Maalim Seif: Kikwete ndio adui wa Wazanzibar

Ngaliba Dume

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,710
3,675
Maalim Seif Sharif Hamad anazungumza na viongozi wa CUF wa Wilaya zote na Majimbo yote ya Unguja muda huu kwa lengo la kuwafafanulia Azimio la Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama la kutoshiriki kile kinachoitwa uchaguzi wa marudio uliotangazwa na Jecha Salim Jecha.

Maalim Seif anasisitiza kwamba uchaguzi ulishafanyika na kukamilika tarehe 25 Oktoba, 2015 na umethibitishwa na waangalizi wote kuwa ulikuwa uchaguzi huru na wa haki. Waangalizi hao ni pamoja na wale wa Jumuiya ya Madola (The Commonwealth), Umoja wa Ulaya (European Union), Umoja wa Afrika (African Union), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na waangalizi kutoka nchi za Marekani na Uingereza.

Anasema kwamba kitendo cha kupindua maamuzi ya Wazanzibari kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 kilifanywa kwa baraka zote za aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wakati huo, Jakaya Kikwete. Anasema hakuna mtu mbaya kwa Zanzibar na Wazanzibari kama Jakaya Kikwete. Kwa hivyo, anasema kudai kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano hana mamlaka kuliingilia kati suala la Zanzibar ni unafiki wa hali ya juu.

Maalim Seif ameweka msimamo wa CUF hadharani kwamba uchaguzi wa marudio si halali na si ufumbuzi wa mkwamo wa uchaguzi uliopo huku akisisitiza kwamba uchaguzi ulishafanyika tarehe 25 Oktoba, 2015.

Amewaeleza kwa kina yaliyojiri katika vikao 9 vya mazungumzo kati yake na Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na Marais wastaafu na kuweka wazi kwamba mazungumzo hayo hayakufanikiwa kwa sababu Dk. Shein hana nia njema na si mkweli. Amesema Dk. Shein ni mtu anayeamini kutawala kwa mabavu na matumizi ya nguvu na asiyejali wala kuheshimu Katiba.

Maalim Seif anawataka wana - CUF kutembea kifua mbele wakijua kwamba wao ndiyo WASHINDI HALALI wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar.

Amemalizia kwa kusisitiza tena kwamba msimamo wa CUF kama ulivyotangazwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa UKO PALE PALE!
Chanzo:Ismail Jussa Fb Account
 

Attachments

  • image.jpeg
    image.jpeg
    39.2 KB · Views: 80
  • image.jpeg
    image.jpeg
    39.8 KB · Views: 77
Zanzbar Inahitaji Maombi !
Lakini inahitaji Ukweli zaidi !!

Kuna watu wanapotosha kuhusu Uchaguzi wa Zanzibar wakidai ni wa marudio !

Ukweli ni kwamba ni Uchaguzi mpya unohitaji
Kuanza Upya Na wagombea waombe upya!!

Sifa za Uchaguzi wa Marudio kwa mujibu wa sheria duniani kote:

Kwanza :
Uchaguzi wa marudio
ni
ule ulioharibika kwenye
baadhi
ya maeneo ,Na hurudia maeneo husika .

Pili :
Uchaguzi wa Marudio ni ule ambao unaoongozwa

Na Sheria inayomtaka mshindi
kupata asilimia ya kura zaidi nusu ya waliopiga kura ,

Sifa za Uchaguzi uliofutwa :

1:Uchaguzi uliofutwa ni zaidi ya kuharibika''

2:Ni kama hakuna kilichokuwa kinafanyika

3heria zilikiukwa
kuanzia Uteuzi wa wagombea ,,,'

4:Wapiga kura walio wengi
hawakuwa Na sifa za kupiga kura

5:Upigaji kura haukukamilika katika maeneo yaliyo
Mengi !

6:Ni vigumu kuyatambua Na kuhakiki matokeo yaliyotoka vituoni. Nk

7:Ni kitu cha kuanza Upya kila hatua ikiwemo uteuzi wa wagombea

Kwa Maoni yangu :

Hii Tabia ya kurudia Mtihani
darasa zima, Kisa Mtoto wa
mwaalimu kafeli !!

Ikiendekezwa itatupeleka Tanzania pabaya !

Mwana wa Adili :
Kiwaryalema
 
hivi kwani ccm wasipoongoza huko zenj watapungukiwa na nini?
 
Huyu Maalim Seif atulie tu. kadri anavyoongea anazidi kujidhalilisha. Ameamua kutoshiriki uchaguzi akae pembeni

SI YEYE PEKEE YAKE ANAYE ENDELEA KUONGELEA JUU YA MKWAMO HUO, , JE HAO WENGINE HAWAJIDHALILISHI KAMA UNAVYOFIKIRI WWW? TAFAKARI KWANZA !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Zanzbar Inahitaji Maombi !
Lakini inahitaji Ukweli zaidi !!

Kuna watu wanapotosha kuhusu Uchaguzi wa Zanzibar wakidai ni wa marudio !

Ukweli ni kwamba ni Uchaguzi mpya unohitaji
Kuanza Upya Na wagombea waombe upya!!

Sifa za Uchaguzi wa Marudio kwa mujibu wa sheria duniani kote:

Kwanza :
Uchaguzi wa marudio
ni
ule ulioharibika kwenye
baadhi
ya maeneo ,Na hurudia maeneo husika .

Pili :
Uchaguzi wa Marudio ni ule ambao unaoongozwa

Na Sheria inayomtaka mshindi
kupata asilimia ya kura zaidi nusu ya waliopiga kura ,

Sifa za Uchaguzi uliofutwa :

1:Uchaguzi uliofutwa ni zaidi ya kuharibika''

2:Ni kama hakuna kilichokuwa kinafanyika

3heria zilikiukwa
kuanzia Uteuzi wa wagombea ,,,'

4:Wapiga kura walio wengi
hawakuwa Na sifa za kupiga kura

5:Upigaji kura haukukamilika katika maeneo yaliyo
Mengi !

6:Ni vigumu kuyatambua Na kuhakiki matokeo yaliyotoka vituoni. Nk

Zanzibar sivyo ilivyokuwa !!

7:Ni kitu cha kuanza Upya kila hatua ikiwemo uteuzi wa wagombea

Kwa Maoni yangu :

Hii Tabia ya kurudia Mtihani
darasa zima, Kisa Mtoto wa
mwaalimu kafeli !!

Ikiendekezwa itatupeleka Tanzania pabaya !

Mwana wa Adili :
Kiwaryalema
 
Back
Top Bottom