Maalim SEIF Jijini MWANZA

ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,906
6,909
Jana Maalim Seif, makamu wa kwanza wa rais SMZ, alitua Mwanza airport na kusababisha kama kawaida adha kubwa kwa watumiaji wengine wa barabara, baada ya vipenyo na barabara zote alizopanga kupitia kufungwa ili yeye apite kwa amani na kwa heshima kubwa kama kiongozi.

Alitokea airport, akaenda kupata lunch Gold Crest Hotel, akaenda kwa Kabwe Wilson ofisi za jijini na baadae kuelekea wilayani Kwimba.

Masuala ninayojiuliza ni haya:

(a) Maalim Seif, ana wajibu kikatiba wa kufanya ziara jijini Mwanza ikizingatiwa yeye ni kiongozi wa SMZ?
(b) Na kwimba alienda kufanya nini?

MAALIM SEIF MKURUPUKO HUU WOTE KILA KONA TANZANIA BARA HUKO 'KIJANI ZAMBAU' KUNANI?

Hivi huyu baba mbona anamaliza soli ya kiatu chake kote Tanzania Bara kiasi hiki mara baada yaa kudumazwa muda mwingi na kuku na asali wa 'Serikali ya Umoja Zanzibar' kwenye mrija na sasa kuanza kukurupuka ovyo mitaa yote hivi??

Je, inakua vipi kwa Maalim Seif yeye aone utamu wa kurandaranda mikoa yote Bara bila bughudha yoyote wala kubaguliwa na mtu wakati kwake yeye kwenye kile kinachoelezewa kuwa ni ngome yake kule Pemba pindi vyama
vingine vinapodhmirie kwenda huko kuuza sera zao yeye HUTIA NGUVU, HUKODISHA WAHUNI KUSHAMBULIA VYAMA PINZANI KWAKE na hata kudiriki kuamsha Udini na Ubara huko kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotuelekeza??????

Hapana mkurupuko huu lazima kuna mtimua nyongo hukokwenye serikali ya Umoja wa Zanzibar na pengine jambo zito zaidi liko nyuma ya mzani wa kupimia nyama kwa namna ambavyo sisi wanunuzi wa ujumbe anaotembeza hivi sasa kamwe halijawa wazi kwetu.
 
Inabidi awekwe pembeni hana msaada tena katika muongo wa pili wa karne ya 21. Hawa wazee kasi ya mabadiliko ya dunia hawaiwezi. Cha kushangaza hata hawataki kujenga misingi imara ya taifa wanabaki kulipuana na kukomoana kila siku.
 
Katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania haimtambui Seif Shariff, Iki ni kiburi cha viongozi wetu wa nchi kuvunja katiba kwa makusudi na hali walikula kiapo cha kuilinda katiba yetu.
Huu ndio utawala wa sheria. Wamethubutu wameweza na wanasonga mbele we hata ukipiga vipi kelele hawakujali.
 
Huyu anafukuzana na kivuli cha Hamad Rashid. Msafara wake unapaswa kuwa wa magari ya chama chake na si ya serikali. Hiki ni kieelelezo cha jinsi serikali yetu inavyotumia rasirimali zake ovyo.
 
Huyo keshapata alichokitaka. Amewasahau watu wake walozama Pemba!!
 
Kwa nini Maalim Seif atumie rasilmali za serikali ya Zanzibar kuendeshea kampeni binafsi za Chama Cha Wananchi KAFU huku Tanzania Bara?

Kama Mgonja tuliweza kumfungulia kesi ya matumizi mabaya ya ofisi huko nyuma je, kwa huyu bwana anayetugasi na vingora kila mkoa huku Tanzania Bara asikotambulika kisheria ni kwamba tunangoja nini kote huko?
 
Jana Maalim Seif, makamu wa kwanza wa rais SMZ, alitua Mwanza airport na kusababisha kama kawaida adha kubwa kwa watumiaji wengine wa barabara, baada ya vipenyo na barabara zote alizopanga kupitia kufungwa ili yeye apite kwa amani na kwa heshima kubwa kama kiongozi.

Alitokea airport, akaenda kupata lunch Gold Crest Hotel, akaenda kwa Kabwe Wilson ofisi za jijini na baadae kuelekea wilayani Kwimba.

Masuala ninayojiuliza ni haya:

(a) Maalim Seif, ana wajibu kikatiba wa kufanya ziara jijini Mwanza ikizingatiwa yeye ni kiongozi wa SMZ?
(b) Na kwimba alienda kufanya nini?

Ndevu hana lolote yote hiyo ni katika harakati za kumshughulikia Mpiganaji HAMAD RASHID..ikulu ya zanzibar sasa haikaliki tena mpaka HAMAD RASHID akione cha moto,mbaya zaidi ni tax payers money ndio inayotumika!
 
Hapana mkurupuko huu lazima kuna mtimua nyongo hukokwenye serikali ya Umoja wa Zanzibar na pengine jambo zito zaidi liko nyuma ya mzani wa kupimia nyama kwa namna ambavyo sisi wanunuzi wa ujumbe anaotembeza hivi sasa kamwe halijawa wazi kwetu.

".......amelaniwa mtu yeyote amfanyae binadamu kuwa kinga yake mwenyewe......." mithali

Leo ndo safari ya kwenda Kwimba

Kijiji wanachokwenda KUGANGWA, kinaitwa KINYAMPANDE

Ndevu hana lolote yote hiyo ni katika harakati za kumshughulikia Mpiganaji HAMAD RASHID..ikulu ya zanzibar sasa haikaliki tena mpaka HAMAD RASHID akione cha moto,mbaya zaidi ni tax payers money ndio inayotumika!

Kwimba kuna mganga mashuhuri mpaka kajengewa nyumba na serikali, Kikwete kila mara lazima aende kuhiji pale
 
seif mpemba hawezi kufuata uganga kwimba....akauacha mwambe na bumbwini...!yuko katika ziara za 'kuimarisha uhai" wa chama tu

NDO ATUMIE POLISI WA TANZANIA? NDO ATUMIE MAGARI YA SERIKALI YA TANZANIA? NDO AFUNGE ROAD ILI YEYE APITE?

Katishiwa kuvuliwa ukatibu, msasa anaganga kila kona. Kwani Kikwete anayeenda kila mara, bagamoyo hawako?
 
polisi wako tayari kuongoza msafara, vingo'ora vinalia, barabara zimefungwa
 
Nadhani Maalimu anataka kupewa uraisi wa znz 2015 huku shein akirudi ikulu ya magogoni kama boss, tutegemee vizee vya miaka 80 kushika nyadhifa kubwa jan 2016,
 
Ukiona twiga anatisha kila kijiji kwa spidi kama hii tena akila majani tu ya chini basi moja kwa moja ujue kwenye mtu kule matawini kuna jambo.
 
Hizo barabara na vichochoro vilifungwa kwasababu gani? Katiba ya JMT inawatambua viongozi wakuu
wa SMZ ambao ni Rais wa SMZ na Waziri kiongozi. Maalimu Seif ni kama mpemba tu mwingine aliyekuja
kuitembea Mwanza. Je kila Mpemba atakayekuja kutembea Mwanza barabara zote zitafungwa na kupewa
lunch Gold Crest, Sijui kwa gharama za nani?

Hivi kwanini JK huyu anaendelea kuvunja katiba ya JMT ambayo aliapa kuilinda? Mbaya zaidi na sisi Mi-Tanganyika
tupo tu kimya tunamkenulia meno bila kuchukula hatua.
 
Hivi kwanini JK huyu anaendelea kuvunja katiba ya JMT ambayo aliapa kuilinda? Mbaya zaidi na sisi Mi-Tanganyika
tupo tu kimya tunamkenulia meno bila kuchukula hatua
.

we mweneyewe mbaya, kwani9 zaidi ya kuandika kwa jazba humu ndani, kipi umefanya cha kukumbukwa? shme on all Tanganyikans
 
hivi ninyi wafurukutwa wa chama cha maandamano na migomo mmekosa cha kuongea ila ni kumsema maalim sefu na kufuatilia ziara zake mpaka chooni? sefu ni mtanzania, katibu mkuu wa cuf, na zaidi ni makamu wa kwanza wa rais wa serikali ya umoja wa kitaifa zanzibar ambayo KATIBA yake inatambuliwa rasmi na katiba ya muungano hivyo acheni ubaguzi wenu na upuuzi wenu ninyi wana chama wa chama cha maandamano na migomo.

SIMPLE MIND DISCUSS PEOPLE.....
 
Maalim Seif nadhani akiwa kwenye Ziara za Tanzania bara anatakiwa kuwa kama katibu mkuu wa chama chake na si kama Makamu wa Rais smz..Sasa hapo wasomi wanaiojua Katiba ya njii waseme what next..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom