Kuna wakati mwengine unatakiwa upige hesabu kambla ya matumizi,unajua kama hii kazi ndio inayonipa jeuri yakuweza kulipa kodi,chakula,na mahitaji yako yote iweje useme basi staki tena kazi? wanasema usi achie tawi kabla hujashika tawi, hakuna raha mda wote kazini,mimi DG wangu ni mwanamme ila kuna siku anakuja na mood mbaya mpaka unajiuliza hivi huyu bwana ni binadamu au mnyama? sababu nimesha msoma hua najaribu sanaa kua nae mbali akifanya party kwake siendi,sijui mikutano ile ya kulala mahotel siendi mpaka kuna siku akaniita akanambia ivi unajisikiaje mpaka nikikualika huwezi kuja? nikamwambia ingekua ipo kwenye mkataba wangu ningefata boss au ningekua free ningefata lakini ni haipo utanisamahe nna majukumu nyumbani,tangu siku hiyo hawaniuliza kwanini huji, anyway jitahidi upate kwengine lakini sikunyengine hakikisha umepata kazi kwengine ndio unawacha ulipo ajiriwa..