Maalim Seif: Ukimya wangu una mshindo kwa Zanzibar

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,839
20,285
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kukaa kwake kimya kuna kishindo kikubwa kinakuja visiwani Zanzibar.

Maalim Seif ambaye aliwahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa visiwani humo, alisema kamwe hatorudi nyuma, kwani hajashindwa na wala haitotokea kushindwa katika maisha yake.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini Unguja, alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani, ambapo pamoja na mambo mengine alisema umaskini sasa umekuwa ukiwatesa wananchi katika kila eneo.

Katika uchaguzi huo CUF inawakilishwa na mgombea wake Abdulrazak Khatib Ramadhan ambaye anapambana vikali na mgombea wa CCM, Juma Ali Juma.

Maalim Seif ni kama alikuwa akijibu mapigo ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdurhamn Kinana ambaye mwishoni mwa wiki alisema kuwa kiongozi huyo anazungumza hali ya kuwa hajui lolote kinachoendelea katika nchi wala katika chama chake.

“Sasa nawaambieni musinione kimya, kimya kikuu kina mshindo mkubwa wala usidhani kuwa tumeshaachia hapana bado kabisa tunaendelea kupigania haki yenu na haki Inshallah haipo mbali na mimi niwaambieni vijana sijashindwa na sitoshindwa.

“…na kama itatokea bahati mbaya nishindwe nitawataarifuni mchukue uamuzi wenu lakini sitegemei kufika huko kwani mambo haya yana miiko yake,’’ alisema Maalim Seif.

Akizungumzia hali ya umaskini nchini alisema tangu uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano, ulipoingia madarakani kwa kile alichodai kwa kutumia mabavu hali ya umaskini imeendelea kuwatesa wananchi.

Alisema hali hiyo inachangiwa na uongozi kufanya mambo yasiyokuwa na tija ambapo kwa kushirikiana na kiongozi mstaafu wa Serikali iliyopita walifanya mapinduzi na kubatilisha matokeo ya uchaguzi yaliyofanywa na Wazanzibari waliyoyafanya Oktoba 25, mwaka 2015.

“Lakini kilichotokea mwaka juzi sasa Serikali imekuwa ya dhulma wale wenye ajira wanapokonywaa ajira zao ikiwemo kuwaondosha wafanyabiashara darajani, Kijangwani na sasa wanakwenda Michenzani jambo ambalo ni hatari kwa Taifa hili,’’ alisema Maalim Seif.

Katibu Mkuu huyo wa CUF ambaye alikuwa mgombea urais katika uchaguzi uliopita, alisema pamoja na hali hiyo lakini bado suala la mafuta na gesi limekuwa na upungufu hasa kupitia sheria yake ambapo sasa kunaifanya Zanzibar kuwa kama manispaa.

Lowassa akumbusha ya 2015

Naye aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), aliyeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Edward Lowassa, alimpongeza Maalim Seif kwa kumwalika na jinsi alivyokuwa mvumilivu katika mambo yote wanayomfanyia.

Alisema Maalim Seif alimshinda aliyekuwa mgombea urais wa CCM, Rais Dk. Ali Mohamed Shein kwa wastani wa kura 16,000.

Kutokana na hilo aliwashukuru vijana waliosikia wito wake wa kutofanya vurugu baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo kwani kama wangefanya hivyo kulikuwa na hatari ya kupoteza maisha.

Akizungumzia suala la njaa alisema ni ajabu kwa Rais aliyepo madarakani kubeza suala hilo.

Lowassa alisema kuwa wakati wa utawala wa Rais wa Awamu ya Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere, hasa pale nchi ilipokubwa na baa la njaa, alisema yupo tayari kuzungumza na makaburu ili kuweza kukabiliana na baa hilo lililoikumba nchi kwa wakati huo.

Alisema ni lazima kuhakikisha katika uchaguzi mbalimbali kunakuwa na ushindi na kila mmoja akatae azuie wizi wa kura kama uliotokea 2015.

“Lazima kukataa kuibiwa kura ni lazima kukataa kutiwa hofu na kutishwa hii ni nchi yetu sote tufuate sheria na uchaguzi ujao ni lazima kushinda na viongozi wanaopambana ni lazima kuungwa mkono kama ilivyokuwa kwa Maalim Seif ni mfano wa kuigwa,’’ alisema Lowassa.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Mazrui alisema wanaingia katika uchaguzi huo bila kuwa na ruzuku lakini hadi sasa tayari Sh milioni 20.4 zimepatikana kutoka kwa wanachama wenyewe.

Aliyashukuru majimbo yaliyochanga ikiwa ni pamoja na Nungwi, Makunduchi, Mtoni, Magomeni, Kikwajuni, Konde, Chambani, Chakechake, Chonga, Bububu na Ole.

Naye Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi Zanzibar, alisema wataendesha kampeni kistaarabu tofauti na wa upande wa pili ambao ni CCM wanaorusha maneno badala kueleza sera.

Alitoa ratiba za kampeni hiyo ambapo Januari 11 atakuwepo Mbunge wa Singida Tundu Lisu na Januari 15 Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro atakuwa
mgeni rasmi.
source; Mtanzania
 
Mmemsikia Jecha lakini nyinyi chichiem? Kasema Zanzibar Hali ya kisiasa ni mbaya sana... Watu hawazikani tena unajua hatua hiyo ni mbaya?? Halafu ninyi mnachekelea
 
Kashindwa kumpokonya Uenykt Lipumba ataweza kumpokonya Urais Dr.Shein?

Huyu Mzee Ana mikwara sana ukiwa fala fala unaweza ukaogopa.

1995 kwa Wakubwa wenzangu wanakumbuka alikuwa Ana Msemo wake ' Salmin hafiki 2000' akimaanisha atampindua kabla hajamaliza Muda wale lakini zilikuwa story tu na walioziamini Akina Hamad Rashid na Juma Duni na kina Machano Hamisi wakaishia kukaa Gerezani Miezi 18 wakati Mwenzao Sief akajigeuza Vasco Dagama kuzunguka Ulaya eti anaenda kudai Ushindi wake.

Ushindi uporwe Kisiwandui ukaudai Pennyslivania au Newyork ?. Seif bana!
 
Kashindwa kumpokonya Uenykt Lipumba ataweza kumpokonya Urais Dr.Shein?

Huyu Mzee Ana mikwara sana ukiwa fala fala unaweza ukaogopa.
1995 kwa Wakubwa wenzangu wanakumbuka alikuwa Ana Maemo wake ' Salmin hafiki 2000' akimaanisha atampindua kabla hajamaliza Muda wale lakini zilikuwa story tu na walioziamini Akina Hamad Rashid na Juma Duni na kina Machano Hamisi wakaishia kukaa Gerezani Miezi 18 wakati Mwenzao Sief akajigeuza Vasco Dagama kuzunguka Ulaya eti anaenda kudai Ushindi wake.
Ushindi uporwe Kisiwandui ukaudai Pennyslivania au Newyork ?. Seif bana!
Duh!

Watanzania mna maneno!

Hata kama hutaki kucheka inabidi ucheke.

Eti Ushindi uporwe Kisiwandui ukaudai Pennyslivania au Newyork.

Ama kweli, Jamiiforums is Where We Dare to Laugh!

Kinachoshangaza kuna baadhi ya watu wanaamini porojo zake!
 
Duh!

Watanzania mna maneno!

Hata kama hutaki kucheka inabidi ucheke.

Eti Ushindi uporwe Kisiwandui ukaudai Pennyslivania au Newyork.

Ama kweli, Jamiiforums is Where We Dare to Laugh!

Kinachoshangaza kuna baadhi ya watu wanaamini porojo zake!

Inafanana na zile porojo za sijui za ICJ baada ya 'kuibiwa' kura zao ' team Mafuriko' ya 2015!
 
Inafanana na zile porojo za sijui za ICJ baada ya 'kuibiwa' kura zao ' team Mafuriko' ya 2015!
Nilishangaa kuna watu walijazwa upepo na kuamini eti ameenda ICJ.

Wanasiasa wa aina ya Maalim Seif wanatumia ujinga wa wananchi/wafuasi wao ili kuendeleza siasa za uwongo na unafiki.
 
Kiboko yake prof lipumba tu.
Lipumba si kiboko yake bali wabaya wake ni msajili na wafadhili wa Lipumba yaani CCM,tambua kuwa lipumba bila pesa za CCM hana lolote kwa sasa anatamba kuwasumbua CUF kutokana na uchunaji buzi pesa za CCM.
 
Mkuu Pascal Mayalla nakumbuka mwaka 1995 ukiwa DTV na kipindi chako cha Mada motomoto kama sikosei, mlimtangaza Maalim Seif kama mshindi kabla Tume ya Uchaguzi haijatoa matokeo yake. Ulishiriki kuvunja sheria ya uchaguzi. Mwaka jana Maalim kayafanya yale mliyoyafanya 1995. Mwasisi wa hali hii ni wewe ma DTV yako enzi hizo.
 
Mkuu Pascal Mayalla nakumbuka mwaka 1995 ukiwa DTV na kipindi chako cha Mada motomoto kama sikosei, mlimtangaza Maalim Seif kama mshindi kabla Tume ya Uchaguzi haijatoa matokeo yake. Ulishiriki kuvunja sheria ya uchaguzi. Mwaka jana Maalim kayafanya yale mliyoyafanya 1995. Mwasisi wa hali hii ni wewe ma DTV yako enzi hizo.
Mkuu Kimbunga, kwanza nikupongeze kwa kuwa ni mtu wa kumbukumbu sana kwa sababu kweli ni mimi na kipindi hicho cha Mada Moto ndicho kilichokuwa TV Talk Show ya kwanza Tanzania kikafuatiwa na kipindi cha Kiti Moto.

Sii kweli kuwa tulitangaza matokeo bali tulitangaza mwelekeo ambapo ni kiukweli kabisa CUF ndio walishinda ila aliyetangazwa ni CCM.

Kuna tofauti ya kutangaza trends na final results. Kazi ya media ni kutangaza trends za matokeo ya jimbo kwa jimbo na hili linafanyika kote duniani tena uchaguzi wa Marekani, trends zinaonekana live kadri zinavyoingia ambapo Hillary Clinton alishinda kwenye popular votes lakini Donald Trump akashinda kwenye electro votes.

Na chaguzi zote zilizofuatia Zanzibar tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, CUF ndiyo inashinda popular votes kwa upande wa trends ila inayotangazwa ni CCM kwa sababu inashinda kwenye electro votes zilizomo ndani ya chombo pekee, chenye mamlaka halali ya kutangaza matokeo ni NEC kwa Tanzania Bara na ZEC kwa Zanzibar, hivyo kufuta trends zote zilizotangazwa kabla.

Hata Maalim Seif hakutangaza matokeo bali alitangaza tuu trend, kutangaza matokeo ni kosa la jinai hivyo Seif angetangaza matokeo, angeisha kamatwa na kushitakiwa ZamanI. Kitendo cha Seif kutangaza trends za matokeo na kutokushitakiwa ni uthibitisho tosha kuwa Seif hakutangaza matokeo.

https://www.google.com/url?sa=t&sou...i-hajashitakiwa-jecha-kapata-wapi-mamlaka-ile.

Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda
Paskali
 
Kashindwa kumpokonya Uenykt Lipumba ataweza kumpokonya Urais Dr.Shein?

Huyu Mzee Ana mikwara sana ukiwa fala fala unaweza ukaogopa.

1995 kwa Wakubwa wenzangu wanakumbuka alikuwa Ana Msemo wake ' Salmin hafiki 2000' akimaanisha atampindua kabla hajamaliza Muda wale lakini zilikuwa story tu na walioziamini Akina Hamad Rashid na Juma Duni na kina Machano Hamisi wakaishia kukaa Gerezani Miezi 18 wakati Mwenzao Sief akajigeuza Vasco Dagama kuzunguka Ulaya eti anaenda kudai Ushindi wake.

Ushindi uporwe Kisiwandui ukaudai Pennyslivania au Newyork ?. Seif bana!
Na slogan ya "mapanga shwa shwa"
 
Back
Top Bottom