Maajabu ya Nchi ya Australia

Maajabu ya Nchi ya Australia

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,154
Reaction score
13,267
Robo+tatu+ya+Waustralia+wanaishi+katika+majiji+makubwa+na+maeneo+ya+pwani.+Fukwe+pia+ni+sehemu+za+utambulisho+wa+Australia.jpg

1.Australia ni bara pia ni nchi. Ni bara dogo kuliko yote duniani, na ni kisiwa kikubwa kuliko vyote katika Sayari Hii. Ni Kisiwa kilichoko kusini mashariki Mwa Dunia. Mji mkuu unaitwa Canberra Jiji kubwa linaitwa Sydney na Mbili ya tatu ya bara hilo (kisiwa)/nchi ni Jangwa. Inakadiriwa kuwa na idadi ya watu milioni 24, ambao wengi wao wanaishi katika miji ya pwani. Australia ni nchi inayoongozwa kwa muundo wa ufalme wa kikatiba na mfumo wa bunge la serikali. Kabla ya kuhamia Waingereza nchi hiyo ilikuwa ikikaliwa na wakaazi asilia.

2. Zaidi ya Asilimia 95 ya Raia wake hulazimika kupiga kura kwa kuhofia kutozwa faini ya dola 20 iwapo hutapiga kura na tozo huzidi iwapo utashindwa kulipa faini hii yaani ni KERO tu

3. Ukidhani Watanzania wanabeti umeingia chaka kwani Australi ndiyo nchi inayoongoza kwa Kamari duniani ikiwa zaidi ya 80% ya Raia wake wanacheza michezo ya kamari

4. Huenda Umesoma kuhusu 'Kondoo Australia' kwenye jiografia, ukweli ni kwamba kuna Kondoo wengi kuliko hata wanaume wote wa nchi hiyo. Idadi ya Kondoo wote ni milioni 150 ilihali wanaume wote ni milioni 20 tu na hao pia ni mara tatu ya watu wote wa Australia............

5. Hii ni nchi yenye wakazi wachache duniani ikiwa ni uwano wa watu wawili kwa kila kilomita ya mraba ilihali Japan ina wakazi 327 kwa kilomita ya mraba. Robo ya wakazi (26%) wa nchi hiyo wamezaliwa nje ya Australia......yasemekana 70% ya Waaustralia asili yao ni waingereza... hata hivyo Kuna wimbi la kutaka kuandika upya historia ya Australia kwani iliyopo inapotosha. Wanafunzi wamekuwa wakihamasishwa kukwepa baadhi ya maneno yaliyopo kwenye historia ya sasa. Wanatakiwa kusema wakoloni au wavamizi badala ya wakazi wapya au wagunduzi na wavumbuzi. Kabila la Aborigines, wakazi wa awali hawakupewanafasi husika katika historia ya sasa. Waliishi hapo kwa makabila mbalimbali na hivyo kuijua nchi hiyo kabla wa wageni.

6. Uzio wa Dingo ndio mrefu kuliko yote duniani ukiwa ni mara mbili ya Ukuta mkuu wa china

7. Nyumbani kwao wanyama waitwao kangaroo
Kangaroo+hupatikana+Australia+pekee.jpg

8. Licha ya Kupata Uhuru wake mnamo mwaka 1901, Bado Inamkubali Malikia wa Uingereza kama Mkuu wa Dola akiwakilishwa na Gavana Mkuu
Robo+tatu+ya+Waustralia+wanaishi+katika+majiji+makubwa+na+maeneo+ya+pwani.+Fukwe+pia+ni+sehemu+za+utambulisho+wa+Australia.jpg

10. Serikali ya Australia imetangaza kwamba inapania kuwa muuzaji mkubwa zaidi wa bangi ya kutumiwa kwa ajili ya matibabu duniani. Taifa hilo linapanga kufanyia mabadiliko sheria zake na kujiunga na Canada na Uholnazi ambazo kwa sasa ndizo nchi pekee ambazo huuza bangi nje ya nchi.
_99459289_gettyimages-663787336.jpg

"Lengo letu liko wazi: kuwapa wakulima na wenye viwanda wa Australia nafasi bora zaidi katika kuwa wauzaji nambari moja wa bangi ya kutumiwa kwa sababu za kimatibabu duniani," Bw Hunt amesema.
 
Ni Kisiwa kilichoko kusini mashariki Mwa Dunia. Mji mkuu unaitwa Canberra

Jiji kubwa linaitwa Sydney

Mbili ya tatu ya bara hilo (kisiwa)/nchi ni Jangwa

Nyumbani kwao wanyama waitwao kangaroo
 
Ni Kisiwa kilichoko kusini mashariki Mwa Dunia. Mji mkuu unaitwa Canberra

Jiji kubwa linaitwa Sydney

Mbili ya tatu ya bara hilo (kisiwa)/nchi ni Jangwa

Nyumbani kwao wanyama waitwao kangaroo
nimeongeza juu pale
 
pole. ukipata uje utie nyama humu
Mwaka wa pili huu wananizungusha kunipa viza
Wananizururisha tu na bahasha yangu Nairobi
We balozi MUNGU anakuona ujueeee
 
Mwaka wa pili huu wananizungusha kunipa viza
Wananizururisha tu na bahasha yangu Nairobi
We balozi MUNGU anakuona ujueeee
Kaka ukitaka kuomba visa hakuna haja ya wewe kusumbuka ubalozini.

Kwa kuwa unataka kwenda kutalii ni simple sana...tafuta hoteli ya bei nzuri unayotaka kufikia site nzuri ya hotel ni booking.com hapo utakuta hoteli zote na bei yake.

Chagua unayoipenda then fanya mawasiliano nao, waambie utakaa hotelini kwao kwa siku utakazo. Watakuomba docs zako watakufanyia visa na ata ukitaka booking ya ndege watakufanyia.

Pindi utapofika kule utawakuta airport wanakupokea, wewe una pesa hakuna haja husumbuke mteja ni mfalme watakufanyia kila kitu. Wao ndio watakuwa sponsor wako.

Hata unapotaka kwenda shopping china au dubai kama kwa mfano unaenda kununua laptops,j ua duka gani linauza ukifanya mawasiliano nao ata duka kwa kuwa wana leseni wanauwezo wa kukusponsor visa.

Nadhani umeelewa, +971504374387 Dubai!
 
Mwaka wa pili huu wananizungusha kunipa viza
Wananizururisha tu na bahasha yangu Nairobi
We balozi MUNGU anakuona ujueeee
mkuu habari? ukiwa na scholarship ya kusoma australia unapata usumbufu wowote kwenye visa
 
Hivi mji mkuu wa Austria ni Vienna?
Australia ni Canbera? Ahsante sana.

Vipi Vaticani?
 
Hivi mji mkuu wa Austria ni Vienna?
Australia ni Canbera? Ahsante sana.

Vipi Vaticani?
Wa Vatcan ni Vatican city na ule wa Djbout ni Djibout.
By the way, are you a mathematician or an economist?
 
Back
Top Bottom