Maajabu ya mimba ya huyu mwanamke

Maajabu ya mimba ya huyu mwanamke

Azarel

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2016
Posts
29,020
Reaction score
40,793
Habarini wadau,

Leo asubuhi niliamka nikiwa na mood mbaya ila wakati nakunywa chai nikajikuta naanza kucheka sana na kila nikikumbuka najikuta nacheka tu hata kimoyoni.

Ni hivi nina kaka yangu, ni mtu mzima tu na alishaoa na kuwa na mtoto mmoja na sasa mkewe ni mjamzito hivyo anatarajia mtoto wa pili.
Asubuhi nimempigia simu mama kumjulia hali, baada ya maongezi mafupi akaniambia kwa kilugha

"Hivi wewe huwezi kupiga nyumba rangi?"

Nikamwambia hapana mama, mara akaniambia

"sasa si ukaongee na kaka yako kuhusu huyo mpiga rangi?"

Akaongeza..."Nyie ni watu wazima sasa msinisumbue" akakata simu.

Ikabidi nimpigie kaka kujua kuna nini juu ya mpiga rangi.
Kumbe bana wiki mbili zilizopita alimleta mpiga rangi kwenye nyumba yake kwaajili ya kubadilisha rangi sebuleni kwake.

MAAJABU:
Mke wake (shemeji yangu) ambaye ni mjamzito aliipenda sana harufu ya ile rangi ya ukutani na kila mara alipenda kukaa sebuleni siku nzima tena karibu na ukuta kabla rangi haijakauka.

TATIZO LILIPOANZIA:

Mke wa brother alichukua namba ya simu ya fundi rangi kumbe akawa anamwambia mara kwa mara

"Fundi si uje kurudia rangi koti nyingine jamani" kwani nilikufukuza kwangu? Na alikuwa akimkumbusha mara kwa mara na mume wake akaja kuona messages ila hakumuuliza chochote.

Sasa mtoto wake kachafua ukuta kwa kuchora chora ndio kaka kaja juu kuwa mke wake ndio kachafua kwa makusudi ili nyumba ipigwe rangi na fundi yule yule. Jana alipomtembelea mama jana ndio akamwambia anahisi mke wake anamsaliti kwa kutembea na fundi rangi.

Sasa mama anachosema ni kwamba "mimba" yake ndio imependa hiyo harufu hivyo kaka aache kulia lia. Hivi Kweli mimba ya mwanamke inaweza kupenda harufu kali kama hiyo ya rangi na wakati inaletaga hadi mafua?
Najua mwanamke akiwa mjamzito anaweza kupenda harufu ya dagaa ama malimao.

Ila Rangi?
 
Kaka mimba huwa inawafanya hawa wanawake wafanye vitu vya ajabu kabisa... yaan anaweza kusema anataka kuku wa kuchoma. Ukamletea.. ile tu unafika mezani.. anasusa ..anakwambia anataka ndizi.
Yaani ni kuvumilia tu.. ni kipindi cha mpito
 
Kuna dada mmoja alichukia deodorant za wanaume wote wa kazini kwao, kila siku akija ofisini tu anaanza kutapika. Sasa utawaambia watu waache kutumia deodorant? Ilibidi aende likizo ya ugonjwa.
 
Kuna mtu mimba yake ilikuwa inapenda mabarafu (maji yaliyoganda)

Breakfast barafu
Lunch barafu
Dinner barafu

Inaonekana mimba ina mambo ya ajabu sana

Nasubiri kuona yangu itapenda nini
 
Kuna dada mmoja alichukia deodorant za wanaume wote wa kazini kwao, kila siku akija ofisini tu anaanza kutapika. Sasa utawaambia watu waache kutumia deodorant? Ilibidi aende likizo ya ugonjwa.
Harufu ya deodorant tena?
Hii hali inawaisha baada ya muda gani wanawake wajawazito?
 
Sitasahau siku niliamshwa saa tisa usiku nikamtafutie embe bichi, nikatoka room nikaenda kulala sebuleni. Asubuhi ndo balaa, akasema nisiende kazini anataka kushinda na mimi nimkumbatie tu. Hizi mimba hizi, sijawahi kuzielewa.
 
Mimba zina mambo mengi. Wa kwangu ni mjamzito yy anapenda tu harufu ya jasho langu, sana sana shati ambalo nimelivaa cku mbili tatu. Yy nikiwa mbali naye basi ndo starehe yake analikumbatia anapopumzika na kulinusa nusa. Mimba zina mambo na vimbwanga vyake hakuna cha kuhisi anasalitiwa. Mwingine kununa tuuu, wivu, hasira au visirani. Cha msingi kuvumilia maana yatapita tu
 
Kuna mtu mimba yake ilikuwa inapenda mabarafu (maji yaliyoganda)

Breakfast barafu
Lunch barafu
Dinner barafu

Inaonekana mimba ina mambo ya ajabu sana

Nasubiri kuona yangu itapenda nini
Joanah yako nahisi itapenda udongo
 
Harufu ya deodorant tena?
Hii hali inawaisha baada ya muda gani wanawake wajawazito?
Inategemea, wengine inaanza wiki mbili tu baada ya mimba kutunga na inaisha baada ya miezi mitatu lakini kwa wengine ni mpaka ajifungue.
 
wifi yangu yeye ilikuwa mwendo wa coca barrdii plus udongo yan ndio breakfast yake kila asbh
 
Back
Top Bottom