Babu wa Kambo
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 559
- 808
Miongoni mwa viumbe wanaonishangaza dunia hii ni pamoja na Wabunge wa CCM, kila siku wanatuonyesha maajabu mapya
Hivi majuzi ulipitishwa utaratibu kwa Wabunge wa UKAWA wanaotoka nje baada ya kuingia kwa Naibu Spika kwamba wakatwe Posho, baada ya kutangazwa utaratibu huu walipiga meza mpaka basi
Sasa ninalojiuliza mimi na wengine wenye akili timamu, hivi ni nani hasa anayepaswa kukatwa Posho kati ya hawa Wanaoingia na kutoka Bungeni kwa hizi siku mbili tatu kuonyesha kutoridhishwa kwao na matumizi mabaya ya kiti cha Spika kwa maslahi binafsi (ya chama) badala ya Taifa na wao wanaokaa tu kujaza nafasi mwanzo wa mwaka mpaka mwisho wa mwaka na wakisimama wanatuambia tuweke Sanamu la Diamond Posta?
Haya binafsi yananishangaza na kunifanya nione kama kuna haja ya kuwaongeza Wabunge hawa kati ya maajabu tunayojivunia Tanzania ili kila mgeni aje ashangae
Wabunge wa UKAWA wanaonyesha utii wa Sheria na wanafanya hayo kwa maslahi ya Taifa na wakirudi ni wazungumzaji wazuri kwa maslahi ya Taifa na huu ni utaratibu wa kawaida, sasa hawa CCM wanaokaa kujaza mabenchi tu mle Bungeni wanafanya hayo kwa maslahi ya nani? Kwa nini hawaombi kukatwa posho? Haya kweli ni maajabu, ina maana watu wazima wale hata hawajishtukii?
Ilikuwa hivi hivi kwenye BUNGE MAALUM LA KATIBA, walikaa kujaza mabenchi na hata walipojadili walijadili kama wanatengeneza Katiba ya Chama chao cha Lumumba mawazo yao yakiwa kwenye Posho ya Milioni 30 lakini sasa yako wapi, wametuingiza hasara kwa kitu ambacho wao wenyewe wanaona aibu hata kukiongelea. Jamani, "mtu mzima ukivuliwa nguo chutama". Waone aibu basi, au wanadhani bado tuko Tanzania ya miaka ya 60 kwamba hatuwezi kuchanganua?
Kwanini hawa wanakimbilia kuongelea Posho badala ya nini kinachowatoa nje UKAWA, au hoja za wananchi kudhalilishwa kwa kufukuzwa mashuleni kama Mbwa wao haziwahusu?