Maalim Seif ampongeza Mbowe

Maalim Seif ampongeza Mbowe

wewe mama, kaa ukijua kuwa haitakuja kutokea Maalim kumpongeza Mbowe. sababu zinaeleweka. mnaanzisha vithread ambavyo havina kichwa wala miguu

Wewe nenda kwenye kile kikao chenu cha usambazaji wa sembe hapakuhusu huku.
 
seif ni boya kama alivyo mbowe.lakini nawasikitikia sana hawajui wanalofanya kwa kutaka kuwaangamiza watanganyika

Tambua siku zote boya ndio linalotumika kuokaa watu wanapozama maji. Watanzania wameshazama seif lipumba mbowe mbatia ndio maboya yakuwaokoa watanzania wasife. Hongera kwa kulitambua hlo.
 
wacha uongo wewe. mkutano gani amehutubia maalim seif kumsifu mbowe? haitakuja kutokea hata siku moja

Lizabon
Kampongeza leo kibandamaiti katika mkutano wa cuf uliofanyika jioni ya leo, pia kamuonya CHIKAWE kwa kujifanya mungu mtu, pia kasema pinda kamuandikia barua makamo wa pili wa zanzibar lakini mapendekezo yaliyotolewa na waziri wa sheria wa zanzibar na mwanasheria mkuu yalipuuzwa, kamati ya sheria ya bunge ikaongeza mambo mapya. Maalim seif kasema cuf na wazanzibar HAWATOITAMBUA sheria iliyopitishwa. Pia JUSSA kamshambulia KINGUNGE na kusema kuwa uzee ndio unaomfanya kingunge aongee asichokijua. LIZABON, UNALO JENGINE?
 
Last edited by a moderator:
CCM iko kwenye mtanziko mkubwa kuliko wakati mwingine wowote wa uwepo wake na kwa yakini hakitavuka huu mtihani salama. Ilikuwa ajenda ya wengine wakaona ni mtaji kwao kwamba itawapandisha chati pengine ili kurudisha "hadhi" yake kumbe tego linawapeleka kuzimu hivyo.

Sio ajabu makada wenyewe kwa wenyewe wameanza kurukana vimanga kwamba haikuwa ilani yao hivyo waachane nayo kana kwamba Katiba ni mali yao! Kazi kwenu CCM kumeza au kutema bali mapenzi ya Mungu yatatimizwa hata na mawe; naam ikimpendeza Mola hata siafu, sisimizi, na mchwa watawaandikia waTanzania Katiba!

Kwani nyinyi CCM mmetukuka kuzidi falme na tawala za enzi na enzi ambazo leo zimebaki historia? Uko wapi Babeli? Iko wapi Rumi? Uko wapi Uru wa Wakaldayo? Yuko wapi Firauni enyi majuha? Iko wapi Ottoman Empire enyi wajinga? Mwamzidi Nebukadreza ninyi? Suleman, yule mwenye hikima na maonyo, kaja na kupita seuze mafisadi? Wamekuja manabii watukufu, wenye udhu, walionena na Mungu kinywa kwa kinywa, uso kwa uso - tangu Adam hadi kipenzi chetu Mtume Mtukufu (S.A.W) sembuse wauza sembe! Heri asikiaye maonyo haya!
 
Ajenda ya katiba mpya tanzania ni ya kikwete na wapinzania na sio wanaccm! Hongera maalim seif kwa kutambua mchango wa mbowe na Chadema kiujumla!
 
Nampongeza Maalim Seif kwa kutambua kuwa njia pekee ya kuwaondoa CCM madarakani ni kwa kuungana , kwani nani hajui kwamba karibu mara zote ulipofanyika uchaguzi mkuu visiwani CUF walishinda ikafanyika mizengwe ya kuwanyang'anya ushindi walioupata kihalali kwa visingizio mbalimbali. Sasa kama kweli wapinzani wanataka kushinda uchaguzi mkuu ujao hakuna njia ya mkato zaidi ya kuunganisha nguvu zao. Tunajua CCM watakashifu na kukejeri muungano huo kwa sababu wanajua dhahiri kwamba huo ndiyo mwisho wao. Nawasihi viongozi wa vyama vya upinzani waache tofauti zao zinazochochewa na CCM ambazo kwa hakika hazina tija, waache kufikiria maslahi binafsi wawaangalie Watanzania ambao wako katika taabu kwa takribani miaka 50 sasa.
 
wewe mama, kaa ukijua kuwa haitakuja kutokea Maalim kumpongeza Mbowe. sababu zinaeleweka. mnaanzisha vithread ambavyo havina kichwa wala miguu

hahahahaha umeshikwa pabaya na maalim seif anazidi kuwaumbua.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, katibu mkuu wa CUF Maalim seif sharifu hamad amemsifu na kumpongeza kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni freeman mbowe kutokana kuonesha ujasiri wa hali ya juu kupinga kile alichokiita udhalimu wa naibu spika. Amesema hoja iliyotolewa na wabunge wa upinzani ya kutaka taasisi za zanzibar zishirikishwe ilikuwa na mashiko. Amemtuhumu ndugai kwa kutumia ubabe wa kumtoa mbowe wakati anajuwa kiongozi huyo wa kambi ya upinzani bungeni ana haki sawa na waziri mkuu. Mkutano unaendelea, maelfu ya watu wamehudhuria.

Hata siku moja KUB hawezi kuwa na hadhi sawa na PM. Huku nikujidanganya kwa akili chache na kujipa hadhi usiyo nayo. Mbowe yeye ni kiongozi wa upinzani, na hata baraza lake la mawaziri linaitwa baraza kivuli. Na maana ya kivuli ni kitu kisicho halisi (kwa maana nyingine Feki). Kwa hiyo yeye ni kiongozi feki wa baraza la mawaziri kivuli.
 
sana mkuu. ila kuwa makini na kila unachokisikia. wengine wapo humu kutunga uongo kama uzi huu unavyoonekana

Shule za kata zina faida na madhara,nukta nyingi kama meseji za house girl
 
Hata siku moja KUB hawezi kuwa na hadhi sawa na PM. Huku nikujidanganya kwa akili chache na kujipa hadhi usiyo nayo. Mbowe yeye ni kiongozi wa upinzani, na hata baraza lake la mawaziri linaitwa baraza kivuli. Na maana ya kivuli ni kitu kisicho halisi (kwa maana nyingine Feki). Kwa hiyo yeye ni kiongozi feki wa baraza la mawaziri kivuli.

Povu la nini? Ukiwashwa tulia ukunwe,basi
 
Maalim Leo alikuwa na mkutano kibanda maiti ni amemsifu mbowe, huyu ni mwanasiasa pekee tuliyebakia naye baada ya kufa baba wa taifa
 
acha uongo wewe. kwanza maalim hayuko unguja leo. yupo Pemba. ona mnavyoumbuka

upumbavu mtupu munashusha hadhi ya jamvi tunawakosa watu wenye michango ya kuelimisha jamii sababu ya nyinyi makorokochwa mumewekwa na mwigulu na Nape
 
Hata siku moja KUB hawezi kuwa na hadhi sawa na PM. Huku nikujidanganya kwa akili chache na kujipa hadhi usiyo nayo. Mbowe yeye ni kiongozi wa upinzani, na hata baraza lake la mawaziri linaitwa baraza kivuli. Na maana ya kivuli ni kitu kisicho halisi (kwa maana nyingine Feki). Kwa hiyo yeye ni kiongozi feki wa baraza la mawaziri kivuli.

Narrow minded
 
Back
Top Bottom