Maamuzi haya ya serikali yana mapungufu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maamuzi haya ya serikali yana mapungufu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Sep 16, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Serikali imetangaza kwamba kuanzia sasa watoto wa shule wasiingie kwenye vijiwe vya kuonyeshea TV.Naipongeza serikali kwa kuelewa kwamba vijiwe hivyo vinachangia katika uharibifu wa maadili, lakini mbona kwa kuchelewa sana?Hata hivyo hatua hiyo ni ndogo sana.Ninaloshauri mimi ni kwamba serikali iende mbali zaidi.Ihakikishe kwamba vituo vya Television na Radio havitoi matangazo yeyote yanayopotosha maadili,na pia makampuni ya biashara nayo hayasambazi matangazo yanayochangia katika uhamasishaji wa ngono na upotoshaji wa maadili.Tukumbuke kwamba upotoshaji huo hautokei kwenye vijiwe vya kuonyeshea kanda za video na matangazo ya television tu, bali unatokea hata majumbani.
   
 2. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2008
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Tikerra, hilo silo jambo la ajabu kwa serikali yetu. Kuna msemo: Nyoka huuma afikiapo. Yaani, hiyo ni namna serikali yetu inavyotenda. Siyo rahisi, kuziba ufa bali kujenga ukuta! Na ukiangalia mambo mengi yanaenda hivyo.

  Kulikuwa na fununu wiki hii kuwa kuna kiwanda fulani hapa jijini kinatoa moshi unaoathiri wakazi wa eneo fulani. Lakini nilisikia kuwa "Hakuna taa**** kama hiyo" badala ya kusema watafuatilia. Halafu kuna kiwanda kingine pale Mbagala Mission kinaharibu mazingira na pia moshi wake unaathiri wakazi wa eneo hilo, maana kiko katikati ya makazi ya watu. Lakini hutasikia neno lolote kutoka serikalini.

  Labda kutakapoanza kutokea magonjwa ya ajabu ndiyo serikali itajifanya inawajali watu. Kwa hiyo, hata hilo la TV au filamu fulani zisizofaa kwa watoto lilishasemwa muda mrefu tu, lakini huko mitaani bado zinaonyeshwa na watendaji wa serikali wapo. Kelele kutoka baa zilizo katikati ya makazi ya watu bado zinaendelea lakini hakuna kinachofanyika.

  Ndiyo, maana mimi naona watoto wakishaharibika na baadaye serikali kujifanya inajali sana, naona imejitahidi sana kwani haiwezi kuzuia kabla mpaka uharibifu utokee. Hiyo ndiyo NGUVU MPYA, KASI MPYA NA ARI MPYA!
   
Loading...