MAAJABU ya Tanzania- Tunachemsha yai kupata omelet

Sungurampole

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
984
205
Wakati mwingine nashangazwa sana na 'maajabu ya Tanzania' na mchango wa wasomi wetu kutuonesha njia.

Huenda tungeomba Tanzania ingeizwa katika maajabu saba ya dunia' kwa “ombwe la uongozi” badala ya kuombea mlima Kilimanjaro tungefaulu.

Hivi ukiwa Mrengo wa kijani unapata upofu fulani kiasi hata ‘basic faculty’ zako zinavia?

Siamini nikiwasikia wasomi wetu na michango yao katika kutoa majibu ya maswali ambayo hata mwerevu wa kawaida asiyefuta ujinga anaweza kujibu.

Eti Prof Kabudi akitetea mchakato mbovu wa kupata katiba ya wananchi anasema tunaweza kuchemsha yai vizuri tukapata Omelet, Prof Ndulu anasema pamoja na kukosa umeme uchumi wetu unakua kwa kasi ya kutisha. Pro Ndulu anatuambia tunauza dhahabu kwa wingi nje lakini hatuna forex. Pro anasema ubovu wa wazi wa noti mpya ni matokeo ya kuhidhiwa vibaya.

Dr. Kikwete anasema hajui kwa nini Tanzania ni maskini japo katumia nguvu zote kupambana ili apewe kuiongoza.
Dr. Hosea anasema kuwa Richmond iko Powa, Dr Mwakyembe anasema Richmond hewa na Dr. Jk anakubali taarifa zote wala haoni kuwa kuna haja ya kumwajibisha mtu.
'Dr' Feleshi anasema mwenye ushahidi wa Kagoda ampelekee, anapewa anasepa
'Dr' Luhanjo anasema kutumia pesa kinyume na mipango ni jambo la kawaida serikalini. Cha kufurahisha ni kwamba ni jambo la kawaida kiasi kwamba Waziri Mkuu wa Serikali hiyo hiyo halijui.
CAG - Utouh anachunguza ukiukwaji wa taratibu anatoa taarifa kuwa kiasi kilichotuhumiwa na idadi ya makampuni yaliyoamrishwa na Jah Hero yamekosewa na aliyetoa tuhuma hivyo mambo powa.
Msomi wetu wa sheria na katiba Mh Kombani anasema muswada uliowasilishwa bungeni April 2011, ulikua mzuri kabisa tatizo ni Chadema kuupotosha, baada ya hapo anaenda kuufumua (kuuoverhaul) muswada huo. Hivi kama shida ni kupotoshwa unaufumua muswada au unauelezea kuondoa upotoshaji?

Hivi tumekosea wapi- wasomi wetu?

Na

Tufanye nini turudi katika mstari?
 
Nilitarajia na majibu pia au hata njia ya kupita, kulifahamu tatizo tu bila kuwa na namna, wazo au nia ya kutatua ni tatizo.

Mjenga hoja, tunafanyaje kama nchi kupata omelete?

Nivumilie kwa kukujibu kwa swali, bahati nzuri swali lako linakaribisha maswali zaidi.
 
Hilo ni letu wote - nafikiri kujua swali ni mwanzo wa safari ya kutafuta sulhisho au jibu

Samini katika kuwa mkiritimba wa mawazo yangu - haina sina mawazo yangu juu ya haya

Karibuni tutafakari kwa pamoja
 
Back
Top Bottom