MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,980
Kundi la Maalim Seif linachekesha kama sio kusikitisha!
Like a lamb to the slaughter ni nahau inayomaanisha mtu anafanya jambo bila kujua madhara yake na anafanya kwa upole bila kutumia njia mbadala ya kuzuia madhara yake. Ni kama kondoo anavyopelekwa kwenye machinjio kuchinjwa!
Kinachonishangaza kwenye kundi la Maalim Seif ni aina ya mbinu ambayo wamechagua katika mapambano na kundi la Prof. Lipumba.
Niliwahi kutoa ushauri kwa Maalim Seif kupitia thread hii;
LINK>>Maalim Seif tulikuambia achana na Lowassa, hukusikia!
Maalim Seif kama bado anadhani Edward Lowassa atamsaidia kutatua matatizo ya CUF atakuwa anapoteza muda wake!
Edward Lowassa ni mzuri katika mikakati ya kisiasa nchini katika mazingira kama umeshika dola lakini sio katika mazingira kama hujashika dola. Lowassa hajui fitina za kisiasa ukiwa upande wa upinzani kwa sababu maisha yake yote ya kisiasa amekuwa ndani ya CCM. Utazidi kupotea kisiasa kidogo kidogo kama utaendelea kuweka matumaini kwa Lowassa.
Maalim Seif na kundi lake wanadhani kutoa lawama na tuhuma nzito kwa taasisi ambazo ndizo wanazitegemea kuwasadia ndio watafanikiwa, lazima watambue kwa kufanya hivyo wanajidanganya na kujikaanga wenyewe.
Wakati Maalim Seif na kundi lake wamejikita kwenye media wakipiga kelele kutaka huruma kwa wananchi huku wakizituhumu taasisi zilizopewa mamlaka kisheria kushughulikia tatizo lao, mwenzao Prof. Lipumba na kundi lake wameamua kufanya mambo yao kimya kimya.
Ieleweke kuwa Prof. Lipumba na kundi lake wamekwenda mara nyingi mahakamani na kugonga mwamba lakini hawajatoa lawama kwa mahakama kwa sababu wanatambua madhara ya kutoa lawama kwa taasisi wanayoitegemea katika kutatua matatizo yao.
Moja ya njia ya kutatua tatizo kwa usahihi ni kuelewa chanzo chake, kuyatambua madhaifu na kuyakubali ili upate nafasi ya kutafuta majawabu sahihi.
Dhambi ya kuandika katiba ya CUF na kumpa Mwenyekiti wa CUF Taifa na Katibu Mkuu madaraka makubwa ndani ya chama kwa sasa inamtafuna Maalim Seif na kundi lake. Waingereza husema, ‘’What goes around comes around’’.
Kama isingekuwa ubinafsi wa Maalim Seif, kwa sasa wangekuwa wameenda mahakamani kuzuia kazi zote za CUF zisifanyike kwa upande wao na upande wa Prof. Lipumba mpaka pale mahakama itakapotoa tafsiri ya katiba ya CUF kama kweli wanaamini/wanajua kuwa Prof. Lipumba sio Mwenyekiti au sio mwanachama wa CUF.
Maalim seif na kundi lake wanachokifanya kwa sasa ni reactive action badala ya proactive action.
Wanasubiri Prof. Lipumba akiwapiga ngumi, ndio wanaanza kutafuta mbinu ya kujikinga wakati ngumi imeishawapata. Kuendelea kupigwa ngumi na Prof. Lipumba watajikuta nguvu za reactive action zinawashia na hatimaye Prof. Lipumba kuibuka mshindi.
Anachokifanya Maalim Seif na kundi lake kwa sasa hakina tofauti na kuwa kwenye mtumbwi ndani ya bahari bila life jacket huku mwenzako akiwa amevaa life jacket. Kila akitoboa mtumbwi unahangaika kuziba lakini kabla hujamaliza kuziba anatoboa tena sehemu nyingine.
Maalim Seif na kundi lake wameshindwa kukubali kuwa walifanya kosa la msingi kwa kutoitisha kikao cha Baraza Kuu au Mkutano Mkuu kuridhia hatua ya Prof. Lipumba ndani ya zaidi ya miezi 10 tokea alipoandika barua ya kusudio la kujiuzulu Unyekiti wa CUF Taifa na baadaye kuandika barua ya kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu.
Kwa mujibu wa Katiba ya CUF, Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu Mkuu Msaidizi uamuzi wao wa kujiuzulu unapitishwa na Mkutano Mkuu wa CUF baada ya mtu anayekusudia kujiuzulu kuandika barua kwa Katibu Mkuu wa Chama, hata kama Katibu Mkuu asingekuwepo angeandika barua.
Ni jukumu la ofisi ya Katibu Mkuu kuitisha kikao cha Baraza Kuu ili kuandaa mkutano mkuu maalum kwa ajili ya kujadili jambo nyeti la aina hiyo. Endapo jambo hilo litatokea kipindi ambacho Mkutano Mkuu wa kawaida haujaitishwa kwa mujibu wa katiba, mkutano wa Baraza Kuu utajadili sababu za anayetaka kujiuzulu kwa kuziafiki au kuzipinga kabla ya Mkutano Mkuu haujaitishwa ndani ya muda unaokubalika kwa mujibu wa katiba ya CUF.
Maalim Seif hakuitisha Kikao cha Baraza Kuu ili kuandaa Mkutano Mkuu na kutokufanya hivyo kunamgharimu kila siku. Hili ni kosa ambalo Prof. Lipumba na kundi lake wamelitumia vizuri na wanaendelea kulitumia huku Maalim Seif akibaki kuhangaika na media.
Kama CUF Zanzibar wataendelea kuweka matumaini kwa Maalim Seif watajikuta hata kile kidogo walichonacho wanakikosa.
CUF Zanzibar lazima wakumbuke maneno ya Mjerumani, Albert Einstein aliposema, ‘’We cannot solve our problems with the same thinking we used when we created them’’.