Maajabu ya bodi ya mikopo elimu ya juu HESLB

Maajabu ya bodi ya mikopo elimu ya juu HESLB

Deadbody

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2015
Posts
4,292
Reaction score
6,693
MAAJABU KUHUSU MIKOPO YA WANAFUNZI VYUO VIKUU MWAKA2016 .(CONFUSION ABOUT LOAN ALLOCATION TO HIGHER EDUCATION STUDENTS)
1. Wanafunzi wa mchepuo mmoja, wanaosoma masomo sawa, assignment zao zote ni sawa, Lakini pesa ya Field training practicals and stationaries zinatofautiana. ( maajabu haya)
2. Wanafunzi wa faculty/kitivo kimoja lakini pesa ya faculty allowance zinatofautiana. (Maajabu mengine)
3. Wanafunzi wa chuo kimoja, watatumia cafeteria moja, Bei ya chakula itakuwa sawa kwa wote, nauli ya usafiri itakuwa sawa kwa wote, Ila pesa ya Boom zinatofautiana kwa kila mwanafunzi (Ajabu sana hii)
4. Wanafunzi waliopata mkopo Kwa mara ya kwanza inaweza kuwa ndio idadi ndogo zaidi kuwahi kupata mkopo.( i stand to be corrected)

Huku ni kutengeneza matabaka vyuoni, Huku ni kutengeneza kubaguana vyuoni, Huku ni kufanya baadhi ya wana vyuo wajione bora zaidi kuliko wengine. Serikali iangalie Jambo Hili upya na kwa upana wake kuepusha hatari zitakazoambata na maisha magumu ya wana chuo kama nilizo ainisha katika Toleo langu lililopita.
 
ahaa wewe unaona waathirika wa tetemeko kule kagera wanahitaji msaada alafu wewe unajalii kushiba na litumbo lako
 
Yaani mengine muda huu hatukupaswa kuanza kujadiliana,hili la mikopo ya chakula ilipaswa kutekelezwa tu na si kuwaeka watu katika tension namna hii,450? daaaaahhh hiyo si hela ya maji ya kandoro kabisa.Thnx j.k hakika tumeanza kukukumbuka baba yetu ila mbona tumeanza kukukumbuka mapema hiviiiiiii,hivi mwaka huu kuna mtu hajaguswa na madhahama ya kariba namna hii
 
Back
Top Bottom