mpemba mbishi
JF-Expert Member
- Nov 27, 2011
- 1,132
- 185
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, katibu mkuu wa CUF Maalim seif sharifu hamad amemsifu na kumpongeza kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni freeman mbowe kutokana kuonesha ujasiri wa hali ya juu kupinga kile alichokiita udhalimu wa naibu spika. Amesema hoja iliyotolewa na wabunge wa upinzani ya kutaka taasisi za zanzibar zishirikishwe ilikuwa na mashiko. Amemtuhumu ndugai kwa kutumia ubabe wa kumtoa mbowe wakati anajuwa kiongozi huyo wa kambi ya upinzani bungeni ana haki sawa na waziri mkuu. Mkutano unaendelea, maelfu ya watu wamehudhuria.