Wanamkakati wa Maalim Seif wakiongozwa na Mansour na Amani Karume wametajwa kusaliti mipango ya kugomea uchaguzi wa marudio baada ya kujitokeza na kushiriki zoezi la upigaji kura, ambapo Mhe Amani Karume kapiga kura katika kituo cha Skuli ya Kiembesamaki na Mansour Yusuph Himid amepiga kura akiwa jela ya Kiinua miguu iliyopo Unguja.
Wawili hawa wanatajwa kuwa ni wanamkakati ambao walipendekeza na kushauri mpango wa kutoshiriki zoezi la upigaji kura katika uchaguzi wa marudio uliofanyika leo tarehe 20th March 2016.
Jambo hilo pamoja na baadhi ya wagombea wa nafasi ya uwakilishi kupitia CUF takribani 13 kushiriki upigaji kura na wagombea wa nafasi za udiwani kupitia chama cha wananchi wameshiriki pamoja na kuwepo zuio kutoka kwa kiongozi huyo mkuu wa Chama hicho kwa Zanzibar.
Majina ya wagombea uwakilishi waliojitokeza kupiga kura na majimbo yao mpaka sasa ni hawa wafuatao;
1. Omar Ali Shehe (Chake chake)
2. Hijja Hassan Hijja (Kiwani)
3. Abdilahi Jihad Hassan (Mwanakwerekwe)
4. Said Ally Mbarouk ( Gando)
5. Suleiman Simai Pandu (Kijitoupele)