RockSpider
JF-Expert Member
- Feb 16, 2014
- 6,859
- 2,758
Kuna mambo mengi uliyoandika sikubaliani na wewe.
Mwaka 1975 kweli uchumi wa Tanzania ulikuwa mzuri, kwa mwaka ule kutokana na bei ya kahawa kupanda sana baada ya kahawa ya Brazil kuungua kwa baridi 1974. Mwaka 1973 na 1974 uchumi wa Tanzania haukuwa mzuri kabia kutokana na kupanda sana kwa mafuta- Petroleum.
Hata kabla ya vita vya Amini mambo hayakuwa shwari sana. Vitu madukani mara nyingi vilikuwa vinakosekana hasa hasa, unga, mchele, mafuta ya kupikia, sabuni, n.k.
Nyerere aliondoka madarakani akiiacha Tanzania ikiwa hoi kwelikweli kiuchumi. Benki Kuu walikuwa hawana hata dollar millioni moja!
Alipoingia Mwinyi alikuta mambo mazito. Mwanzoni tu nchi nzima ilikuwa haina kabisa mafuta (hiki kilikuwa ni kitu cha kawaida wakati wa JKN). Ilibidi kusaini mkataba na Waarabu kubadilishani kahawa na mafuta. Mwinyi alijaribu kufungua uchumi wa Tanzania lakini walionufaika walikuwa ni wachache sana na kodi hazikulipwa. Tanzania ilibanwa sana na World Bank, IMF, na nchi wafadhili hasa kutokana na deni kubwa lililokuwa linaisonga Tanzania.
Mkapa alipoingia alijitahidi kulipa madeni kusudi angalau nchi ikopesheke. Ukata (Ukapa) uliumiza wengi lakini baada ya hapo madeni yalisamehewa madeni mengi. Migodi mingi ilifunguliwa na mashirika mengi yaliuzwa. Kwenye migodi kwa kweli Watanzania hawakunufaika sana lakini vile vile hili lilitokana na shinikizo la World Bank na IMF waliotaka Tanzania ifuate model ya nchi kama Chile. Uuzaji wa mashirika ulikuwa na matatizo yake lakini binafsi nakubaliana naye 100%. Mashirika na viwanda vilikuwa ni mzigo mkubwa kwa wananchi. NBC ilikuwa ni mzigo mkubwa kwa wananchi. Serikali ilikuwa haipati kodi kutoka NBC. Sana sana NBC ilikuwa mbele kuchangia mikutano ya NEC ya CCM kule KIzota na sherehe nyingin za chama. Afadhali ilikufa! Leo wanalipa kodi na serikali inapata gawio la faida.
Mkapa alifanaya vizuri sana sana katika kuinua uchumi wa Tanzania. Kikwete alipoingia madarakani alikuta mwanga na hewa safi katika uchumi wa Tanzania. Forex Reserves aliyoacha Mkapa ilikuwa kama USD 4 bn na Export zilikuwa juu kuliko alipochukua nchi.
Marais walioingia madrakani wakiwa na wakati mzuri ni Nyerere na Kikwete. Nyerere alichukua nchi ikiwa maskini lakini system zote zilikuwa zinafanya kazi. Kikwete amechukua nchi ikiwa katika hali afadhali kiuchumu kuliko wakata Mwinyi na Mkapa wanaingia madarakani.
Samahani kwa ujumbe mrefu.
Mkuu hapo ndipo penye shida kubwa sana... Tuna ongoza ku-export Diamond, Gold, Nickel, Tanzanite, Ruby, nk Lakini mapato hayaonekani! Why? Mikataba mibovu ya Mkapa!!!! Grrrrr Tumebinafsisha TIPER na sasa hatuna uwezo wa kudhibiti mfumuko wa Bei ya MAFUTA! Why? Mkapa ameuza TIPER na sasa tuna nunua mafuta kutoka kwenye makampuni ya Ulaya badala ya kuingia mikataba na nchi zenye mafuta kama Iran et al... Mkuu JK hakukuta fedha hazina, Zile zilikuwa mbwembwe za IMF & WB zilizokuwa zinaficha mauchafu ya Mole wao Mkapa... Mkuu hata ukijaribu kupaka rangi bado itabaki kuwa MKAPA ameuza nchi yetu ....