Maalim Seif Atinga Washington DC na ujumbe wake

usipotoshe umma. wakati ASP ikitetea maslahi ya mzanzibar mnyonge, ZPPP ilikuwa ikitetea maslahi ya waarabu wachache kutoka Oman, na kile kikundi cha wachache kikapewa uhuru Dec 1963, na baadae kupinduliwa na wanyonge kwa maslahi ya wote ASP na Karume akawa Rais
 
japo ni kweli kufutwa kwa uchaguzi wa October kulikuwa ni haramu, lakini kwa vile hakuna yoyote aliyepinga rasmi haramu ile, kutokupinga huko, kumeihalalisha haramu ile kugauka halali!,
Sura zote tatu za mtu mnafiki umezionesha Pasco. Hata kama utajipanga rangi tofauti utabakia kinyonga tu.

Bila ya haya wala aiby ya nafsi unasema kufutwa kwa uchaguzi wa October kulikuwa ni haramu, lakini kwa vile hakuna yoyote aliyepinga rasmi haramu ile!!! ulitaka ipingwe kwa hali gani? watu waingie mitaani na kupotezeana maisha> au wende mahakamani wakati sheria inasema uamuzi wa Tume ni wa mwishona hauwezi kupingwa kwenye mahakama.Sisi ni wastaarabu, kuna njia lukuki za kiungwana za kupinga kilichotokea. Sisi si "wakuja" wa kuchagua fujo ndio njia sahihi ya "kudai haki" ijapokuwa tumeonesha wingi wetu.

Kupinga kitu haimaanishi kubeba Rocket Launcher na vifaru mitaani, kuchukia tu kunatosha kuonesha hisia kutoka watu wastaarabu na wazawa kwa tunapinga na hatukubaliani.

Nilisema hapo kabla na nasema tena, wazawa wa Zanzibar ni watu wastahamilivu, waungwana na wachamungu. Walikaa miaka 200 chini ya utawala wa kidhalimu wa kireno,wazee wetu hawakutetereka, walibaki na imani yao na kuirithisha kizazi kwa kizazi, mpaka mungu aliposikia sala zetu kwa udhalimu wa kireno kupotea. Sasa ni kuzidisha ibada na kumuomba mola ili hawa mahasidi zetu awajaze khofu ndani ya mioyo yao na kuwazindua kusimamia haki na unyenyekevu wa kufuata sharia!
 
Kwanza kwenu wapi? tusihangaishaene. Unajua walioanzisha ASP na unawajua walioanzisha ZPPP?

Walioanzisha ASP ni Sheikh Ameir Tajo (MBE), Mwanasiasa wa mwanzo mshirazi ( mzawa) na alietunukiwa nishani na Malkia wa Uingereza.

ASP klimeguka baada ya wazawa kutoridhishwa na uvamizi wa " wakuja" kwenye chama na wakaunda chama chao cha wazawa ZPPP kikiongozwa na Moh'd Shamte na Ameir Tajo, wote wazawa asilia. Alau kama ungesema ZNP Kikitetea maslahi ya waarabu ingeingia akilini sio ZPPP.

Waaarabu wa Oman waliozaliwa Zanzibar kizazi kwa kizazi tokea mwaka 1698 huwezi kuwafafanisha na Karume wa 1905 kutoka malawi.
 
ASP ikitetea maslahi ya mzanzibar mnyonge
Mzanzibari mnyonge 1963 , leo amezidi kuwa mnyonge marudufu. Yeye alipokwenda shule alikuwa anakaa kwenye dawati,maziwa kila siku wakati wa mapumziko, shida ilikua kutafuta kuni tu, health care inafuata mashuleni, michezo ( vifaa), vyoo vya kutosheleza, vifaa vya kuandikia nakusomea kedekede na vyote bure na bila mchango wowote. Leo imekuwa hadithi ya kusimulia wajukuu na watoto.
 
ajenda ya ZPPP hazikuwa na maslai mapana kwa taifa la Zanzibar
Unaelewa kiswahili vizuri, soma hii tena "ASP klimeguka baada ya wazawa kutoridhishwa na uvamizi wa " wakuja". Sasa utasemaje agenda ya ZPPP hazikuwa na maslahi na Zanzibar wangejimegua na ASP
 
Huu mjadala huko vizur maamae tatizo mda wa kaz. Nikmaliza hii ngwe ya pili saa kumi nataka niingie library niuosome wote pamoja na comments. Imenifanya niwe interested kuisoma zenj kiundan sikuwajua akina mwinyimkuu cjui mamtuba big up jf big up pasco na baraghash yani mnabishana kwa hoja had raha. Vionjo kama hiv mnaviposti Kwanzaa jmos asibahi
 

Mkuu Baragash, maelezo yako yanaweza kuwa ya ukweli kutokana na itikadi uliyonayo kuhusu unavyotamani Zanzibar iwe. Kuna mchanganyiko wa maelezo ambayo yapo halali kihistoria, lakini pia, unachomekea mambo mengi yanayokuza itikadi yako " ya kuendeleza ubaguzi". Maneno yako hapo juu, ni maneno yanayoendeleza chuki na kutokutoa mwelekeo wa kutatua tatizo la Zanzibar. Kama wewe ni mmoja wa wasemaji wakuu wa hilo kundi linaloendeleza huo ubaguzi,waambie wenzio kuwa mwaiangamiza Zanzibar. Mnahitaji kutulia, na kutatua matatizo ya Zanzibar kwa kutokuendelea kubaguana.
 
Nina heshimu na mtazamo wako mkuu na kwa hilo nakushukuru. Ila umeghafilika kueleza mchango wa " mamluki" katika chaguzi zote za Zanzibar ni donda ndugu na ndio linalotupeleka pabaya na kupelekea dhana ya kibaguzi ya wazawa na wakuja.Ina uma sana mtu aliezaliwa Zanzibar lakini anakoseshwa haki ya kitambulisho cha kuweza kupiga kura na wakuja anakuja Zanzibar mwezi mmoja anapata shahada ya kupiga kura kwa sababu atapigia chama fulani. Nisaidie msamiati sanifu wa kuelezea hali hii na ifahamike
 
Ina uma sana mtu aliezaliwa Zanzibar lakini anakoseshwa haki ya kitambulisho cha kuweza kupiga kura na wakuja anakuja Zanzibar mwezi mmoja anapata shahada ya kupiga kura kwa sababu atapigia chama fulani.
Kwa maelezo yako, pamoja na maelezo ya Pasco, inaonyesha kuwa Zanzibar kuna tatizo kubwa la watu kubaguana na pia zinatumika mbinu mablimbali kutaka kutatua tatizo hilo bila kuangalia "root causes" za tatizo. Mbinu za kutumia "mamaluki" kwa mfano, ni njia nzuri kwa kundi moja na mbaya kwa kundi jingine, kama ulivyoeleza katika post yako na litaendeleza mgogoro. kwa watu kama wewe ambao wamaeyaona hayo, ni kuyaweka wazi kwa umma( kama unavyofanya hapa), na kutafuta njia zisizo za kibaguzi katika kutatua suala hili. Ni tatizo lililodumu kwa miaka mingi sana ( kama ulivyoeleza historia yake...ofcourse mimi sijui sana kama hiyo historia ni sahihi) , lakini halijafikia kuwa sugu kama tatizo la wapalestina na waisrael. Hili la kwetu, linaweza tatulika kwa upendo , bila chuki au umwagaji wa damu.
 
Sisi tunadai Zanzibar yetu, Lamu na Mombasa tumeiuza kwa Kenya na tumelipwa na Kenya, Bagamoyo na Tanganyika tuliiuza kwa Mjarumani,nakuletea ujinga wako!
Zanzibar tunawadai chenji yetu tu, nenda kamuulize Sultan Baraghash
 
Unaelewa kiswahili vizuri, soma hii tena "ASP klimeguka baada ya wazawa kutoridhishwa na uvamizi wa " wakuja". Sasa utasemaje agenda ya ZPPP hazikuwa na maslahi na Zanzibar wangejimegua na ASP
....Wapemba walinunuliwa na waarabu wakaambiwa wao ni karibu na mwarabu ! Ndio maana Pemba nzima bado kasumba inawasumbua !
 
Lol,duh hatari tuombe M/Mungu atustiri. Tatizo ni 'Mindset' ya huyu baraghash,anakuja na point lakini mtizamo wake upo kwenye kuona kizazi cha waarabu waamiaji waislamu wana haki kuliko waamiaji wengine,unaweza kukuta yeye mwenyewe kachanganya zaidi ya mara kumi!hii ni hatari maneno haya angeyasema native wa zanzibar 'Mtumbatu' ningemwelewa.Anasahau kuwa majority zanzibar ni watu wenye asili ya bantu.Mi nawaonea huruma sana hawa jamaa kisiwa chenye kidogo,watu wachache,wengi wavivu wa kazi,elimu ndio wanajivuta sasa na bado wanalo zigo la kubaguana!karume na nyerere walifanya jambo bora sana kuungana naona walishawastukia hawa jamaa.
Peace!!!
 
Sultan barghash haya maneno utayasema tena mwaka 2020 trust me.na mwaka 2025 utasema hayo hayo. Wanaume watakamata tena nchi na ukiuza Rais wa tanzania inayemzingumzia wewe hatokuwepo.

Mi nadhan kwa sasa tujikite kwenye kulima karafuu na pia tukipata muda tujichezee bao tu.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…