Maalim Seif Anaaminika?

Seif ni mwanasiasa kama walivyo wanasiasa wengi tu...hawana maadui wala marafiki wa kudumu..maamuzi yao hutegemea na maslahi yao kisiasa.

Ukirudi nyuma kidogo mpaka 1984..utakuta kuwa Seif alichangia sana kuangushwa kwa aliyekuwa raisi wa Zanzibar kipindi hicho..Mzee Aboud Jumbe Mwinyi....Seif akiwa waziri kiongozi alitegemea kuwa madaraka yale yangekwenda kwake...iliposhidikana naye akaasi na kushughulikiwa na CCM mpaka alipokuja ibuka tena na KAMAHURU katika vuguvugu la vyama vingi mwishoni mwa 1980s na mwanzoni mwa 1990s.

Kwa Zanzibar kwa mfano..waunguja hawamuoni Seif kama ni mtu wa-kuaminika hasa wakikumbuka mchango wake wa fitina zake za kisiasa dhidi ya mzee Jumbe lakini kwa Wapemba wanamuona kama ni shujaa kwa vile amesimama nao muda wote wakiwa marginalised na SMZ.

kwa kifupi Seif ni very intelligent katika kucheza mchezo wa siasa.
 
Back
Top Bottom