Maajabu ya vichaa: Wanakula vichafu lakini hawaumwi

Naughty by nature

JF-Expert Member
Jan 22, 2023
2,128
2,356
Hivi wakuu, ni sayansi au ni kitu gani au wana kipi special wendawazimu na vichaa, kiasi kwamba wanakula vyakula vibovu majalalani, lakin kamwe hawaumwi typhod fever wala cholera,

Jana nilikuwa Morogoro kule hospitali ya mkoa nikakutana na kichaa mmoja, yule kichaa tangu utoto wetu,mpaka sasa naendea 45yrs, nimestaajabu jana kumkuta hai na yupo bonge vilevile.

Hebu wanasayansi uchwara kina Kiranga watuambie kuhusu ili, maana wanatukanya tusiseme nikaz ya Mungu
 
Maradhi yanaanzia akili ukidhani unaumwa utaumwa kweli
Tumekunywa maji ya mtoni lakini sikuwahi kusikia typhoid kijijini kwetu...
Yap nilikuwa nahisi dalili zote za marelia.

Nikaenda KUPIMA nikaambiwa sina marelia.

Nikameza DAWA TATU. nikalala keshoyake nimeamka nikawa nimesahau kabisa kama nilikuwa na dalili za marelia basi ikawa imeisha hiyo mpk now nadunda

Fact ni kuwa mwili wa kila binadamu unauwezo wa kujitibu wenyewe ni vile wewe utakavyoweza seti MIND yako basi na zile TEZI NEVA UBONGO zitareact vile wewe unavyohitaji
 
Iv wakuu, ni sayansi au ni kitu gani au wana kipi special wendawazimu na vichaa, kiasi kwamba wanakula vyakula vibovu majalalani, lakin kamwe hawaumwi typhod fever wala cholera,


jana nilikuwa morogoro kule hosp. Ya mkoa nikakutana na kichaa mmoja, yule kichaa tangu utoto wetu,mpaka sasa naendea 45yrs, nimestaajabu jana kumkuta hai na yupo bonge vilevile,..ebu wanasayansi uchwara kina Kiranga watuambie kuhusu ili, maana wanatukanya tusiseme nikaz ya Mungu
Hawana majukumu, hawawazi, hawana stress, hawateswi na mapenzi

Sasa kwanini wasinenepe?
 
Mambo Mengi ya Binadamu yapo set up in mind

Huyo kichaa once anaanza kula jalalani lazima Mwili uli-react na kuumwa ila siku zinavyozidi kwenda ile hali inapokelewa na Akili na Mwili na kukitafsiri chakula kichafu Kama kisafi

Then kuhusu hao vichaa wengi huwa wana life expectancy ndogo wengi hupoteza MAISHA kwa umri Mdogo .

Maana unaweza muona mtu mnene Kama unavyosema mtoa Mada lakini hakawa na Afya mbovu Sana , hivyo kusema vichaa hawaumwi nadhani sio Kweli Hawa watu huwa wanaumwa ikifika Muda wake na huwa wanakufa sema kwa idadi Yao ni ndogo na hakua anayewafatilia basi ni ngumu kulifahamu hili jambo.

Wakuu tujitahidi kuwa makini na Afya ya Akili hili tatizo linatesa na kuua ndoto zetu vijana kwa wazee , Kuna watu ukiwatazama kwa nje They are looking good ila upstairs has already shaken .
 
Hofu ndio ugonjwa mkubwa sana duniani.

Ukitaka uishi kwa amani basi epuka kuwa na hofu. Hofu ndiyo inayoongoza kuua duniani.

Maradhi mengi tunayapata kwakuwa na hofu.

Kichaa mfumo wake wa ubongo hauna hofu hata kidogo nandomana anaweza kula chochote asidhurike.

Mtu mwenye akili timamu kwenye ubongo kuna kitu kinaitwa hofu, ukila kitu kichafu lazma udhurike kwaajili ya hofu.
 
Back
Top Bottom