Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,306
- 25,929
Wakati jitihada za kutafuta suluhisho la mgogoro wa kisiasa Zanzibar zikiendelea,vikao vinavyoendelea baina ya CCM na CUF havina uwiano wa uwakilishi;makada sita wa CCM dhidi ya Maalim Seif Sharrif Hamad wa CUF. Pande hizo zimeunda Kamati Maalum inayoongozwa na Rais wa Zanzibar, Dr. Ali Mohamed Shein lakini inakosa uwiano wa uwakilishi.
Mbali na Dr. Shein, wengine walio kwenye kamati hiyo ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Rais wa Awamu ya Pili ya Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Serikali ya awamu ya nne, Jakaya Kikwete na Marais wastaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na Dr. Salmin Amour. CUF inawakilishwa na Katibu Mkuu wake Maalim Seif ambaye ndiye aliyegombea Urais wa Zanzibar.
Kamati husika imeshaanza vikao vyake.
Chanzo: Mwananchi la 29/12/2015, uk. 4