Maalim Seif ampongeza Mbowe

Maalim Seif ampongeza Mbowe

Mimi leo nilikuwepo kibanda maiti na nimemsikia maalim kwa masikio yangu, yote anayoyasema mleta uzi ni ya kweli.

Maalim amesema kwamba Mbowe anastahiki sifa na anafagam wajibu wake kama KUB na kwa mujib wa sheria Ndugai hakupaswa kumwambia akae chini na huo ndio utaratibu wa mabunge ya commonwealth countries kwamba KUB anapaswa kusikilizwa anapikuwa na hoja, pia kamkosoa Ndugai kutumia uimla na udikteta wa kutofata sheria za Bunge na kwamba hata mswada ulivyopitishwa sio halali kwa mujibu wa sheria za bunge kukitokea tokeo kama lile spika anapaswa kuhairisha kikao cha bunge.
 
Lizabon
Kampongeza leo kibandamaiti katika mkutano wa cuf uliofanyika jioni ya leo, pia kamuonya CHIKAWE kwa kujifanya mungu mtu, pia kasema pinda kamuandikia barua makamo wa pili wa zanzibar lakini mapendekezo yaliyotolewa na waziri wa sheria wa zanzibar na mwanasheria mkuu yalipuuzwa, kamati ya sheria ya bunge ikaongeza mambo mapya. Maalim seif kasema cuf na wazanzibar HAWATOITAMBUA sheria iliyopitishwa. Pia JUSSA kamshambulia KINGUNGE na kusema kuwa uzee ndio unaomfanya kingunge aongee asichokijua. LIZABON, UNALO JENGINE?

Lizaboni
Iwapo haya niliyoyangea kesho hayatothibitishwa na vyombo vengine vya habari, basi MODS NAOMBA MUNIPIGE BAN ili tujue nani muongo na huyo lizaboni.
 
Last edited by a moderator:
Kuhusu mswada amesema Pinda na ccm wenziwe wamempoza makamo wa pili, barua alioituma pinda ilimtaka makamo wa pili kutoa maoni ya SMZ juu ya mambo sita na wakafanya hivyo ila hayakufatwa mapendekezo yao badala yake wamefanya marekebisho ya vifungu nane vipya ambavyo hawakuwashauri SMZ wala asasi za kiraia znz.

Badala yake makamo wa pili kavikwa kilemba cha ukoka kaitwa bungeni mswada mpya hajapewa kadhani ni ule wa mwanzo kumbe sio yeye akathibitisha kuwa znz imeshirikishwa kumbe sivyo.
 
Mwisho kamtanabahisha rais kikwete asije akausain mswada na ikiwa atasign basi yeye kama katibu mkuu wa cuf atawazuia wajumbe wa bunge maalum kutoka cuf wasishiriki ili ccm ipitishe hiyo katiba yao.

Kwakweli ccm wanataka kuuteka mchakato mzima la kusikitisha moja katika vipengele vilivyomo kwenye mswada ni kwamba hata tume hii ya marekebisho ya katiba ikikamilisha kutoa rasimu ya pili ya katiba ivunjwe iwe haipo tena kisheria kwa maana eti itakuwa imekamilisha kazi zake hata kabla ya rasimu hiyo haijajadiliwa kwenye bunge maalum.


Kipengele chengine ni cha kutumia simple majority ikiwa kutakua na kipengele kitakacho kwama kupita kwa two third, hii wameiweka wakijua simple majority watakua nayo ccm.

Yapo mengi ila kwakweli ccm nia zao hazipo kuwatumikia wananchi zaid ya maslhi yao. Kubwa ni kutafuta yanayowaangamiza wananchi.

Nawasilisha.
 
Na mimi nimeshangaa seifu kahutubia wapi khaa cdm uongo mtaacha lini nyie au ndio mnataka aropoke subirini kile ni kichwa nakiamini kitawajibu tuu huu upuuzi wenu
wacha uongo wewe. mkutano gani amehutubia maalim seif kumsifu mbowe? haitakuja kutokea hata siku moja
 
Hawa chadema hawabebeki maalim, achana nao na siasa zao mbumbumu wamekuja kuungana na CUF kutaka umaarufu Visiwani, wasahau ammiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii., wamekuja na kanzu watarudi na vilemba.,
 
siasa ni mchezo mchafu na utayaona mengi zaidi ya hayo kwenye huu mchezo unaoitwa siasa,wote hao ni walewale tu,sidanganyiki ng'o.
Nalog off
 
tuishukuru sana CCM kwa kuwaunganisha wapinzani. big up CCM! keep it up! yaani CCM sasa ndio wanafanya kazi wanayotakiwa kuifanya, kuleta muungano wa vyama, taasisi za dini na wananchi wengi tu kwa ujumla. huo ndio mshikamano! ni lini CCM walifanya jema namna hii kwa nchi yetu? sikumbuki...

Waliokuwa na akili zao kubwa ndani ya CCM walikianzisha kwa lengo la kuleta mabadiliko (mapinduzi) makubwa kwa kutumia jembe na nyundo! Wenye akili ndogo waliopo mle ndani kwa sasa wanatumia zana zile zile tena bila kujua kuharakisha na kuhalalisha mapinduzi dhidi ya CCM!!!

"Bora upofu wa macho kuliko wa akili" (Solar, 2012)
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, katibu mkuu wa CUF Maalim seif sharifu hamad amemsifu na kumpongeza kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni freeman mbowe kutokana kuonesha ujasiri wa hali ya juu kupinga kile alichokiita udhalimu wa naibu spika. Amesema hoja iliyotolewa na wabunge wa upinzani ya kutaka taasisi za zanzibar zishirikishwe ilikuwa na mashiko. Amemtuhumu ndugai kwa kutumia ubabe wa kumtoa mbowe wakati anajuwa kiongozi huyo wa kambi ya upinzani bungeni ana haki sawa na waziri mkuu. Mkutano unaendelea, maelfu ya watu wamehudhuria.

Ni mtu gani aliye hai aisyekubali kwamba Mbowe ni jembe?
Watakubali tu kwamba Chadema ni chama cha ukombozi!
Watakubali tu kwamba vuguvugu la mabadiliko M4C ni ya kudumu na ndiyo njia pekee ya kumkomboa Mtz,
Watakubali tu Chadema hakikurupuki katika hoja zake, chama chenye viongozi makini wanaosimamia kile wanachokiamini angali msimamo wa Kamanda Mbowe kwa askari waliolipua mabomu soweto.... si mmeonaaa? haponi mtu hapa
Watakubali tu kwamba Chadema kimejipanga na mbinu zote za maccm zinazidi kukiimarisha chama,
Watakubali tu kwamba Chadema ni chama cha Vijana waliona shahuku ya mabadiliko hata kama yatakuwa hasi,
watakubali tu kwamba Chadema kimekuja kuwashika CCM, kuwakumbusha muda wa kudangnya wananchi umekwisha, sera za uongo hazina mashiko tena, issue ni kutoa hoja si kupuliza vuvuzela kama wanavyofanya majukwaani akinia .....
Watakubali tu kwamba chadema kimesimama kitaifa na kimataifa, si unaona yaliyomkuta yule balozi wa kichinachina kule shy?
Watakubali tu kwamba chadema ......jazia mwenyewe
 
Tushaanza mazoezi ya viungo !!!!!!!!!
:msela::msela::msela::msela::msela:
 
Back
Top Bottom