Kakke
JF-Expert Member
- Dec 4, 2010
- 1,883
- 1,482
Msaidizi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kisiasa (Assistant Secretary-General for Political Affairs), Tayé-Brook Zerihoun
Friday, June 17, 2016
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Maalim Seif Sharif Hamad akiwa pamoja na Msaidizi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kisiasa (Assistant Secretary-General for Political Affairs), Tayé-Brook Zerihoun mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyochukua muda wa saa moja katika makao makuu ya Umoja huo, mjini New York.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim akisalimiana na Tayé-Brook Zerihoun
Bw. Tayé-Brook Zerihoun aliambatana na wasaidizi wake wanne katika mazungumzo hayo yaliyokuwa na mafahamiano makubwa ambapo alisema wanathamini sana kitendo cha Maalim Seif na ujumbe wake kufika mwenyewe Umoja wa Mataifa na kuwapa nafasi ya kuwajuza yanayoendelea Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim akiwa na Tayé-Brook Zerihoun, ambae ni Msaidizi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kisiasa (Assistant Secretary-General for Political Affairs)
Maalim Seif Sharif Hamad akiwa kwenye alama ya bastola iliyofungwa kwenye mdomo wa kutokea risasi ambayo imewekwa mbele ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mjini New York kuashiria kukataa matumizi ya nguvu na umwagaji wa damu katika kukabiliana na migogoro duniani.
Alama hiyo ilitolewa kwa Umoja wa Mataifa na nchi ya Luxembourg mwaka 1988.
Maalim Seif siku zote amesimamia njia ya mazumgumzo na amani katika kutatua migogoro ya kisiasa.
Picha hii ni ukumbusho wa jitihada zake na msimamo wake usiyoyumba katika kukataa matumizi ya nguvu au fujo na kusimamia amani na njia ya mazungumzo.