Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,011
- 9,879
Mgombea urais Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharrif Hamad amesema katika uongozi wa serikali watajali makundi maalum ambayo ni wanawake, watoto, wazee, walemavu na walioathirika na UKIMWI na dawa za kulevya.
Kwa wanawake amesema watahakikisha wanawake hawabaguliwi kwenye masuala ya kazi, hivyo watahakikisha uwiano makazini na kupinga udhalilishaji wa aina zote. Kwa watoto amesema watahakikisha wanapata lishe.
Pia amesema wazee wana mchango mkubwa katika nchi hiyo. Hivyo atafanya kila mzee anapata Tsh laki moja kwa mwezi na kupewa bima za afya. Pia wazee wenye miaka zaidi ya 65 wazee watalipiwa nauli ya daladala na serikali.
Aidha kwa walemavu amesema kila jengo la Zanzibar litakuwa na mazingira rafiki kwa walemavu kuweza kuitumia. Pia kwenye ajira walemavu hawatabaguliwa. Pia watazuia dawa za kulevya zisiingie Zanzibar ili kuwaepusha vijana na uraibu.