Maajabu ya simu mpya itel S12

Maajabu ya simu mpya itel S12

Wanjiro

Member
Joined
Oct 27, 2016
Posts
55
Reaction score
110
Kuelekea sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya Itel mobile imeachia simu mbili kali mpya ni S12 na S32 zenye kamera mbili za mbele huku kila kamera ikiwa na kazi yake maalum.

Kamera mbili za mbele


Unaposikia simu ina kamera mbili za mbele unaweza kutamani kufahamu zaidi kuhusu simu hizi pamoja na matumizi yake, lakini kwa sasa utafahamishwa sifa muhimu za itel S12 kwanza.

itel-S12.jpg


Kitu kinachotofautisha itel S12 na simu nyingine ni kamera zake mbili za mbele ambazo kila mojawapo ina kazi ya kupiga picha tofauti na nyingine.

Moja inakuwezesha kupiga selfie ya kundi la watu wengi zaidi yaani group selfie kwa upana mkubwa au wide angle unaofikia mpaka nyuzi 86⁰, kamera hii ambayo ina MP5 inasaidia ukiwa mahali na watu wengi na wakati huohuo unahitaji ndugu jamaa na marafiki wote ulionao hapo mtokee kwenye picha moja ya kumbukumbu basi hapo unapaswa kutumia kamera hii.

Kamera nyingine ni mahsusi kwaajili ya upana wa kawaida, mathalani ukiwa peke yako au wawili unatumia kamera hii ili picha yako ya selfie itoke ikiwa ang’avu iliyojitosheleza vizuri kwenye screen yako. Kamera hii yenye MP2 ina uwezo wa kupiga selfie yenye angle pana kufikia nyuzi 63⁰.

Kamera ya nyuma

Hautaishia kwenye selfie pekee kwani S12 imekuja na kamera ya nyuma yenye MP8 ikiwa na outofocus kwa picha za kawaida na pia ina filters amabazo ukiwa umefungua kamera zinakusaidia kuangalia picha yako itaonekanaje ukishapiga.

Kuhusu Fingerprint

Pamoja na kwamba S12 imeundwa kwa kamera mbili za mbele, pia ina fingerprint inayokuwezesha;

i. Kupiga picha kwa kubofya fingerprint

ii. Ku-unlock simu

iii. Kumrekodi mtu unayeongea nae kwenye simu

iv. Kupokea simu unapopigiwa

v. Kurekodi video

Umbo la simu hii

Kinachofurahisha zaidi itel S12 ni nyembamba sawa na upana wa vipande thelathini vya karatasi za rimu vilivyobebana. Hii inafanya usichoke kuwa nayo kiganjani mwako nyakati zote kutokana na fasheni yake ya kuvutia. Ina rangi tatu; Nyeusi, Champagne Gold na Moonlight silver.
 
Itel na tecno sijui iweje mpk nije kuzitumia
 
Itel na Tecnl ni simu za majaribio, bado kufikia kiwango cha ubora wa smartphones kuhusu picha, mtandao, betri, mwanga, spidi, nk.
 
Back
Top Bottom