Maajabu ya wanafuzi wa DIT

Mtoa mada nimemuelewa agenda yake inaonekana ni maajabu kwa lugha iliyotumika na siyo maajabu ya kinachofanyika
 
Kama serikali haitowekeza vya kutosha kwenye sayansi na teknolojia tutaendelea kuona hayo ni maajabu. Supa kompyuta zilianza miaka ya 1960 na teknolojia yake iko mbali sana. Wakati wenzetu wakiwa kwenye nanoteknolojia, sisi tunashangaa kitu walichofanya hao watoto. Serikali na wadau wawe serious na hilo na kuacha mzaha.
 
Tatizo letu ni siasa ndugu, mfano mzuri kuna Kajengo kanaitwa Teaching Tower kanajengwa hapo DIT miaka nenda rudi kapo tu unafikri kuna wachawi
 
hamna lolote hapo, vilaza tu,hicho kitu kipo siku nyingi.
 
Tatizo letu ni siasa ndugu, mfano mzuri kuna Kajengo kanaitwa Teaching Tower kanajengwa hapo DIT miaka nenda rudi kapo tu unafikri kuna wachawi
Ni kweli kabisa, siasa imechukua mahala pa wataalam. Nchi hii ukiwa mwanasiasa hata kama ni std 7 unafikiri unajua kila kitu na kutoa maamuzi bila ya kushirikisha wala kusikiliza wataalamu. Nchi za asia zinazoendelea ni kwa sababu ua uwekezaji mkubwa kwenye sayansi na teknolojia na kupunguza siasa kwenye mambo ya msingi. Vituo vyetu vya utafiti haviko vizuri kwa sababu serikali haitoi pesa na wanategemea kuandika proposals kwa wahisani. Hatutofika
 
DIT ni chuo ambacho kinasemekana kinaongoza kwa Technology Tanzania angalia maajabu ya kitechnolgy wanayofanya hapa

Elimu ya hapa ni imara kwenye technical issues, but shida ipo kwenye kumfanya mwanafunzi kuto kuwa na understanding capacity kubwa kwenye taaluma husika,
 
"Ok watchers" [emoji39][emoji39][emoji39][emoji39][emoji39]
 
Mkuu hiyo miaka ya 1960 ni majuz. Kuna mifumo ya umeme pale Uingereza/Europe at large ipo tangu miaka ya 1880 huko,sisi hadi leo hatuna.
 
Mi nina experience kuna lecture waliosoma master's nje lugha ya malkia ilikua ni shida class. Siwatetei hao vijana ila wanapofanya demonstration juu ya supercomputers ni jambo jema maana mitaala ya DIT inaonekana inaenda na wakati na practical wako poa mi hadi namalizia chuo hatukuwahi oneshwa router, switch na device nyingine bila we mwenyewe kupanda kujifunza. Tusilaumu kila kitu kuna watu wakubwa wenye nafasi kubwa kuongea dakika kumi fluent kimalkia ni utata
 


mimi nimetoa comment kutokana na wao walivyokuja kujitangaza

unajua maana ya neno MAAJABU

yaani ni kama something ambacho wao ndio wamegundua.,, nilitegemea kuona something HUGE kumbe ni hiyo pathetic SUPER COMPUTER nilitegemea kuona maybe wamegundua 10K camera or something...

sasa hivyo watu wanafanya sana na yet sio maajabu ni vya kawaida sana
 


sio kama hauoni changes ni kwamba wanaajiriwa na makampuni makubwa ya technologia wakiboresha kampuni hizo mfano

ninawajua wabongo wanne wa MIT ninawahifadhi kwa majina

mmoja yuko

Qantas Airline (Australia)
mwingine yuko Google

mwingine sijui alipo

na mwingine yupo CBS
 
....ok sawa ila kwa taarifa yako tu Maxence Mello naye kasoma hapo hapo DIT.
Kusoma DIT sio kitu wala kufanya Degree MIT sio kitu.. Kitu Ni Wewe mwenyewe unasimamaje kwenye uwajibikaji wa kile ulichojifunza au unachojifunza. Tupo mtaani na tunafanya vitu vya walioenda skul. Maarifa yanaanzia kwako kabla hujayapata kwingine
 
Melo mwenyewe kasoma DIT, DIT wako vizuri mkuu
 
....nini wewe;
..anza we kuwa serious kwanza kwa kupost tena hii post yako kwa ung'eng'e!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…