Maalim seif aonya viongozi wanaovuruga amani

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=1]
k1.JPG
[/h]Written by Elbattawi // 23/09/2012 // Habari // 9 Comments









KATIBU Mkuu wa Chama cha wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kuna baadhi ya viongozi ndani ya Zanzibar, hawafurahishwi na hali ya amani na utulivu iliyoko katika Visiwa hivyo.



Amesema kiongozi anayesajiisha wananchi kukataa umoja na mashirikiano ya wananchi, anakusudia kuirejesha Zanzibar katika matatizo na wananchi wake kuishi kwa uhasama na ugomvi kila siku.



Maalim Seif, alieleza hayo katika mkutano mkubwa wa hadhara wa CUF uliyofanyika jana jioni katika Jimbo la Bububu, nje ya mji wa Zanzibar. Maalim Seif, alikuwa nje ya Zanzibar, wakati wa kampeni za uchaguzi wa Jimbo hilo.



Akifafanua hotuba yake Maalim Seif, alisema kuna viongozi ambao wanawaambia wananchi wakatae mashirikiano ya chini na mashirikiano yabaki kwa viongozi wa juu, “vipi anawaambia watu kauli hiyo,”? alihoji Maalim Seif:



“Sikuwepo katika kampeni lakini nimeona kapitia facebook na kila kitu nakiona lakini niliporudi nikaletewa CD moja kampeni ya ufunguzi wa kampeni ya CCM na CUF na kuangalia nataka niseme,” alisema na kuongeza:



“Nataka nisema maneno yaliyosemwa pale katika ufunguzi wa kampeni ile ni kwamba ni dhahiri kwamba watu wale wawili hawaitakii mema Zanzibar ni dhahiri kabisaaa, vipi wewe kama kiongozi unasema mashirikiano yabaki huko juu,” alisema na kufafanua zaidi:



“Wananchi kataeni mashirikiano…kataeni chini mashirikiano mashauri yabaki huko juu tu vipi unawaambia watu kauli hiyo…kama yaliosemwa hivi eti wale pilau peke yao…kama yalivyosemwa hapa,” alisema Maalim Seif.



Maalim Seif, ambaye pia ni Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, alisema hali ya amani na utulivu iliyopo katika Visiwa hivyo ni kutokana na wananchi kuchoshwa na kauli za viongozi wasiyoitakia mema Zanzibar kwa kuwagombanisha.



Alisema Chama chake kinasimamia kwa busara na nguvu zote hali ya sasa ya amani na utulivu wa Zanzibar, na kufanya hivyo hawana maana kwamba viongozi wake wanahitaji madaraka bila kuwepo kwa amani miongoni mwa wananchi wa Zanzibar:



“CUF ikiamua hapakaliki hapa, wewe kiongozi unawaambia wananchi wakatae mashiriano na yule mwengine yeye anaturejesha katika mapinduzi kama wao peke yao ndio weneye milki ya Zanzibar, nasema wenye milki ya Zanzibar ni Wazanzibari wote,” alisisitiza Maalim Seif.



Maalim Seif alisema amesikia maneno ya wanachama wa Chama hicho, kupitia risala, utenzi na kauli za viongozi wa CUF, zilizotangulia kutolewa katika mkutano huo na kuahidi hatua zitachukuliwa:



“Nimesikia maneno yenu nimesikia risala, utenzi na maneno yote lakini nawahakikishia kwamba haya yaliyotendeka ni ushenzi uliofanyika, hayawezi kupita hivi hivi…hata huko Afrika Kusini hayakufanyika,” alisema na kuongeza:



“Leo mnakwenda kumshuti mtoto wa miaka 14 hana kosa lolote kisa nini, kaulizwa kwenu wapi…kasema kwetu Pemba…Dk Shein huu ndio uongozi unaoutaka? alihoji Maalim Seif.



Maalim Seif alisema katika uchaguzi mkuu wa 2010 askari walikuwa hao hao, lakini waliambiwa na uongozi uliyokuwepo hawataki fujo, wanataka nidhamu lakini leo askari wanafanya uhuni:



“Askari ndio hao hao, mbona 2010 ulikuwa na nidhamu kwa sababu uongozi uliokuwepo, uliwaambia hatutaki fujo tunataka nidhamu lakini leo askari wanafanya uhuni,” alisema na kuongeza:



“Kwanini 2010 yaliwezekana sasa hivi ishindikane? viongozi wa sasa wanataka kuturejesha nyuma na mimi nakwambieni hawa wanafanya hivyo kwa sababu wametishika na umoja wa Wazanzibari,” alisema na kusisitiza:



“Wazanzibari sasa hivi wameungana, sasa walipoona mambo ni magumu ndio wakatuma watu wao maana siku zote wanataka kutugawa,” alisema Maalim Seif.



Katibu Mkuu huyo wa CUF, alitoa mfano wa miti na shoka…adui wa miti ni shoka lakini bila shoka kuwa na mpini wa mti, adui huyo anashindwa nguvu kuweza kukata miti.



“Hii ni hadithi ya miti na shoka…naijua miti ilikaa ghafla wakaliona shoka linakuja wakapiga makelele shoka shoka shoka…mzee akawauliza ndugu yetu yumo? wakasema hayumo, wakaambiwa ondoeni wasiwasi,” alisema na kufafanua:



“Ghafla akaona shoka linakuja sasa lina mpini mzee akawauliza…ndugu yetu yumo, wakasema ndio yumo…wakasema mara hii hatuponi. Hakuja Katibu Mkuu wa CCM kuja kutugombanisha,” alisema na kuongeza zaidi:



“Wala hakuna mwengine Naibu Katibu Mkuu wa CCM hapa kuja kutungonisha lakini nataka niwaambie waziwazi…hapa tulipofika usiwe na matumaini kwamba tutarudi nyuma? au mtarudi nyuma,”? alihoji na kuendelea.



“Mnapambana na mkondo wa maji unataka kusalimika nenda na mkondo na kama huna kifua utapambana na mabadiliko ya Wazanzibari wanayodai na yule ambaye anajaribu kupingana na mkondo hufa maji…kwa hivyo hapa haturudi nyuma…Waheshimiwa kinachogombewa nini? Wazanzibari wanasema mfumo wa muungano tulionao hatuutaki,” alisema Maalim Seif.



Maalim Seif alisema wakati umefika kwa Wazanzibari kuendesha nchi yao wenyewe ikiwa na mamlaka ya ndani na nje na yeye ni miongoni mwa Wazanzibari wanaounga mkono hatua hiyo:



“Wazanzibari wanataka kuendesha nchi yao yenye mamlaka kamili…mimi binfasi ni muumini wa Muungano wa mkataba,” alisema Maalim Seif.



Alisema kuna baadhi ya watu wakiwemo wanachama wa Chama hicho wanasema kuwa Kiongozi huyo wa CUF ameleweshwa madaraka na kuwacha solemba wananchi wa Zanzibar:



“Kama kuna mtu anasema Maalim Seif ana king’ora sijui nini kama hamjui mimi sio mara ya kwanza kupanda king’ora mie tokea 85,…mie msimamo wangu unajulikana mimi ni muumini wa muungano wa mkataba,” alisema na kuongeza:



“Muungano wa mkataba utaturudishia haki zetu Wazanzibari na sasa hivi tuna Serikali, lakini leo Serikali yetu kila kitu lazima tukapige magoti Tanganyika,” alisema na kufafanua:



“Tunashangaa kuwa tunashuhudia sote kunatiwa saini baina ya World Bank na ujenzi wa barabara ya Zanzibar lakini Waziri wetu wa fedha kaa pembeni…tunataka kurejesha mamlaka kamili, tulikuwa na kila kitu chetu…tunataka turejee na hali hiyo,” alisema na kusisitiza.



“Tunataka Banki Kuu yetu ya Zanzbar na Tanganyika watakuwa na yao…halafu tukishapata Muungano wa mkataba Zanzibar huru, Rais wetu anatoka popote Duniani,” alisema Maalim Seif.



Kiongozi huyo mwenye mvuto kwa wananchi wa Zanzibar, alisema kuna nchi ndogo kuliko Zanzibar na viongozi wake wanahadhi mbele ya Ulimwengu, Jumuiya za Kimataifa na Taasisi nyingene, kwanini Rais wa Zanzibar hathaminiwi:



“Marais wote katika nchi zilizokwenda katika mkutano wa UNESCO walionekana hata katika nchi ndogo ndogo lakini sisi Rais wetu anatoka Zanzibar…mmh kama,” aliguna Maalim Seif.



Maalim Seif alisema kufuatia hali iliyojitokeza katika uchaguzi mdogo wa Bububu, imewaogopesha kutokana na Jeshi la Muungano kusimamia uchaguzi mdogo uliyochini ya Serikali ya Zanzibar:



“Uchaguzi wa BUBUBU limewaogopesha…leo inakuwaje Jeshi la Muungano wanasimamia uchaguzi…na cha ajabu hakuna kambi…Maalim anajibiwa ipoooooo anasema hata ikawepoooo….lakini wana haki gani kuingia katika kituo cha uchaguzi na silaha nzito nzito,” alihoji Maalim Seif.



Alisema aliwaeleza Wamarekani na Taasisi nyingine kuhusiana na mchakato wa marekebisho ya Katiba kwamba yanakwenda vizuri na hadi sasa asilimia 77 wameishauri Tume kuwepo kwa Muungano wa Mkataba:



“Inshallah kwa uwezo wa Mwenyenzi Mungu, Zanzibar itarudi katika mamlaka kamili…tutaisimamia na mote humo sikutafuna maneno nimewaambia, Wazanzibari wanachokitaka…nimewaambia wanataka kuungwa mkono na mataifa makubwa,” alisema na kueleza:



“Nimewaambia kuwa tayari maoni yanachukuliwa na tayari Mikoa miwili na zaidi ya asilimia 77 wanataka Muungano wa mkataba na Kusini chake-chake aslimia 75, wanataka Muungano wa Mkataba kwa hivyo nikawaambia wakubwa hawa haya ndio mawazo ya Wazanzibari,”:



“Wao hawataweka vizingiti kwa Wazanzibari katika kufikia malengo yao…walituuliza masuali magumu lakini nikawajibu wakatuuliza nyinyi mnataka mamlaka kamili mtaweza kujiendesha…nikacheka nikawaambia tunaweza nikawaambia visiwa vidogo vinaweza kujiendesha sisi kwa nini tushindweeeee wakasema sawa sawa,” alisema Maalim Seif.



Maalim Seif aliwahimiza wananchi wa Zanzibar, kuwa kitu kimoja katika kutoa maoni yao kwa Tume ya Katiba mpya, ili kusimamia madai ya nchi yao na waache wasiwasi kwamba Tume hiyo ni ya usanii na kiini macho.



“Wananchi kama mmekasirishwa na jimbo la BUBUBU lakini muwe makini kabisa Tume ya Katiba inakuja, mjitokeze mkatoe maoni yenu na msiogope kitu…ikisha itakwenda Pemba…ni haki yetu kuhakikisha hatuogopi hatutishwi,” alisema na kuongeza:



“Mimi nasema hayatachakachuliwa na bahati nzuri takwimu zote tunazo kila shehia watu wametoa maoni vipi kwa hivyo kuna sheria waliotoa, hivyo Tume haithubutu kutudanganya kwa sababu takwimu zipo..kwa hivyo nawaomba nyote mkatoe maoni,” alisema Maalim Seif..
 
Mtu huyu ana uchu wa madaraka sana. Kawauza wazanzibar na kuwadanganya kwa faida yake binafsi. Iko haja ya kumvua madaraka ndani ya CUF. Haweze akafanya kazi za CCM na CUF kwa wakati mmoja.
 
Huyu nyumba ndogo ya CCM hana jipya. Ameona muda wa kula unaisha anaanza kujijenga kwa wale aliowauza ili kupewa madaraka kipande. Ni mlafi na mchoyo hakuna mfano. Mapochopocho ya umakamu wa rais yalimfanya auze damu ya wananchi waliouawa na utawala wa Mkapa na Karume! Huyu anapaswa kuzomewa hata kupopolewa na kukumbushwa kuwa wananchi wana kumbukumbu kuliko yeye. Shame on you maalim Seif na uroho wako!
 
Maalim Seif tulishamsahau! Siku hizi anakula mema ya nchi na kutoa sauti za kitawala za Chama cha Mapinduzi!
 
chama gani kinasimamisha mgombea mmoja wa uchaguzi kwa miaka17? yaani hakuna mzanzibari mwingine zaidi ya hamad ana uwezo wa kugombania urais kupitia cuf? its amazing
 
Big Up Maalim, binafsi nimekusoma. nadhani watakutendea haki kujibu hoja zako kwa hoja sio kwa kubwabwaja. ila mie naomba ufafanuzi kidogo kuhusu huo muungano wa mkataba. hii imekaaje wadau??? naomba ufafanuzi tafadhali kwa anayeelewa hii kitu.
 
Tatizo lenu nyiyi linafahamika wabara, mukitajiwa wazanzibar kudai nchi yao nyiyi munafanya nongwa, nongwa za nini na muungano ukivunjika nyiyi mutakuwa na nchi yenu na sisi yetu.

Mulicho kipenda ni nini kutoka kwa wazanzibar?au mumependa singa muchanganye? Maana siku zote munasema wazanzibar wamejazana bara na bila ya muungano hawawezi kuichi watakufanjaa kwa vile chakula chote kinatoka kwenu ,sasa munawangagania nini?.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom