Maalim Seif anena

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
20,479
24,350
12734277_1120813921262076_4625484709494804269_n.jpg


SEIF SHARRIF HAMAD AMEHOJI
SABABU ZA CHAMA TAWALA CHA
CCM KUHOFIA CUF KUONGOZA
ZANZIBAR.
Wakati saa 864 zimesalia kabla ya
kurudiwa kwa uchaguzi wa
Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Maalim Seif Sharrif
Hamad amehoji sababu za chama
tawala cha CCM kuhofia CUF
kuongoza visiwa hivyo.
Maalim Seif ambaye aligombea
urais wa Zanzibar katika uchaguzi
wa Oktoba 25 mwaka jana ambao
matokeo yake yalifutwa, pia
amesema endapo CCM itasitisha
uchaguzi uliopangwa kufanyika
siku 36 zijazo, CUF itakuwa tayari
kufanya mazungumzo, lakini siyo
wakati huu ambao maandalizi ya
kupiga kura yanaendelea.
Akizungumza na waandishi wa
habari jana, katibu huyo mkuu wa
CUF aliitoa hofu CCM kuwa chama
chake hakina ajenda ya kulipiza
kisasi.
Matokeo ya uchaguzi wa Rais wa
Zanzibar, wawakilishi na madiwani
yalifutwa na Mwenyekiti wa Tume
ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salum
Jecha siku ambayo chombo hicho
kilitakiwa kumtangaza mshindi, na
mwezi uliopita alitangaza Machi
20 kuwa siku ya uchaguzi wa
marudio visiwani humo.
Wakati CUF ikipinga vikali kufutwa
matokeo na kutangaza tarehe
mpya, Serikali imesema kuna
nafasi ya kufanya mazungumzo
kabla ya uchaguzi wa marudio
kwa kuwa kuna muda ni mrefu wa
kufanya hivyo.
Jecha alitangaza uamuzi huo
wakati tayari matokeo ya urais ya
majimbo 31 yalishatangazwa, na
ya majimbo tisa yaliyosalia
yalishahakikiwa, huku washindi wa
viti vya uwakilishi na udiwani
wakiwa wametangazwa na kupewa
vyeti vya ushindi.
“Sijui kwa nini CCM wanaogopa
sisi tukiongoza?” alihoji Maalim
Seif kwenye mkutano huo na
waandishi akiwa pamoja na
aliyekuwa mgombea urais wa
Jamhuri ya Muungano kwa tiketi
ya Chadema, Edward Lowassa.
“Wana wasiwasi gani, kwamba
CUF ikiongoza kutatokea nini? Sisi
hatuna ajenda ya kulipiza kisasi,”
alisema.
Katika mkutano huo, Maalim Seif
mbaye pia ni katibu mkuu wa
chama hicho alisema kama CCM
ina wasiwasi na idadi ya wajumbe
wa Baraza la Wawakilishi kwenye
Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK),
haina budi kuondoa shaka kwa
kuwa idadi kwa pande zote
inakaribiana.
“Hawa wanahisi hawatapata
uwakilishi mkubwa, lakini mbona
miaka yote tunakuwa na idadi
isiyopishana ya wawakilishi?”
alihoji.
Hali ilivyo Zanzibar
Katika mkutano huo, Maalim Seif
alisema kumekuwapo vitendo vya
wananchi kupigwa na vikundi vya
watu wasiojulikana.
Alidai wafanyakazi wa Serikali na
taasisi zake wameamrishwa
kupeleka vitambulisho vyao vya
kazi na vya kura serikalini ili
vikahakikiwe.
“Hii si mara ya kwanza
wafanyakazi wa Serikali kutakiwa
kupeleka vitambulisho, sisi
tunajua kuwa wanataka wawatishe
kuwa watajua nani kapiga kura na
nani hajapiga,” alisema na
kusisitiza:“Hii ni kama kitisho cha
kuwalazimisha wakapige kura,
zaidi hasa hizo ni dhuluma
ambazo wananchi wanafanyiwa.”
Uwapo wa mazombi
Kadhalika Maalim Seif
alizungumzia uwapo wa watu
wanaovaa soksi usoni na
kuwashambulia raia, akisema
Serikali haijachukua hatua stahiki
kudhibiti hali hiyo.
Alisema watu hao ambao
wamepachikwa jina la mazombi,
wamevamia maeneo kadhaa kama
Baraza la CUF, Jang’ombe na
yaleambayo yana wafuasi wa
chama hicho kikuu cha upinzani
visiwani humo.
“Wanawapiga watu, wanawajeruhi
na wanaiba mali, lakini
inashangaza sana mambo haya na
si Serikali wala polisi iliyochukua
hatua,” alisema.
Maalim Seif alisema
amezungumza na Rais wa
Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein
kuhusu matukio hayo ya uharamia
wanaofanyiwa wananchi, lakini
hakuna hatua zinazochukuliwa.
Alisema CCM wanatafuta sababu
ili machafuko zaidi yatokee
visiwani humo wapate kisingizio.
Aliwataka wafuasi wa CUF
kuvumilia hali hiyo ili nchi isiingie
kwenye machafuko kama
yaliyotokea mwaka 2000, wakati
watu zaidi ya 20 waliuawa na
wengine kukimbilia Shimoni,
Mombasa nchini Kenya ambako
waliishi kama wakimbizi.
CHanzo : Mwananchi
 
Paka wa nyumbani hawindwi...CCM walimlea Sefu wanamjua vyema wanacheza nae wanavyotaka wao..ndio maana yeye tu anaongea ccm wapo kimya wanasubiri kuunda serikali..
 
Back
Top Bottom