Maalum kwa wanawake: Je, ni fahari kutumia jina la mumeo?

TANZANNIA

JF-Expert Member
Sep 29, 2015
1,047
384
Hii imekaaje!?

Mwanamke kabla hajaolewa anatambulika kwa jina la 'Miss X' ambalo ni jina la ukoo wa baba yake. Akishaolewa title inabadilika na kuwa 'Mrs Y' ambalo ni jina la utambulisho la ukoo wa mumewe.

Je, kwao ni fahari kuacha jina la ukoo wenu na kuhamia ukoo mwingine?

Kwa ujumla wetu tujadili.
 
Kwa upande wangu sioni sababu ya msingi ya kubadili jina la family yangu nihamie kwa Mume kwani mzazi wangu atabakia kua yeye regardless.
Mume ni Baba wa watoto wangu au mzazi mwenzangu namuheshimu nampenda lakini hapana watoto wake wamechukua jina la ukoo wake imetosha,isitoshe ndoa zenyewe hizi za ki china mbona utamaza majina na ukoo wa mume...
 
Miulize Juice dyudyu atakuwa na jibu zuri by the way sijaona kwa waislam haya mambo ya kubadili majina kama alikuwa frame Kadili atabakia vivyo hivyo.
 
Ni kitu tulichokikuta la sivyo hakuna sababu na sasa hivi hiyo fasheni inaishia! Mama Fulani (jina la mtoto) au Jina lako ikifuatiwa na jina la mumeo inatosha kabisa mfano Gudila Mambi mke wa Joshi Penda.
 
Si ufahari, ukihis ni ufahari bas ni ulimbukeni. Jna langu halijawahi kubadilika na sitarajii hvyo. Japo yapo baadhi ya maeneo itabdi ulitumie ijulikane nyie n couple
 
Imeandikwa mwanamke ataacha wazazi wake naye ataambatana na mumewe nao watakua mwili mmoja
Sasa hamuwezi kuwa mwili mmoja majina tofauti.
Basi achukue jina la mke...ukiona mume anang'ang'ania mke abadili jina jua ni insecurity....mume wangu hajawai complain wala kugusia swala la majina...jina halina maana yoyote...hata cheti cha ndoa akijaunganisha majina...kila mtu amesign kwa majina yake kamili...sijui huu muungano unatoka wapi???!!!
Ndio maana mnachukia watoto wa kike...mimi baba yangu anaendelea kula matunda ya kunisomesha ...maana sijatupa jina lake kwenye dustbin
 
Na utamu unaanza pale mnapo divorce...mnaanza kugomania mali na jina...kazi kweli kweli

mambo ya leticia nyerere.. baada ya divorce mumewe anakomaa aache tumia jina la nyerere.. mama kakomaa nalo mpaka mwisho.. as yeye na watoto wake ni nyererez.

jina linampa heshima dunuani.. akipita ma airport ya ukweli wakaguzi wakisoma passport wanamgwaya na kumpa heshima yake.. ataliacha vp
 
Wanawake ndiyo upenda kutumia majina ya mumewe na hii ni ktk aina mbili tu, mwanaume awe na hela au cheo fulan bila hivyo sahau mwanamke kutumia ukoo wako?
 
Akiwa mbunge, waziri n.k ntatumia lake ila sahivi jina lake ntatumia kwenye vikoba tu

Na huo ndiyo ukweli kama huna hela jaribu kumwambia mwanamke atumie jina lako kitakachofata utakuja kutuambi, tena raha mwanamke awe muajiriwa alafu ww mfuga kuku flan cku hiz mjasiliamali? Sasa mwambie aende kazin kwake eti abadili ukoo wake kama ajachukua mtaji wake wa kuku aliwokukopea na doa la ndoa likaanzia hapo.
 
Vyeti vyangu vinaonesha luckyline flani so jina la mme ni kwa watoto tuuu.
 
Back
Top Bottom