Maajabu ya popo

Maajabu ya popo

kisungu

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2013
Posts
788
Reaction score
266
popo add.jpeg
Popo ndio mnyama pekee anayeweza kuruka (fly) kama ndege, mara nyingi anatembea usiku, na huwa anakula wadudu wadodo wadogo, watu wengi wanadhani kuwa popo haoni kwa macho ila ukweli ni kwamba anaona vizuri kushinda hata wanyama wanaotembea mchana.

Popo anawezaje kuwakamata wadudu usiku? hii ni changamoto, ila popo amejitengenezea aina ya mawimbi ya sauti yanayomsaidia kuwinda, njia hii inaitwa echolocation. Hii inafanyeje kazi, kama ulishawai kutoa sauti kubwa kwenye pango huwa sauti inakurudia, vivyo hivyo na popo ndivyo inavyokuwa.

Maajabu yake..!

Popo ndiye mnyama pekee anayetoa hii sound waves duniani, cha ajabu ni kuwa hii sound wave inayotolewa na popo ni kubwa sana kushinda sauti zote hapa duniani na ipo nje wa uwezo wa binadamu kuweza kusikia, hapa ina maana ukisikia unaweza kuwa kiziwi au ukafa kabisa, hii sauti ikigonga kitu kiwe mti au mdudu inarudisha taarifa kwenye ubongo na kutafsiri na popo anakuwa tayari amejua ni kitu gani hicho.

Pia anaweza kujua umbali wa hicho kitu kwa haraka sana.
Ukipima frequency ya sound waves ya popo ni makadirio kuanzia 14,000 mpaka 100,000HZ ambapo binadamu ana uwezo wa kusikia kuanzia 20 mpaka 20,000HZ. Tofauti ni kubwa sana.

Popo mmoja anaweza kula hadi mbu 1,200 kwa saa moja
 
Duh! Sasa kwani huwa anajining'iniza miguu chini kichwa chini,mbona huwa akiingia ndani ya chumba anajigonga gonga kwe ukuta?
 
Kumbe popo wanaweza kutumika kuzuia uzalianaj wa mbu na kupunguz malaria
 
Ushasema anaruka,

Halafu unasema anatembea usiku!

Tukueleweje hapo?

Msema kweli ni wewe au popo?
 
Nadhani popo sio mnyama pekee anaeweza kuruka. Kuna wanyama wengine kama nguchiro ila wao ni qadogo kidogo nao wanaruka kama kawaida (google.. flying mamals)
 
Jamani nisaidieni dawa ya kudumu ya kuua popo wanatuharibia nyumba zetu, mwenye dawa ya kuwaangamiza tafadhari
 
Kisungu hongera ingawa hapa katika udadavuaji wako hujaeleza ni aina gani ya popo.. mimi ni mdau wa mambo haya ya study za viumbe ila kwa kukusaidia tu ni kwamba popo unaemzungumzia anaitwa Black Winged Bat yeye ni insectivore yaani anakula wadudu wadogowadogo na saizi ya kati.sasa ukisema popo unakuua too general ingawa wanaojua mambo haya watapata kufahamu intention yako lakini kwa wasiojua itakua kama vile unawapa taarifa zisizo sahihi.. ni mchango tu ndugu tangu
 
Je popo anaona au anatumia hiyo echolocation kugundua hapa kuna tu au ukuta ?
 
Kisungu hongera ingawa hapa katika udadavuaji wako hujaeleza ni aina gani ya popo.. mimi ni mdau wa mambo haya ya study za viumbe ila kwa kukusaidia tu ni kwamba popo unaemzungumzia anaitwa Black Winged Bat yeye ni insectivore yaani anakula wadudu wadogowadogo na saizi ya kati.sasa ukisema popo unakuua too general ingawa wanaojua mambo haya watapata kufahamu intention yako lakini kwa wasiojua itakua kama vile unawapa taarifa zisizo sahihi.. ni mchango tu ndugu tangu

eti yule popobawa yupo kundi lipi ??
 
Back
Top Bottom