Maamuzi sahihi kwa wakati sahihi

Pamputi

JF-Expert Member
Apr 22, 2016
982
724
HAKUNA NAMNA YA KUMVUMILIA MSALITI MWENYE SIFA HIZI NDANI YA CHAMA (CCM)

1. Mnategemea mbinu zake kuleta ushindi wakati kichwani mwake anapambana kuwamaliza kwa faida ya wapinzani aliowakabithi moyo wake.

2. Msaliti ni wakala wa taarifa nyeti kutoka kwenye vikao vya chama kwenda kwa wapinzani (mvujisha siri)

3. Msaliti ndani ya chama ni kikwazo cha kufikia matarajio ya chama kwenye chaguzi, kutekeleza ilani na shughuli za chama kwa ujumla

4. Msaliti ni mtu anayefurahishwa na kushindwa au kusulubiwa kwa chama (CCM) na wapinzani, mkiwa nae anajifanya kuumia pembeni anafanya sherehe.

5. Msaliti ni sawa na kifaa kibovu kwenye gari wakati dereva anapambana kusonga mbele kifaa kibovu kinakwamisha safari.

6. Msaliti ni adui mwenye siraha ndani ya chama, maana anajua nguvu na udhaifu wa chama ni rahisi sana kuleta matatizo kwenye chama .

7. Msaliti ni kama mpishi anayepika chakula akiwa na sumu mkononi, muda wowote anaweza kuleta anguko la chama.

8. Msaliti hana tofauti na kichaa aliyekabithiwa siraha muda wowote anaweza kubomoa ngome ya chama ( CCM)

9. Msaliti ni ugonjwa ndani ya chama, wakati viongozi na wanaCCM wengine awaleta afya njema ya chama msaliti anakidhoofisha.

10. Msaliti ndani ya CCM ni halufu mbaya mbele ya wanaCCM waadilifu akikaa karibu nao wanaanza kutoa halufu mbaya.

CCM imefanya maamuzi sahihi, wakati sahihi kwa maslahi ya CCM na taifa kwa ujumla maana bila CCM imara taifa litatikisika , nawapongeza viongozi na wajumbe wote waliokubaliana kuwachapa wasaliti bila huruma.

Ni vema sasa rungu hili likawachape wanaotumia rushwa kwenye uchaguzi wa chama na serikali, hii ndiyo njia muhimu ya kuirudisha CCM mikononi mwa wananch wa kawaida.
 
Magamba mna vituko, yaani mbwembwe zote hizo Ila mtaishia Kuiba kura, poleni sana.
 
In the game of thrones its either you win or you die,there is no middle ground.

When you know which friend is not yourfriend,utajua nini cha kufanya kwa usalama wako.
 
CCM vipi mbona mmepanic wenyewe kiasi kwamba kila baada ya dakika 5 inabidi mfungue thread mpya ya kutetea maamuzi ya chama Chenu?

Mnahofia nini hasa?
 
Saaafi sana. Sema wazee wa ufipa hii inawauma kupita kiasi, wanaumia kisa mirija yao inakatwa katwa kama nyanya ya kachumbari vile
 
Very very nice na kesho mfukuze na wengine ili muendeleze unpopularity yenu mloipata tangu muokote embe chini ya mnazi. Pia endeleeni kumtumia professor yule ambaye PhD yake I'm expire kwa kukuhurumia cuf in anticipation you gonna win. Endeleeni pia kuwakamata watu wa opposition huku mkijiona you are godesses
 
Back
Top Bottom