Maalim Seif Kuburuzwa Mahakamani?

Mtanganyika

JF-Expert Member
Jul 18, 2007
1,601
944
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), kisiwani Pemba, imesema inamchunguza Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Seif Shariff Hamad, kama alichochea wafanyabiashara wa Pemba kususia kuuza mazao yao Unguja na kama itaibinika hivyo watamshitaki.

Kadhalika kiongozi huyo atafikishwa mahakamani kama pia itabainika kuwa ameshawishi wafanyabiashara kuwabagua wateja wanaowauzia bidhaa madukani kwa misingi ya itikadi.

Tamko hilo lilitolewa na Wakuu wa Mikoa miwili ya Pemba, Bw. Dadi Faki Dadi na Bw. Juma Kassim Tindwa, wanaowakilisha mamlaka ya utawala katika kisiwa hicho.

``Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini, tahadhari mti na macho tutamchukulia hatua yeyote, hatumuogopi mtu? Seif hatumuogopi. Yeyote anayevunja sheria atachukuliwa hatua... Juzi maduka 10 tumeyafungia kama watayafungua tutawapeleka polisi na kuwafungulia mashtaka na wengine wakiendelea tutawafungia,`` alisema Bw.Tindwa.

Walisema wafanyabiashara 10 kisiwani humo wamefungiwa leseni baada ya kubainika kuwa wanafanyabiashara kibaguzi na kuwanyima huduma wateja wenye itikadi tofauti.

Akizungumza kwenye mahafali ya Chuo cha Ualimu cha Benjamin Mkapa Wete kisiwani Pemba, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, aliongeza kuwa vitendo vya kuwashawishi wafanyabiashara kutouza mazao yao Unguja na kubagua wateja kwa misingi ya kiitikadi vinakiuka masharti ya leseni na ya haki za binadamu.

Aliwashangaa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na wabunge wa CUF wanaohudhuria vikao na kulipwa posho na SMZ lakini wanathubutu kuwahamasisha raia wasiuze mazao Unguja wakati wakijua kuwa uamuzi huo utaathiri mapato ya wananchi?

``Wananchi wanafanyabiashara ili kupata fedha za kuendesha, maisha kama kususia waanze Wawakilishi na Wabunge ambao wanahudhuria vikao na kulipwa posho, huku Hamad akilipwa mafao na serikali,`` alisema Bw. Tindwa.

Aliwataka wafanyabiashara kujua kuwa iwapo maduka yao yatafungwa wao ndiyo watakaoathirika.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Bw. Dadi, alisema licha ya wafanyabiashara kupinga ushauri huo wapo baadhi ya wanasiasa wanaowashawishi kutoa huduma kwa ubaguzi na itikadi za kisiasa.

Walipinga madai ya viongozi wa CUF kuwa Wapemba wametengwa kimaendeleo ikilinganishwa na Unguja wakisema hayana msingi kwa vile huduma za jamii zinatolewa pote visiwani.

SOURCE: Nipashe
 
Swali ni moja tuu, jee kwa kutowauzia chakula waunguja wanakiuka sheria? Jee hiyo ni sheria gani? Kwa nini watu wanyang'anywe leseni zao sababu wamechagua nani wa kumuuzia? Jee kuna sheria inayolinda hiiyo. Kama hapa US kuna commerce clause ambayo inawabana wafanya biashara. Jee Tanzania kuna statute yoyote?
 
thread-fail-stamp.gif
 
Hakuna lolote Wahindi walipinga kununua bidhaa za muingereza na hata kuacha kupanda train ,lipi jipya kwa wapemba ,juzi tu wamewafungia wapemba maduka kiasi ya maduka kumi yamefungwa ,hakuna sababu ya wenye maduka hao kutowauzia bidhaa wafuasi wa CCM ,hilo sio kweli kwani Pemba kama kuna wafuasi wa CCM basi ni wafuasi kadi tu.
Ila siri iliyokuwepo hapa ni kufunga maduka muhimu yanayoonekana kutoa huduma kwa wapemba ili kujibu mapigo ya kutopeleka bidhaa Unguja ,hilo ndilo jambo kubwa ambalo wamelitafutia sababu,na bado wataendelea kuyafunga maduka yale yote yaliomstari wa mbele wakisaidiwa na askari kanzu.
Jengine ni kutaka kuzima harakati za kuilazimisha Serikali ya Karume ijiuzulu kwani inaelekea mwezi sasa imeshindwa kuurudisha umeme na sasa shida inaanza kutambalia masha ya watu hapo Unguja ,ni habari za kusikitisha kusikia makundi ya watoto wachanga yameanza kulundikana kwenye hospitali kuu ya Mnazi mmoja wakishambiliwa na marazi ya tumbo tena tumbo la kuhara na kutapika ,ingawa serikali imezidi kubana kutangaza kuwa janga hilo ni maradhi ya cholera lakini wachunguzi wa mambo wanasema tayari unguja imeshakumwa na gonjwa hilo hatari ,kinachosubiriwa ni nani ataanza kupoteza roho.
Mbali ya kujitapa kuwa mafundi watafika au wameshafika na eti serikali imeweka majenereta kwenye mashine za kusukumia maji lakini kila siku zinavyozidi ndivyo uongo wao unavyozidi kutoka nje ,kuna habari kuwa kisiwa cha Tumbatu nacho kimeshakauka maji na kilikuwa kinategemea maji ya kutoka kwenye mashine za serikali ,lakini sasa watu wameanza kupanda ngalawa na kwenda kutafuta maji kusiko julikana.
Tayari wananchi wenye hasira wameanza kuitupia lawama Serikali ya Muungano ,wananchi hao wamedai hakuna hata kiongozi mmoja aliefika kujulia ni nini kinachoendelea.Na lipi linalongojewa na ni kitu gani kilichowazuia kufika Unguja ? Je huu ndio Muungano unaotakiwa baina ya Nchi mbili .
Masuali ni mengi na majibu hakuna ,Kikwete ametunisha msuli Karume nae kawa bubu.
Wanaojisubirisha ni wananchi kutoa msimamo wao dhidi ya serikali.
 
Ya pemba nayo Mhh ebu wanasheria tupeni maoni yenu wengine hatujui sheria zinasemaje. Unajua wakati mwingine hawa wakuu wa mikoa huwa wanakurupuka tu hata sheria hawajui. Si unajua wengine hata shule ilikuwa ni kuimba ccm oyee majukwani tu? anapewa cheo? namkumbuka mkuu wa wilaya mmoja mstaafu sasa kule Kagera katika mkutano wa hadhara akiwa kama MC wakati wa Mwinyi, alisema kama utani "kabla hujaondoka mheshimiwa usitusahau na sisi angalau ukuu wa wilaya" na wiki iliyofuatwa akatangazwa kawa appointed mkuu wa wilaya!? Shame!
 
kuna habari kuwa kisiwa cha Tumbatu nacho kimeshakauka maji na kilikuwa kinategemea maji ya kutoka kwenye mashine za serikali ,lakini sasa watu wameanza kupanda ngalawa na kwenda kutafuta maji kusiko julikana.
Kamanda Duuh!
Baada ya kuishambulia pemba na wapemba wake naona sasa umeamua kuhamia Tumbatu...MMhm! Tumbatu wana visima kibao vya maji tena visivyohitaji pump za kutumia umeme... Iwapo wapemba wangekuwa wanajituma katika kujali makaazi yao kama hawa watumbatu basi kisiwa kile kingekuwa paradise ya Zenj...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom