Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 36,981
- 45,903
Nilibahatika kusikiliza mahojiano ya Maalim na Clouds kwa kweli kama Mtanzania nimesikitika sana.
Nimejiuliza siasa za aina hii zinataka kutupeleka wapi, kwa maana kwa hulka za watanzania visasi si jadi yetu.
Nimeandika haya nikiangalia namna ambavyo maalim amekuwa akibehave pale anapopingana mtazamo na viongozi wenzake.
Kwanza nilimuona akikataa kumpa mkono Rias wa Zanzibar, bila sababu za msingi, na akakiri kabisa kuwa hatompa mkono.
Kesi ya pili, ni katika mahojiano hayo na clouds alisema kwamba, ni bora kuzungumza na CCM kwa kuwa ni adui anayemfahamu kuliko kuzungumza na Lipumba.
Akaenda mbali kwa kusema kuwa endapo lipumba angeingia mahali alipo angeondoka, hata wakati ule wa mahojiano clouds, kama angelikuwepo angeondoka.
Kwa kauli na mitazamo hii ya Maalim namwona kama mtu mwenye visasi na asiye kuwa na uvumilivu.
Naomwona akikosa busara za kisiasa zinazotakiwa kuoneshwa na kiongozi wa aina yake ukuzingatia uzoefu aliokuwa nao katika siasa za nchi hii.
Kauli yake imetikisa sana muonekano wake kwa wengi.
Nimeshituka kwa kauli yake pia, kwamba CCM NI ADUI??? Kauli hii pia kwa msomi na mzoefu kama yeye ni kosa kubwa sana.
Nimetambua sasa kuwa Maalim anafanya Siasa za uadui, siasa za kujenga utengano na kupalilia visasi ndani ya jamii yetu, hii ni hatari sana.
Namwomba Maalim afute kauli zake, ajirudi kwani anapoteza wafuasi wachache waliobaki kwa vitendo na kauli zake.
Maalim anasahau kanuni moja kubwa inayosema , " Don't hate your enemy, it will affect your judgement"
Maalim anatanguliza chuki kwa wapinzani wake mpaka anatoa kauli zinazoharibu namna jamii inavyomwona.