Maajabu ya Nyumbu na Uwezo wa Kuihifadhi Mimba Iliyokomaa Kwa Siku 90 Kusubiria Mazingira Wezeshi

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,681
119,318
Wanabodi,


Haya ni baadhi ya maajabu ya uwezo wa badhi ya viumbe hai, wana uwezo mkubwa kuliko binadamu.

Kwa wale mnaokumbuka kufuka kwa moshi wenye majivu mazito kwenye mlima Oldonyo Lengai miaka kadhaa nyuma, wanyama wote wa porini walilikimbia eneo hilo wiki moja kabla ya tukio hilo, lakini mifugo inayofugwa na binadamu, ng'ombe, mbuzi na kondoo ndio wqlioathirika.

Jee wanyama wa porini walijuaje kuhusu hatari iliyo mbele yao hivyo kukimbia kabla, wakati mpaka kesho, binadamu bado hana uwezo wa kutambua majanga ya asili (natural disasters) kabla hayajatokea.

Sikia hii kubwa kuwahusu wanyama nyumbu.

Nyumbu wa kike huwa wote wanapandwa kwa wakati mmoja tuu wa mwaka, na katika eneo maalum la kupandwa na wote hushika mimba kwa pamoja kipindi hicho. Yaani ni mahali maalum kama chumba cha baba na mama.

Hivyo kabla muda wa kupandwa haujafika, maelfu kwa maelfu ya nyumbu hutoka mbio kutoka nchini Tanzania katika mbuga ya Serengeti na kuhamia katika mbuga ya Masai Mara nchini Kenya kwenda 'chumbani'
kutengeneza watoto.

Tukio hilo hujulikana kwa jina maarufu la Serengeti Migration na ni kivutio kikubwa sana kwa watalii kutoka pembe nne za dunia kukusanyika Serengeti, kushuhudia tukio hilo.

Chumba cha baba na mama kwa Nyumbu ni eneo dogo linaloitwa Ndutu ambapo nyumbu zaidi ya milioni moja hukutana hapo mwezi February na hukaa na ujauzito kwa miezi 11, kisha hurudi eneo hilo hilo kuja kujifungulia hapo na kunyosha mtoto kwa mwezi mmoja tuu, kupokea mimba nyingine na kuondoka eneo hilo hadi mwaka unaofuata.

Hivyo ndivyo inavyakuwa kwa miaka yote kila mwaka, lakini kwa mwaka huu hali ni tofauti kufuatia mabadiliko ya tabia nchi yaliyosababisha ukame, kundi kubwa la nyumbu wenye mimba wamekusanyika eneo la Ndutu wakisubiri kujifungua na kutengeneza watoto wapya. Lakini kufuatia hali ya ukame, hakuna majani mabichi machanga, milli ya nyumbu hao wenye mimba kubwa zilizo komaa, imeweka zuio la muda kuzuia watoto kuzaliwa kwa kusubiria kwanza mvua mpaka zinyeshe, majani mabichi machanga yaote ndipo miili iruhusu watoto wazaliwe.

Kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano wa Tanapa, Pascal Shelutete, nyumbu hao, wanao uwezo wa kuzishikilia mimba hizo matumboni mwao hadi kwa siku 90!.

Kiukweli haya ni maajabu ya wanyama hawa.

Hata hivyo bado kuna maswali mengi bila mujibu. Kwenye kundi la nyumbu hao milioni moja, pía kuna swala 500,000 na punda milia 200,000 na wanyama wengine 300,000 kufanya mkusanyiko huo kuwa na wanyama milioni 2. Swali ni jee wote wanauwezo wa kuzishikilia mimba kusubiria mvua kunyesha? .

Paskali
 
Je unajua ya kuwa kila mwaka zaidi ya Nyumbu milion 1 wanavuka mto mara kwenda Mbuga ya Masai Mara Kenya ?

Lakini pamoja na wingi wao wameshindwa kuwafanya Simba wakala nyasi kwa kuua japo Simba wawili kila mwaka naimani mpaka leo Simba wangewaogopa na kuanza kujifunza kula nyasi si nyama tena
 
Wanyama wana uwezo mkubwa sana wakuji control na kujua mabadiliko ya hali ya hewa na majanga mapema kuliko binadamu. So nyumbu nao wana uelewa wao
 
huo utafiti umefanyika lini kwamba climate change imeleta hayo mabadiliko? sample size ni ngapi? huo utafiti umechapishwa wapi?
 
Back
Top Bottom