Maalim Seif si amrudishie msajili figo yake yaishe

Maalim Seif si amrudishie msajili figo yake yaishe

Yule aliyechoma kadi za ACT wazalendo kule Kigoma tena ni kiongozi wa CCM kafanywa nini? Yule anaehamasisha Lisu na Zito wauawe, ni kiongozi wa CCM kanafanywaje?? Kwanini Msajili usifute CCM, maana kila ovu wanalifanya wazi hata hati chafu kila mwaka ni wao, wauaji na watekaji, rushwa mfano juzi tu.???
 
MAALIM SEIF SI AMRUDISHIE MSAJILI FIGO YAKE YAISHE?

KUNA mlevi alikuwa glasi nyingi kichwani. Nikashtukia kaja mezani kwangu. Akaniomba akae, nikamkatalia. Akaniambia: "Na wewe usiwe kama Msajili, unanichukia nina figo yako?" Nikamtolea macho kwa hasira!

Akasema: "Mimi shida yangu nikuulize swali moja tu... Hivi Maalim Seif alimchukulia nini Msajili?" Badala ya kujibu, nikamuuliza, kivipi?

Akaniambia: "Si unaona jinsi haziivi? Au Maalim alimchukulia Msajili figo yake? Si amrudishie amani iwepo? Vipi, walikutana anga zipi. Kama kuna chochote Maalim alimchukulia Msajili, bora amrudishie maana sasa ni too much!" Nikamuuliza sababu ya kusema hivyo.

Akanijibu: "Si unajua Maalim ndo alikuwa Don pale Cuf? Msajili akambeba Lipumba wakati alijiuzulu na kusepa. Mwisho Maalim akawa hana chake Cuf kwa nguvu ya Msajili. Maalim katimkia ACT-Wazalendo. Msajili kamfuata Maalim hukohuko na sasa anataka kuifuta ACT." Nikamjibu kuwa Msajili anafuata sheria.

Ooh, mlevi akawa mbogo: "Sheria inamshughulikia Maalim tu? Anasema ataifuta ACT kwa sababu ya hesabu za mwaka 2013, wakati mwaka huo ACT ilikuwa haijazaliwa. Mbona kabla Maalim hajahamia ACT, hiyo hoja ya mahesabu haikuwepo? Miaka yote hiyo, alipohamia Maalim tu ndo yameibuka haya." Hapa mlevi akanibana hasahasa!

Mlevi akacheka, halafu akasema: "Tangu vyama vingi vianze, hatujawahi kuona chama cha upinzani kinatetewa na Serikali kama Cuf ya Lipumba. ACT wanatishiwa kufutwa kwa hoja ya wanachama wao kuchoma bendera za Cuf ya Lipumba." Nikaona nimfukuze yule mlevi kwa ukali ili aondoke mbele yangu.

Akageuka aondoke, lakini akaniachia ujumbe: "Simpo tu mwanangu, kama Maalim alichukua figo ya Msajili amrudishie, vinginevyo atapata tabu sana. Au kama kuna anga walikutana, basi akamwangukie, maana Msajili anaonesha hataki mchezo. Anamwandama sana." Sikumjibu ili aondoke.

Kweli aliondoka lakini akarudi mbio: "Unaona sasa, Maalim anaiponza ACT. Unajua Yona alikuwa kimeo melini, alitupwa majini. Sisemi ACT wamtupe Maalim, ila nashauri kama kuna chochote alimchukulia Msajili, amrudishie. Hii vita inaonekana haiishi leo. Atamwandama kokote na hivi kuna sheria mpya!" Nikaona nizibe masikio. Mlevi alipoona simsikilizi akaondoka.

Ndimi Luqman MALOTO

Sent using Jamii Forums mobile app
Mlevi ameongea ukweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maalim Seif Sharif Hamad aliwaambia wazanzibar. Nikiwa serikalini nitawatetea, nikiwa kwenye chama nitawatetea, nikifukuzwa nitawatetea, nikifungwa jera nitawatetea. Sasa lini amewaangusha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwamba ACT ihukumiwe kwa kosa ambalo wakati linafanyika hakukuwa na sheria husika. Taasisi na watu binafsi walitoa onyo juu ya sheria hiyo mpya ya vyama vya siasa, hasa mamlaka aliyopewa msajiri. Ofisi ya msajiri inachangia pakubwa sana kuharibu nchi yetu, inapaswa ijitafakari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom