Maalim Seif anguruma Tanga

Maalim Seif anguruma Tanga

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Posts
858
Reaction score
130
[h=2]Saturday, December 29, 2012[/h][h=3][/h]

Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akionyesha kadi za ADC zilizorejeshwa na baadhi ya wafuasi wa chama hicho na kujiunga na CUF katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na chama hicho katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.(Picha na Salmin Said, OMKR)

Hassan Hamad, Tanga

Chama Cha Wananchi CUF kimesema kuwa amani ya kudumu haiwezi kupatikana katika nchi yoyote bila ya kuwepo haki na usawa katika jamii.

Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad ameeleza hayo wakati akiwahutubia wafuasi wa CUF na wakaazi wa jiji la Tanga katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Tangamano jijini Tanga.

Amesema miongoni mwa sera za msingi za chama hicho ni kuwaunganisha wananchi, na kwamba umoja hauwezi kupatikana kwa kuendeleza sera za kibaguzi na kutowatendea haki wananchi.



“Kila mtu ana haki sawa na mwengine kikatiba na kila mtu anastahiki kuheshimiwa haki zake, kwa hivyo nasema tena kuwa popote penye ubaguzi hapawezi kuwa na umoja”, alisisitiza Maalim Seif.

Katika Mkutano huo Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amewatanabahisha Wakuu wa Mikoa na Wilaya kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, na kuacha kushabikia masuala ya kisiasa.

“Kikatiba viongozi hawa si wanasiasa bali ni watumishi wa umma, lakini cha kushangaza bado wapo Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanajifanya wakereketwa wa vyama fulani na kuwabagua wananchi”, alieleza Katibu Mkuu huyo wa CUF.

Amewapongeza viongozi wa Mkoa wa Tanga kwa kuweka kando tofauti za kisiasa na kushirikiana na wananchi katika kusogeza mbele maendeleo ya Mkoa huo.

Mapema Mkuu wa Wilaya ya Tanga bibi Halima Dendegu ambaye alipanda jukwaani kuwasalimia wananchi waliohudhuria mkutano huo, amesema uongozi wa Mkoa huo unashirikiana vizuri na wananchi na wanaishi kwa kupendana na kuheshimiana.

Akizungumzia kuhusu uchumi, Katibu Mkuu wa CUF amesema chama hicho kina sera imara za kujenga uchumi wa Tanzania kwa lengo la kuwakomboa Watanzania kuondokana na hali ngumu ya maisha.

Amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi ambazo bado hazijatumika ipasavyo kuweza kuwanufaisha watanzania, na hivyo kuendelea kubakia kuwa nchi maskini.

“Ardhi ya Tanzania ina rutba nzuri ambayo takriban inakubali kila aina ya mazao, tuna bahari ambayo nayo ina rasilimali kadhaa wa kadhaa, madini ya kila aina, Tanga kuna bandari na kadhalika, lakini wapi bado rasilimali hizi zinatumika kuwanufaisha watu wachache na makampuni ya kigeni na sisi Watanzani wengi tulio maskini tunabakia kushuhudia mashimo tu”, alifahamisha Katibu Mkuu wa CUF.

Amesema iwapo chama hicho kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi mwaka 2015, kitahakikisha kuwa wananchi wananufaika moja kwa moja na rasilimali za nchi, na kwamba robo ya mapato yatokanayo na rasilimali hizo yatatumika kulipa madeni ya nje ambayo yameripotiwa kufikia shilingi trilioni ishirini (20).

Akizungumzia kuhusu maendeleo ya chama hicho, Maalim Seif amesema chama bado kiko imara na wala hakitoyumba kutokana na kujengwa na misingi ya imara.

“Watakaojaribu kukibomoa watashindwa, CUF hakiwezi kusambaratika hata siku moja kwa kuwa kimejengwa kwa misingi imara na viongozi wake wako imara na madhubuti kabisa”. Alifahamisha.

Katika risala yao wafuasi wa CUF Mkoa wa Tanga wameeleza kuwa changamoto kubwa inayowakabili kwa sasa ni upungufu wa dawa pamoja na kuharibika mara kwa mara kwa X-ray katika hospitali ya rufaa ya Bombo Mkoani humo.

Nae Naibu Mkurugenzi wa haki za binadamu na mawasiliano ya umma wa CUF bw. Abdul Kambaya amesema rasilimali zilizopo Tanzania zinatosha kuwakomboa wananchi na umaskini, lakini mfumo wa uongozi uliopo bado haujazingatia maslahi ya umma na unalenga kuwanufaisha watu wachache.

“Bandari ya Tanga haifanyi kazi vizuri, reli ya Tanga imekufa, mashamba ya mkonge yamekufa, tujiulize watu wa Tanga kuna nini?” alihoji Kambaya na kudai kuwa limetokana na mfumo uliopo wa uongozi.

Katika Mkutano huo Chama hicho kimepoa kadi ishirini (20) za wafuasi wa Chama Cha ADC walioamua kujiengua katika chama hicho na kujiunga na CUF.


Imewekwa na MAPARA at 9:50 AM
 
huyu kuwepo Tanga na ukilinganisha sera zake za 'kujitenga' ni wazi kuwa ana ndoto za kurudisha mipaka ya mjerumani (?) ambapo km 10 upcountry ilikuwa ya sultan. hiyo Mafia kwa asilimia kubwa 'wameshaitia' mfukoni
 
Mkutano wa CUF anahutubia mkuu wa wilaya ambaye ni mjumbe wa Kamati ya siasa ya CCM.Ndoa tamu jamani.
 
Akimaliza awahi mtwara kabla ya dume la mbegu halijarudi kule.
 
huyu kuwepo Tanga na ukilinganisha sera zake za 'kujitenga' ni wazi kuwa ana ndoto za kurudisha mipaka ya mjerumani (?) ambapo km 10 upcountry ilikuwa ya sultan. hiyo Mafia kwa asilimia kubwa 'wameshaitia' mfukoni

hana mpya maalim. Anawapenda sana watu wa Tanga eti! Sasa huo msimamo wa kuwavunjia muungano wao na wapenzi na ndugu zao wa kaskazini Pemba unatokea wapi tena? Whither!! Maalim.
 
hana mpya maalim. Anawapenda sana watu wa Tanga eti! Sasa huo msimamo wa kuwavunjia muungano wao na wapenzi na ndugu zao wa kaskazini Pemba unatokea wapi tena? Whither!! Maalim.
Hana maana huyu! Eti anataka muungano wa MKATABA?!
 
Hakuna dhambi mbaya kama unafiki,eti umoja na mshikamano! Si huyu anayetaka umoja wa mataifa umsaidie kuvunja muungano? Maalim bwana' leo kawashika Tanga,sijui kesho atafanya unafiki wapi! Hiyo ni SIHASA.
 
Hana maana huyu! Eti anataka muungano wa MKATABA?!

mwambieni Maalim. Nchi moja -Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Taifa moja. Serikali moja. Bunge moja. Rais mmoja .Makamo wa rais mmoja. Waziri mkuu mmoja. Waziri kiongozi mmoja-hiyo ndio line up ya JMT. Usitaharuk Maalim kwa kuheshimu SUK ipo nafasi ya Naibu Waziri Kiongozi mwandamizi ambaye kin'gora (bubu) kinaishia Chumbe. Hongera Maalim kwa kuwajali watu wa Tanga. Ni kweli hawastahili kuvunjiwa muungano wao.
 
[h=3][/h]




Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bibi Chiku Galawa akimkaribisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad katika Mkoa huo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga.



Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimia na vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi wa Mkoa wa Tanga, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimia na wananchi mbali mbali waliojitokeza kumpokea wakati walipowasili katika uwanja wa ndege wa Tanga kwa ziara ya siku mbili. (Picha na Salmin Said, OMKR)




TANGA
28/12/2012.


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema wananchi wanahitaji kuelimishwa zaidi juu ya uhifadhi wa mazingira ili waweze kuyalinda na kuepuka kuyachafua.


Amesema uchafuzi wa mazingira mara nyingi umekuwa ukisababishwa na wananchi wenyewe, jambo ambalo linapaswa kupigwa vita kwa wananchi kupatiwa elimu ya mazingira ili kuepusha uharibifu huo.

Maalim Seif ameeleza hayo wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Tanga bibi Chiku Galawa, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga kwa ziara ya siku mbili.


Amesema iwapo wananchi wataelimishwa ipasavyo wataweza kujiepusha na uharibifu wa mazingira, ikiwa ni pamoja na kukata miti kiholela bila ya kuzingatia athari za kimazingira.


Nae Mkuu wa Mkoa wa Tanga bibi Chiku Galawa amesema uharibifu wa mazingira ni moja kati ya changamoto kubwa zinazoukabili Mkoa huo, jambo ambalo linarejesha nyuma maendeleo ya kiuchumi katika Mkoa huo.


Amesema Serikali ya Mkoa huo inatafuta njia mbadala ya kutumia nishati nyengine ili kupunguza matumizi ya kuni ambayo yanachangia ukataji wa miti kiholela.


“Iwapo serikali itazuia matumizi ya makaa na kuni, serikali na wananchi watapata nafasi ya kufikiria nishati mbadala ya kutumia kwa ajili ya kupikia, lakini tukiendelea kutumia kuni mawazo yetu yatabakia hapo hapo tu na tutaendelea kutumia kuni kila siku”, alitanabahisha bibi Chiku.

Amesema ukataji wa miti kiholela katika Mkoa huo umekuwa ukichangia kuwepo kwa athari za mabadiliko ya tabianchi yanayopelekea kuweko kwa upungufu wa mvua pamoja na kuongezeka kwa hali ya joto.


Hata hivyo bibi Chiku amesema Mkoa huo umepiga hatua kimaendeleo, ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa miundombinu ya barabara.


Akiwa Mkoani Tanga, Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF anatarajiwa kuhutubia mikutano mitatu ya hadhara katika viwanja vya Tangamano, Kwadiboma Sokoni na Handeni.


Hassan Hamad (OMKR)

 
mwambieni Maalim. Nchi moja -Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Taifa moja. Serikali moja. Bunge moja. Rais mmoja .Makamo wa rais mmoja. Waziri mkuu mmoja. Waziri kiongozi mmoja-hiyo ndio line up ya JMT. Usitaharuk Maalim kwa kuheshimu SUK ipo nafasi ya Naibu Waziri Kiongozi mwandamizi ambaye kin'gora (bubu) kinaishia Chumbe. Hongera Maalim kwa kuwajali watu wa Tanga. Ni kweli hawastahili kuvunjiwa muungano wao.

Mh! unapaswa kupitia upya katiba ya Zanzibar! Hapo kwenye nyekundu hawapo kabisa sijui unatumia katiba gani?!
 

Sasa ni Faida kuwa na Government of National Unity; Maalim Seif halipii Gharama za USAFIRI kuna NDEGE ya SERIKALI Malazi yeye na UJUMBE wake pia ni BURE; na TANGA CUF inapendeka - hakupata Mashabiki wa KUMZOMEA kama WAKATI ULE Rais Kikwete alipokwenda TANGA...

Kwahiyo CUF pia inakula pesa za WALIPA kodi bila shida YOYOTE na PESA zao za RUZUKU ziko wapi??? Hawafanyi MIKUTANO isipokuwa Maalim SEIF
 
Mh! unapaswa kupitia upya katiba ya Zanzibar! Hapo kwenye nyekundu hawapo kabisa sijui unatumia katiba gani?![/QUOTEba2]

vipi anko tumia nafasi yako kutoa maoni mchakato katiba mpya. Tutumie nafasi kutafuta suluhu ya mazonge yetu. Kwa mfano kwa nini maraisi wawili.makamo raisi wangapi? Titles get in the way. One title one person. Muhimu ni formular ya kushare madaraka. Si unaona hapo title ya waziri kiongozi mwandamizi ni moja tu. Domain ya Maalim mpaka wadau waamue vyenginevyo.
 
Back
Top Bottom