Maalim Seif: Like a lamb to the slaughter!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,976
Kundi la Maalim Seif linachekesha kama sio kusikitisha!

Like a lamb to the slaughter ni nahau inayomaanisha mtu anafanya jambo bila kujua madhara yake na anafanya kwa upole bila kutumia njia mbadala ya kuzuia madhara yake. Ni kama kondoo anavyopelekwa kwenye machinjio kuchinjwa!

Kinachonishangaza kwenye kundi la Maalim Seif ni aina ya mbinu ambayo wamechagua katika mapambano na kundi la Prof. Lipumba.

Niliwahi kutoa ushauri kwa Maalim Seif kupitia thread hii;
LINK>>Maalim Seif tulikuambia achana na Lowassa, hukusikia!

Maalim Seif kama bado anadhani Edward Lowassa atamsaidia kutatua matatizo ya CUF atakuwa anapoteza muda wake!

Edward Lowassa ni mzuri katika mikakati ya kisiasa nchini katika mazingira kama umeshika dola lakini sio katika mazingira kama hujashika dola. Lowassa hajui fitina za kisiasa ukiwa upande wa upinzani kwa sababu maisha yake yote ya kisiasa amekuwa ndani ya CCM. Utazidi kupotea kisiasa kidogo kidogo kama utaendelea kuweka matumaini kwa Lowassa.

Maalim Seif na kundi lake wanadhani kutoa lawama na tuhuma nzito kwa taasisi ambazo ndizo wanazitegemea kuwasadia ndio watafanikiwa, lazima watambue kwa kufanya hivyo wanajidanganya na kujikaanga wenyewe.

Wakati Maalim Seif na kundi lake wamejikita kwenye media wakipiga kelele kutaka huruma kwa wananchi huku wakizituhumu taasisi zilizopewa mamlaka kisheria kushughulikia tatizo lao, mwenzao Prof. Lipumba na kundi lake wameamua kufanya mambo yao kimya kimya.

Ieleweke kuwa Prof. Lipumba na kundi lake wamekwenda mara nyingi mahakamani na kugonga mwamba lakini hawajatoa lawama kwa mahakama kwa sababu wanatambua madhara ya kutoa lawama kwa taasisi wanayoitegemea katika kutatua matatizo yao.

Moja ya njia ya kutatua tatizo kwa usahihi ni kuelewa chanzo chake, kuyatambua madhaifu na kuyakubali ili upate nafasi ya kutafuta majawabu sahihi.

Dhambi ya kuandika katiba ya CUF na kumpa Mwenyekiti wa CUF Taifa na Katibu Mkuu madaraka makubwa ndani ya chama kwa sasa inamtafuna Maalim Seif na kundi lake. Waingereza husema, ‘’What goes around comes around’’.

Kama isingekuwa ubinafsi wa Maalim Seif, kwa sasa wangekuwa wameenda mahakamani kuzuia kazi zote za CUF zisifanyike kwa upande wao na upande wa Prof. Lipumba mpaka pale mahakama itakapotoa tafsiri ya katiba ya CUF kama kweli wanaamini/wanajua kuwa Prof. Lipumba sio Mwenyekiti au sio mwanachama wa CUF.

Maalim seif na kundi lake wanachokifanya kwa sasa ni reactive action badala ya proactive action.

Wanasubiri Prof. Lipumba akiwapiga ngumi, ndio wanaanza kutafuta mbinu ya kujikinga wakati ngumi imeishawapata. Kuendelea kupigwa ngumi na Prof. Lipumba watajikuta nguvu za reactive action zinawashia na hatimaye Prof. Lipumba kuibuka mshindi.

Anachokifanya Maalim Seif na kundi lake kwa sasa hakina tofauti na kuwa kwenye mtumbwi ndani ya bahari bila life jacket huku mwenzako akiwa amevaa life jacket. Kila akitoboa mtumbwi unahangaika kuziba lakini kabla hujamaliza kuziba anatoboa tena sehemu nyingine.

Maalim Seif na kundi lake wameshindwa kukubali kuwa walifanya kosa la msingi kwa kutoitisha kikao cha Baraza Kuu au Mkutano Mkuu kuridhia hatua ya Prof. Lipumba ndani ya zaidi ya miezi 10 tokea alipoandika barua ya kusudio la kujiuzulu Unyekiti wa CUF Taifa na baadaye kuandika barua ya kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu.

Kwa mujibu wa Katiba ya CUF, Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu Mkuu Msaidizi uamuzi wao wa kujiuzulu unapitishwa na Mkutano Mkuu wa CUF baada ya mtu anayekusudia kujiuzulu kuandika barua kwa Katibu Mkuu wa Chama, hata kama Katibu Mkuu asingekuwepo angeandika barua.

Ni jukumu la ofisi ya Katibu Mkuu kuitisha kikao cha Baraza Kuu ili kuandaa mkutano mkuu maalum kwa ajili ya kujadili jambo nyeti la aina hiyo. Endapo jambo hilo litatokea kipindi ambacho Mkutano Mkuu wa kawaida haujaitishwa kwa mujibu wa katiba, mkutano wa Baraza Kuu utajadili sababu za anayetaka kujiuzulu kwa kuziafiki au kuzipinga kabla ya Mkutano Mkuu haujaitishwa ndani ya muda unaokubalika kwa mujibu wa katiba ya CUF.

Maalim Seif hakuitisha Kikao cha Baraza Kuu ili kuandaa Mkutano Mkuu na kutokufanya hivyo kunamgharimu kila siku. Hili ni kosa ambalo Prof. Lipumba na kundi lake wamelitumia vizuri na wanaendelea kulitumia huku Maalim Seif akibaki kuhangaika na media.

Kama CUF Zanzibar wataendelea kuweka matumaini kwa Maalim Seif watajikuta hata kile kidogo walichonacho wanakikosa.

CUF Zanzibar lazima wakumbuke maneno ya Mjerumani, Albert Einstein aliposema, ‘’We cannot solve our problems with the same thinking we used when we created them’’.
 
"Kama CUF Zanzibar wataendelea kuweka matumaini kwa Maalim Seif watajikuta hata kile kidogo walichonacho wanakikosa"

Maalim alizoea kuwa mtemi kwenye chama unaweza kusema cuf ni mali yake.
 
Mleta mada kwanini uwalaumu wanaofanyiziwa tena na dola?! Lipumba kasaidwa na police kufanya mapinduzi yale, au hukuona?! Lipumba kasaidiwa na msajili ktk swala la ruzuku au hiyo hukuiona?! Na sasa NEC na bunge navyo vinatumika!!

Nnacho kuuliza ulitaka Maalim atumie ghasia wakati amedhulumiwa na dunia inajuwa ?! Pro government muwe na soni japo kidogo kwa sababu kwa hali iliyopo wala Tz si mshindi bali kikundi cha watu waliojihalalishia utawala.

Cairo's
 
Huenda hili ni jibu la kile alichokifanya msajili leo kwa kusema hamtambui Maalim Seif kama katibu mkuu wa Cuf. Huu uzi wako ni mrefu ukidhani tutaamini kuna sheria zinafuatwa wakati tunaona ni hila za wazi tu. Kwa hili linaloendelelea Maalim amepoteza kwa uzembe wake wa kutoitisha kikao cha kujadili barua ya Lipumba, lakini kwa sehemu kubwa ni hila toka kwa watawala.
 
Kwenye Katiba ya CUF, Mwenyekiti wa Taifa ni mtemi, Katibu Mkuu naye ni mtemi!

Tatizo la kuandika katiba ya aina hii linakuja kama hawa viongozi wakuu wawili watashindwa kuelewana.
 
Dola ya kiafrika inaelewa lugha ya kutumia nguvu.
Hapa ndipo Maalim amechelewa.
Mzungu ni kama jini, mwambie nataka bunduki atakupa, mwambie nataka nipaze sauti dunia ijue nimedhulumiwa na atakupa vyombo vyake upaze sauti.

Maalim ni mfano mzuri sana wa siasa za kistaarabu.
Ila siasa hizo hazina nafasi Afrika.
Badala ya kwenda UN Maalim angewatembelea HAMAS au Hizboular na angeshatatua kero yake zamani sana.

Your right won't ever be given to you on a silver plate!
 
Mimi nafikiri kosa walilofanya ki binaadamu hawa viongozi wa vyama vya upinzani especially CUF na CDM ni kukubali kuachana uanaharakati na kujaribu kukumbatia siasa za kistaarabu!! Nasema hivyo kwa sababu serikali nyingi za kiafrika hawako ktk kustawisha democracy bali kuivuruga. Mifano ni mingi, lakini kwa uanaharakati hulazimisha watu kukaa mezani. Na ktk kukaa mezani kuna nipe nikupe. Ambayo kwa kiasi huleta usawa siyo hii ya watawala kutumia kodi na dola kudhoofisha democracy.

Cairo's
 
Mleta mada kwanini uwalaumu wanaofanyiziwa tena na dola?! Lipumba kasaidwa na police kufanya mapinduzi yale, au hukuona?! Lipumba kasaidiwa na msajili ktk swala la ruzuku au hiyo hukuiona?! Na sasa NEC na bunge navyo vinatumika!!

Nnacho kuuliza ulitaka Maalim atumie ghasia wakati amedhulumiwa na dunia inajuwa ?! Pro government muwe na soni japo kidogo kwa sababu kwa hali iliyopo wala Tz si mshindi bali kikundi cha watu waliojihalalishia utawala.

Cairo's
Kweli aisee
 
Mkuu;
Hakuna sehemu ambayo nimemlaumu mtu yeyote ila nimesema kile ninachodhani ni makosa ya Maalim Seif na kundi lake.

Nimesema haki inapatikana mahakamani na sio kwenye majukwaa ya habari na siasa lakini pia haki itapatikana kama kweli imechukuliwa bila ridhaa yao.

Maalim Seif na Prof. Lipumba ni kama ule msemo usemao, Waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba.
 
Wewe unaweza kuandika huu utumbo kwasababu ndio unafanya watoto wako waende haja!

Maalim angefanya tu short trip kwa Hizboular badala ya UN ungekuta watu wamekaa mezani zamani sana .
 
Bado wananchi wana hope na upinzani yaani wanaamini kuwa upinzani ni muhim kwa taifa na uhai wake.
Lakini kuna jitihana nyingi kuufuta upinzni kwa visingizio hewa. hii ndo hatari kubwa iliyopo.
 
Kundi la Maalim Seif linachekesha kama sio kusikitisha!

Like a lamb to the slaughter ni nahau inayomaanisha mtu anafanya jambo bila kujua madhara yake na anafanya kwa upole bila kutumia njia mbadala ya kuzuia madhara yake.

Kinachonishangaza kwenye genge la Maalim Seif ni aina ya mbinu ambayo wamechagua katika mapambano na genge la Prof. Lipumba.

Niliwahi kutoa ushauri kwa Maalim Seif kupitia thread hii;
LINK>>Maalim Seif tulikuambia achana na Lowassa, hukusikia!

Maalim Seif kama bado anadhani Edward Lowassa atamsaidia kutatua matatizo ya CUF atakuwa anapoteza muda wake!

Edward Lowassa ni mzuri katika mikakati ya kisiasa nchini katika mazingira kama umeshika dola lakini sio katika mazingira kama hujashika dola. Lowassa hajui fitina za kisiasa ukiwa upande wa upinzani kwa sababu maisha yake yote ya kisiasa amekuwa ndani ya CCM. Utazidi kupotea kisiasa kidogo kidogo kama utaendelea kuweka matumaini kwa Lowassa.

Maalim Seif na kundi lake wanadhani kutoa lawama na tuhuma nzito kwa taasisi ambazo ndizo wanazitegemea kuwasadia ndio watafanikiwa, lazima watambue kwa kufanya hivyo wanajidanganya na kujikaanga wenyewe.

Wakati Maalim Seif na kundi lake wamejikita kwenye media wakipiga kelele kutaka huruma kwa wananchi huku wakizituhumu taasisi zilizopewa mamlaka kisheria kushughulikia tatizo lao, mwenzao Prof. Lipumba na kundi lake wameamua kufanya mambo yao kimya kimya.

Ieleweke kuwa Prof. Lipumba na kundi lake wamekwenda mara nyingi mahakamani na kugonga mwamba lakini hawajatoa lawama kwa mahakama kwa sababu wanatambua madhara ya kutoa lawama kwa taasisi wanayoitegemea katika kutatua matatizo yao.

Moja ya njia ya kutatua tatizo kwa usahihi ni kuelewa chanzo chake, kuyatambua madhaifu na kuyakubali ili upate nafasi ya kutafuta majawabu sahihi.

Dhambi ya kuandika katiba ya CUF na kumpa Mwenyekiti wa CUF Taifa na Katibu Mkuu madaraka makubwa ndani ya chama kwa sasa inamtafuna Maalim Seif na kundi lake. Waingereza husema, ‘’What goes around comes around’’.

Kama isingekuwa ubinafsi wa Maalim Seif, kwa sasa wangekuwa wameenda mahakamani kuzuia kazi zote za CUF zisifanyike kwa upande wao na upande wa Prof. Lipumba mpaka pale mahakama itakapotoa tafsiri ya katiba ya CUF kama kweli wanaamini/wanajua kuwa Prof. Lipumba sio Mwenyekiti au sio mwanachama wa CUF.

Maalim seif na kundi lake wanachokifanya kwa sasa ni reactive action badala ya proactive action.

Wanasubiri Prof. Lipumba akiwapiga ngumi, ndio wanaanza kutafuta mbinu ya kujikinga wakati ngumi imeishawapata. Kuendelea kupigwa ngumi na Prof. Lipumba watajikuta nguvu za reactive action zinawashia na hatimaye Prof. Lipumba kuibuka mshindi.

Anachokifanya Maalim Seif na kundi lake kwa sasa hakina tofauti na kuwa kwenye mtumbwi ndani ya bahari bila life jacket huku mwenzako akiwa amevaa life jacket. Kila akitoboa mtumbwi unahangaika kuziba lakini kabla hujamaliza kuziba anatoboa tena sehemu nyingine.

Maalim Seif na kundi lake wameshindwa kukubali kuwa walifanya kosa la msingi kwa kutoitisha kikao cha Baraza Kuu au Mkutano Mkuu kuridhia hatua ya Prof. Lipumba ndani ya zaidi ya miezi 10 tokea alipoandika barua ya kusudio la kujiuzulu Unyekiti wa CUF Taifa na baadaye kuandika barua ya kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu.

Kwa mujibu wa Katiba ya CUF, Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu Mkuu Msaidizi uamuzi wao wa kujiuzulu unapitishwa na Mkutano Mkuu wa CUF baada ya mtu anayekusudia kujiuzulu kuandika barua kwa Katibu Mkuu wa Chama, hata kama Katibu Mkuu asingekuwepo angeandika barua.

Ni jukumu la ofisi ya Katibu Mkuu kuitisha kikao cha Baraza Kuu ili kuandaa mkutano mkuu maalum kwa ajili ya kujadili jambo nyeti la aina hiyo. Endapo jambo hilo litatokea kipindi ambacho Mkutano Mkuu wa kawaida haujaitishwa kwa mujibu wa katiba, mkutano wa Baraza Kuu utajadili sababu za anayetaka kujiuzulu kwa kuziafiki au kuzipinga kabla ya Mkutano Mkuu haujaitishwa ndani ya muda unaokubalika kwa mujibu wa katiba ya CUF.

Maalim Seif hakuitisha Kikao cha Baraza Kuu ili kuandaa Mkutano Mkuu na kutokufanya hivyo kunamgharimu kila siku. Hili ni kosa ambalo Prof. Lipumba na kundi lake wamelitumia vizuri na wanaendelea kulitumia huku Maalim Seif akibaki kuhangaika na media.

Kama CUF Zanzibar wataendelea kuweka matumaini kwa Maalim Seif watajikuta hata kile kidogo walichonacho wanakikosa.

CUF Zanzibar lazima wakumbuke maneno ya Mjerumani, Albert Einstein aliposema, ‘’We cannot solve our problems with the same thinking we used when we created them’’.
Lipumba anatumiwa na serikali ya ccm kama condom
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom