Maalim Seif alazwa hospitalini, Hali yake yabadilika baada ya kufika uwanja wa ndege Dar

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Siku tatu baada ya kutoka India alikokwenda kwa ajili ya kupata matibabu, Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad jana alilazwa katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassoro Mazrui amesema kuwa chanzo cha Maalim Seif kulazwa katika hospitali hiyo jana asubuhi ni uchovu wa safari yake ya India ambayo alienda kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa mgongo.

Mazrui alikanusha taarifa zilizokuwa zinaenezwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kiongozi huyo wa CUF alilazwa kutokana na matatizo ya moyo. Alisema kuwa hakuna kumbukumbu yoyote ya ripoti ya daktari inayoonesha kuwa Maalim Seif ana tatizo la moyo.

Naibu Katibu Mkuu huyo wa CUF alisema kuwa kiongozi huyo anaendelea vizuri kiafya na kwamba hayuko katika hali mahututi kama ilivyokuwa ikielezwa.

“Anakula na kufanya kila kitu mwenyewe na hata jioni hii nimeongea naye, anakula kila kitu, hivyo Watanzania wasiwe na wasiwasi juu ya afya ya Maalim Seif,” alisema Mazrui.

Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa waliwasili katika hospitali hiyo kumjulia hali akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba.

MY TAKE: Kwa maoni yangu Seif Shariff anapaswa kupumzika siasa ili aangalie afya yake kwa sasa ikiwa ameukosa urais kwa awamu tano ni kheri akapumzika siasa haswa katika kipindi hiki cha ugonjwa.
 
Kaka kama unafikiri vizuri utagundua kwamba huwezi panda ulingoni alafu ukaomba poo utapewa za uso,maalimu anamalizia alichoanzisha. Hawezi kukubali kirahisi tu itakua si sahihi hata kidogo ila pia ujiulize ni kwa nini itokee kurudia uchaguzi Zenji peke yake na sio Nchi nzima.
Ni kwa nn waangalizi wanasema ulikua poa ila tume inasema tofauti
 
Kwa maoni yangu Seif Sharif anapaswa kupumzika siasa ili aangalie afya yake kwa sasa .

Sio yeye tu hata Lowasa anatakiwa kupumzika siasa kwa sababu za kiafya ajitibie.

Tatizo hao watu wangependa kupumzika siasa ila kuna wahafidhina ndani ya hivyo vyama wasiojali afya za Lowasa na Seif ndio wanawaburuza kuwa wabaki kwenye siasa na hata ikiwezekana waende kwenye majukwaa ya siasa wakiwa wana drip NA CHUPA ZA OKSIJENI na wako kwenye vitanda vya ICU.

UKAWA hurumieni afya za Lowasa na Maalim SEIF wapumzisheni jamani.Nyie UKAWA ni wauaji kama hamjali afya za viongozi wenu mnawapandisha hata majukwaani wakiwa hoi bin taabani hivi mngepewa nchi mngejali afya za watanzania?
 
Kuna kiongozi ambaye ambulance iliongezwa ktk msafara wake na kila akisimama walinzi wawili nyuma.Afya zawatu tuziache na la maana tuwaombee Mungu.
 
Nini hasa anachoumwa maalim seif?
Maana nimesoma sehemu fulani jamaa wa Cuf wanaolalamika pia kuhusu ugonjwa wa kiongozi wao

=======≠===================
LAWAMA KWA VIONGOZI
WETU

Tumepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kuugua ghafla kwa kiongozi wetu mpendwa Maalim Seif. Wana CUF wote twamuombea dua apone haraka..Amin.

Pamoja na taarifa hizo na dua zetu kwake...Bado tuna malalamiko ya kutoridhishwa na tabia ya viongozi wetu mbalimbali wa CUF kutotupatia taarifa sahihi za maradhi ya Maalim. Mara nyingi twaambiwa aumwa miguu...leo hii taarifa zasema kanpooza...mara ana upungufu wa damu...tushike lipi? Twambieni ukweli? Maana hili la kupooza ndio litusumbualo.

Sisi ndani ya CUF na hasa vijana tunaokipa chama uhai...twatakajua Maalim aumwa nini? Na uko Hindu Mandal hali kiukweli hasa
ikoje..?? Kwa taarifa za kihospitali mtwambiayo ya Damu si kweli...kuna zaidi ya hapo mtwambie ukweli tuwe na amani ya nafsi...Mambo ta kuziba ukweli kwa siasa tupunguze sasa maana Maalim kuumwa aumwa!! Twambieni ukweli acheni Siasa. Mtu kupoteza fahamu na kuhudumiwa kwa Wheel Chair si ugonjwa mdogo. Tupeni ukweli wa afya yake hofu ituondoke...tunaomba viongozi wetu wa CUF....Tunasubiri..

Pole Maalim...twakuombea kwa Mungu utoke ICU na upone haraka. Amin.
============================
Inaonekana kuna kitu si cha kawaida kuhusu ugonjwa wa maalim seifu,kikubwa tumuombee mungu tu.
 
Aiseeeee mbaya sana, wamfanye aumwe tu lkn asife, wakimmalizia hakika zenji patakuwa zaidi ya Syria
 
20160308_043445.jpg

Kwa maoni yangu Sef Sharif anapaswa kupumzika soiasa ili aangalie afya yake kwa sasa ikiwa ameukosa urais kwa awamu tano ni kheri akapumzika siasa haswa katika kipindi hiki cha ugonjwa.
Kwanini Shein asipumzike ukizingia kishawahi kuwa makamo wa rais hata kuwa rais kamili?
 
Sina hakika na maelezo yako. Vipi UHURU, vipi TANZANIA DAIMA, Vipi NIPASHE
Kinakua no professional kikiandika yanayomfurahisha toilet paper kikiandika yadimfurahisha. Sawa na majarida ya kubenea wrngine wanayafia wengine wanayabeza
 
20160308_043445.jpg

Kwa maoni yangu Sef Sharif anapaswa kupumzika soiasa ili aangalie afya yake kwa sasa ikiwa ameukosa urais kwa awamu tano ni kheri akapumzika siasa haswa katika kipindi hiki cha ugonjwa.
Ww Ndiye Dkt. Uliyemtibu!!?? Kwani Kuugua Kwake Na Kugombea Nafasi Hiyo Vinahusianaje Kwa Kwa Kuhesabu Vipindi Alivyogombea!!!! Ikiwa Kama Dkt Wake Hajamshauri Hilo, Ww Msukule Una Uwezo Gani Wa Kuzungumzia Masuala Ya Kitaalamu Na Afya Ya Mtu, Wkt Ugonjwa Wa AKILI Haujapata Tiba Na Ushauri!!!!
 
20160308_043445.jpg

Kwa maoni yangu Sef Sharif anapaswa kupumzika soiasa ili aangalie afya yake kwa sasa ikiwa ameukosa urais kwa awamu tano ni kheri akapumzika siasa haswa katika kipindi hiki cha ugonjwa.
Seif hana utofauti na akina Mugabe kwani hataki kurithisha na wengine wagombee toka ameanza. Hili la afya yake alishauriwa na madaktari apumzike kwanza kapuuzia eti anafia chama. Duh! Pole mzee.
 
Maalim apumzike Siasa. Alianza na Kina Aboud Jumbe, Mwinyi,Abdul wakeel,Dr.Salmeen, Amani karume na sasa Dr.Shein akubali matokeo Arejee Mchambawima au Kijitoupele kulea wajukuu! Aanze kuwaamini kina Jussa Ladhu.
 
Nini hasa anachoumwa maalim seif?
Maana nimesoma sehemu fulani jamaa wa Cuf wanaolalamika pia kuhusu ugonjwa wa kiongozi wao

=======≠===================
LAWAMA KWA VIONGOZI
WETU

Tumepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kuugua ghafla kwa kiongozi wetu mpendwa Maalim Seif. Wana CUF wote twamuombea dua apone haraka..Amin.

Pamoja na taarifa hizo na dua zetu kwake...Bado tuna malalamiko ya kutoridhishwa na tabia ya viongozi wetu mbalimbali wa CUF kutotupatia taarifa sahihi za maradhi ya Maalim. Mara nyingi twaambiwa aumwa miguu...leo hii taarifa zasema kanpooza...mara ana upungufu wa damu...tushike lipi? Twambieni ukweli? Maana hili la kupooza ndio litusumbualo.

Sisi ndani ya CUF na hasa vijana tunaokipa chama uhai...twatakajua Maalim aumwa nini? Na uko Hindu Mandal hali kiukweli hasa
ikoje..?? Kwa taarifa za kihospitali mtwambiayo ya Damu si kweli...kuna zaidi ya hapo mtwambie ukweli tuwe na amani ya nafsi...Mambo ta kuziba ukweli kwa siasa tupunguze sasa maana Maalim kuumwa aumwa!! Twambieni ukweli acheni Siasa. Mtu kupoteza fahamu na kuhudumiwa kwa Wheel Chair si ugonjwa mdogo. Tupeni ukweli wa afya yake hofu ituondoke...tunaomba viongozi wetu wa CUF....Tunasubiri..

Pole Maalim...twakuombea kwa Mungu utoke ICU na upone haraka. Amin.
============================
Inaonekana kuna kitu si cha kawaida kuhusu ugonjwa wa maalim seifu,kikubwa tumuombee mungu tu.
Ugonjwa ni siri ya mgonjwa na daktari unataka kujua nini? Jambo la muhimu hapa ni dua ili mzee huyu apone aendelee na kazi zake.
 
Tuombe Mungu amlinde, maana likitokea la kutokea wananchi watajua ni mchezo mchafu wa jecha
 
Back
Top Bottom