jyfranca
JF-Expert Member
- Oct 3, 2010
- 297
- 8
Upinzani si kupinga kila jambo - Seif
Thursday, 18 November 2010 19:53 newsroom
Na Esther Mvungi,Dodoma
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Seif Sharif Hamad, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, amesema haina maana kwa chama cha siasa kupinga kila jambo. Amesema CUF kwa upande wa Tanzania Bara kinafanya kazi ya upinzani kwa ustaarabu na kuongeza: ìTutapinga kwa hoja na si kwa malumbano. Seif alisema hayo jana baada ya kuapishwa kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, katika sherehe zilizofanyika Ikulu Ndogo ya Chamwino. Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hoja inayotolewa na baadhi ya wananchi na vyama vya siasa kuwa, CUF si chama cha upinzani kwa kuwa kimo ndani ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Haina maana kama Zanzibar kuna maeleweno na upande wa pili wa Muungano iwe tofauti, tutafanya kazi zetu kistaarabu,î alisema Seif.
Alisema lengo la wote ni kuleta amani, hivyo CUF inataka yaliyotokea Zanzibar yahamie Bara.Seif alisema ni kweli kwa upande wa Zanzibar CUF si chama cha upinzani kwa kuwa kimo ndani ya serikali. CHADEMA imevitenga vyama vingine vya upinzani vya CUF, NCCR-Mageuzi na TLP katika kuunda kambi ya upinzani.Utengano kati ya vyama hivyo umekuwa ukijionyesha wazi bungeni, ambapo katika uchaguzi wa wajumbe wa Bunge la SADC-PF uliofanyika Jumanne wiki hii, wabunge wa CHADEMA walimdhihaki mgombea wa CUF.
Baada ya Injinia Mohammed Habib Mnyaa wa CUF kutangazwa mshindi katika kundi la vyama vya upinzani, wabunge wa CHADEMA walipiga kofi wakisema CCM, CCM.