ni Mpango wa Mungu...Wenye Akili watanielewa namaanisha nini
Hata Sauli kwenye Biblia alikuwa ni mpango wa Mungu..hata Kikwete mlisema ni mpango wa Mungu. kila kiongozi anayetawala nchi ni mpoango wa Mungu awe mzuri au mmbaya sasa inategemea mpango wa Mungu upi ( maana kuna permissive will of God and perfect will of God which one unayomaanisha?
 
Kiongozi wenu ndo anapenda hivyo..ikiwezekana hata mumpigie ngoma acheze ili mumshangilie vizuri..
 
Back
Top Bottom