Mungu amfariji ndugu yetu aliyeachwa, watoto familia na marafiki wote. Ni jambo la huzuni sana. Kikubwa ni kukubali mpango wa Mungu na kuandaa maisha yetu maana hatujui siku wala saa. Tunahitaji kujua ipo siku nasi tutaondoka. Kikubwa sasa ni kujua baada ya kufa unaenda wapi? Kuna uzima wa milele na mauti ya milele. Ukimwamini Yesu utaishi milele na usipomwamini Yesu utaenda katika mauti ya milele.
Tukilitambua hilo, Mungu atusaidie tupate kujua kwamba kuishi ni mara moja na baada ya kifo ni hukumu. Hakuna matengenezo ya maisha baada ya kufa.Tunapaswa kumpokea kumwamini na kumwishia Yesu. Ili maisha haya yanapokoma, tuwe na sehemu katika makao ambayo alipokuwa akiondoka duniani alisema kwamba anakwenda kuyaandaa. Pale alipo na wamwaminio ndipo watakapo kuwa. Ndiyo maana Yesu alisema yeye ndiye njia kweli na uzima mtu hatakwenda kwa Mungu ila kwa njia ya Yesu.
Mungu tusaidie sana na sisi tuliobaki duniani tuijue na kutembea katika njia yako kwa kumwamini Bwana Yes Kristo.